Kupaua nyumba (Makadirio ya gharama)

Kaka naomba haka karamani?
 
Ni kweli mkuu watu wanafikir kupaua ni kazi ya kitoto.
Kupaua ndio stage ngumu kuliko zote kwenye ujenzi wa nyumba.
Kujenga pagala ni rahisi sana ukiwa na kiwanja.
 
Transporter
Mkuu kwenye mbao hapo mmmm mbona kama rahisi sana any way mi si mtaalamu sana
Kwenye mbao pale amekosea.
Kwa kawaida gharama ya mbao huwa inazidi ya bati.
Na ukichukua mafundi wa bei rahisi sana Kuna hatari ya kuharibiwa nyumba yako.
Nyumba ni kitu Cha kudumu na sio kitu Cha kukifanyia majaribio.
Cha msingi ukijipanga ni kumwita fundi na kupatana usiogope fundi anapotaja pesa kubwa ambayo ipo nje kidogo ya budget yako.
Kwa jinsi nilivyokaa nao mafundi na kuwazoea nimegundua huwa hawana bei maalum bali huwa wanaangalia mazingira kazi ilipo.
Kwa mfano bei wanayotaja masaki/upanga/mbezi beach ni tofauti na bei wanayotaja mbagala/vingunguti/gongolamboto.
 
Ni kweli mkuu watu wanafikir kupaua ni kazi ya kitoto.
Kupaua ndio stage ngumu kuliko zote kwenye ujenzi wa nyumba.
Kujenga pagala ni rahisi sana ukiwa na kiwanja.
Kupaua ni gharama lkn mwenye nyumba usiposimamia inakuwa gharama mara elfu kumi
 
Gharama ya mbao inazidi gharama ya bati?
 
We Jamaa mnyonyaji,otherwise nyumba yako ilikuwa ndogo sana
 
Gharama ya mbao inazidi gharama ya bati?
Ndio hivyo mkuu,gharama ya mbao huwa inazidi kidogo ya bati,naongelea bati za msouth migongo mipana au myembamba.
Kwa mfano Mimi nilivyopaua nilitumia milioni 4 kwenye mbao na milioni 3 kwenye bati.
 
Ndio hivyo mkuu,gharama ya mbao huwa inazidi kidogo ya bati,naongelea bati za msouth migongo mipana au myembamba.
Kwa mfano Mimi nilivyopaua nilitumia milioni 4 kwenye mbao na milioni 3 kwenye bati.
Dah Mie nachoka,ninataka kupaua.Bati nataka kutumia za migongo midogo za Rangi.Mbao nimeibajitia milioni 1.5-2 bati milioni 3-3.6 Sasa hapa kusikia mbao zinakuwa juu nazidi kupagawa
 
Dah Mie nachoka,ninataka kupaua.Bati nataka kutumia za migongo midogo za Rangi.Mbao nimeibajitia milioni 1.5-2 bati milioni 3-3.6 Sasa hapa kusikia mbao zinakuwa juu nazidi kupagawa
Hiyo nyumba yako Ina ukubwa gani ndugu?
Na pia inategemea muundo wa hiyo nyumba yako Ina paa la aina gani,Kama ni ujenzi wa kizamani Kama mgongo wa tembo hapo sawa?
 
UNAPATIKANA MWANZA ?????
 
Naomba unipemakadilio ya nyumba ya 12m urefu na 10.6m upana , angle ni 30 nyuzi na plani ya paa ni kama ilivyo hapo chinj
 
Attachments

  • IMG_20200103_131335.jpg
    31.1 KB · Views: 42
Ndio hivyo mkuu,gharama ya mbao huwa inazidi kidogo ya bati,naongelea bati za msouth migongo mipana au myembamba.
Kwa mfano Mimi nilivyopaua nilitumia milioni 4 kwenye mbao na milioni 3 kwenye bati.
Nyumba ya 12m urefu na 10.6 m upana angle 30 nyuzi paa ni kama hapo chini hutumia bati na mbao kiasi gani
 
Attachments

  • IMG_20200103_131335.jpg
    31.1 KB · Views: 45
Nyumba ya 12m urefu na 10.6 m upana angle 30 nyuzi paa ni kama hapo chini hutumia bati na mbao kiasi gani
Mkuu makadirio ni hayo hayo niliotoa kwenye post yangu iliyopita.
Hilo paa lako limefanana kwa kila kitu na paa langu yaani utafikiri uliipiga picha paa ya nyumba yangu.
Utofauti wake ni upana tu wa paa langu ambao ni 9m na urefu ni 12m.
So jiandae tu kwa makadirio yaleyale na usikurupuke Kama hauna milioni 10 kwenye akaunti yako Kama utatumia bati la msauzi na mbao zenye dawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kwli kupaua gharama lakini sio kwa gharama hizo ulizo zitaja!...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…