Kupauka kwa bati. Je, Kuna rangi nikipaka itadumu kwa kitambo kirefu?

Wakuu bati zangu zimeanza kupauka ndani ya miaka 5 toka nipaue Aina yake ni zile za migongo mipana.

Je Kuna rangi nikipaka itadumu kwa kitambo kirefu? Naomba kuwasilisha

Shida TBS wapo wapo tu kulikoni mabati fake kuingia nchini?

Kwamba Kila baada ya miaka 5 kuezua kubandika mapya?

Kwani nayo yamekuwa perishable goods?

Mamlaka kama hizi za nini?
 
Wakuu bati zangu zimeanza kupauka ndani ya miaka 5 toka nipaue Aina yake ni zile za migongo mipana.

Je Kuna rangi nikipaka itadumu kwa kitambo kirefu? Naomba kuwasilisha
Uliza kwenye maduka ya ujenzi PVA KIBOKO, zipo takribani rangi 4: blue, kijani, nyekundu na damu ya mzee.
Usije ukapaka bati rangi ya ukuta.
 
Litakuwa ni funzo, walati ujao nitanunua ORIJILINO

Pale liliingia neno silo: - "kupajua." Daah! Unajua auto-correction tena.

Meant kupauka.

Bati original ndizo sote tunataka. Hakuna anayetaka fake. Sote tuna tatizo kama lako.

Sote tunaugulia maumivu makali na bidhaa fake yakiwamo mabati hayo. Kuwa bila kupenda tumeingizwa mkenge!

Kwamba TBS na hasa serikali tunaowalipa kodi kumbe majukumu yao yalikuwa nini?
 
So hizi ni maalum kwaajili ya bati tu, na je zinapakwa au inapigwa spray Kama gari?
PVA ni rangi maalum kwaajili ya paa tu,hata ukienda dukani utaona maandishi ya PVA kwenye ndoo.
Namna ya kuipaka inategemeana na bajeti Yako,Kuna watu wanatumia brush,mifagio ya kudekia yenye tambi nyingi halafu wenye uwezo wanachukua mashine ya kuspray.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…