Intelligence Justice
JF-Expert Member
- Oct 23, 2020
- 3,443
- 4,006
Wadau,Asalam Ailekum wandugu,
Nahitaji mtaalam wa kunifanyia makadirio ya ujenzi wa nyumba hususan kupaua kwa kutumia bati. Nyumba ipo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Natanguliza Asante.
--------------------
Hatua za ujenzi na gharama zake
1. Kujua kwa yakini ukubwa wa nyumba unayotaka kujenga na malengo yake;
2. Kusafisha kiwanja
3. Kupata Ramani ya nyumba kwa mahitaji na utashi wako
4. Kutafuta ushauri kutoka kwa mtalaamu wa udongo au fundi mbobezi wa ujenzi kuhusu aina ya msingi unaotakiwa kwa aina ya nyumba unayotaka kujenga;
5. Uthibitisho wa eneo unalotaka kujenga ni miliki yako ama kimila au kwa mjibu wa sheria za ardhi;
6. Tafuta uashi (mason) mwenye weledi wa kazi hiyo na mwaminifu;
7. Fanya mapatano ya gharama za kujenga msingi kuanzia kuchimba, kupanga mawe au tofali na kutandaza tofali
8. Pata idadi ya vifaa vinavyohitajika kukamilisha ujenzi wa msingi kama: mawe, tofali, mchanga, kokotoo, simenti, mbao za kukingia jamvi la zege, usafiri wa vifaa kwenda eneo la mradi(site) na maji,
9. Kokotoa gharama kamilifu ya vifaa ulivyofanyiwa tathimini na fundi kisha vinunue na kuweka stoo iliyo chini ya uangalizi wako mwenyewe
10. Gharama za kumlipa fundi ni asilimia 25% ya gharama za vifaa vyote. Kwa mfano kama gharama ya vifaa vyote vitavyowezesha kukamilisha ujenzi wa msingi ni shilingi 1,500,000/= malipo ya fundi yatakuwa ni shilingi 375,000/= gharama za fundi msaidizi na vibarua ni juu yake kasoro maji ambayo utalipa mwenyewe kwa anayetoa huduma hiyo. Hatua hizi zinafana na ujenzi wa boma hadi lenta (lintel), kupaua na umaliziaji (sakafu, rangi, dari. milango, madirisha, vifaa vya umeme na kuunganisha umeme, maji, miundo mbinu ya vyooni, bafuni nk);
11. Kumbuka ukianza ujenzi una hela ambazo hukuzifanyia mpango uliosahihi ukaishia kwenye kuweka kench ujue utapata hasara kubwa kuliko faida maana ubora wa mbao zilizotumika kupaua zikibaki wazi zikiangaziwa na jua na kunyeshewa mvua hazifai tena na kama hukuchukua tahadhari ukaja ukaanza kuezeka baada ya nusu mwaka nakuendelea hilo paa lina hatari ya kuporomoka.
12. Fanya ujenzi unaolingana na ukamilishaji wake kama huwezi kujenga dai mwisho mfululizo basi jenga kwa hatua hizi: Kusafisha, kuchimba na kujenga msingi-fungu la kwanza, kuinua boma na lenta-fungu la pili, kupaua na kuezeka bati-fungu la tatu, kuweka milango na madirisha-fungu la nne, kuweka waya za umeme na bomba za maji ndani ya nyumba-fungu la tano, kupiga lipu (plaster) na sakafu (floor)-fungu la sita, kuweka dari na kupaka rangi-fungu la saba. Ukizingatia haya utajenga bila presha ijapokuwa utachelewa kukamilisha. Usithubutu kuanza ujenzi wa nyumba kubwa ambayo hutakuwa na uwezo nayo kuikamilisha kama ulivyopanga itakufanya uchanganyikiwe hata kutamani kuiuza.
Huo ndio mchango wangu wadau kuhusiana na mada ya mdau.