Hoja yako ni nini haswa? Kuleta mipasho na vijembe kwenye mambo ya msingi ni dalili ya umasikini wa fikra. Tunaongelea uwekezaji wa 1.4T kubomoa na kujenga tena MNH katika kipindi ambacho bado hospitali zetu za Zonal na regional referal bado hazina basic specialized services wewe unaongea shombo. Are you serious?
Wewe ni mtu 'opportunist' hasa unayepigania kuonekana na huyo unayemwabudu ili akuone.
Inatia kinyaa sana kwa mtu kama wewe (kama kweli ni mhitimu wa fani hiyo) kujidhalilisha namna unavyojionyesha waziwazi.
"...kumhujumu (Rais?) Samia" kunaongeza thamani gani katika mada unayojigamba kuwa "ya msingi"?
Nimekuuliza wewe, unafikiri swala la "kumhujumu Samia" linakugusa zaidi wewe kuliko Mchengerwa?
Ukitaka nijadili hiyo habari ya tr 1.4; achana na habari ya kujikomba ili ujionyeshe mbele za hao unaotaka wakuone.
Kama nilivyosema mwanzo, sikusoma, na wala sijasoma umeweka nini kweny bandiko refu hilo; lakini kutokana na uzoefu wa maandiko yako, najuwa huko ndani kutakuwa na mengi ambayo siwezi kukubaliana nayo.
Wazo la kubomoa kilichopo mara nyingi siyo wazo zuri, lakini kuna nyakati uhitaji unalazimu kufanya hivyo.
Hii ni hospitali ya taifa zima, inayotegemewa katika kushughulikia 'specialities' zisozowezekana huko kwingine. Kwa hiyo uhitaji wake upo; kama uhitaji wa kuimarisha uwezo wa kushughulikia matatizo madogo huko mikoani na wilayani kulivyo.
Kwa hiyo ni swala la kupima uwiano kwa sasa upoje katika maeneo hayo mawili.
Na pia ni muhimu ujuwe kwamba hili swala la kuijenga Muhimbili upya siyo swala geni; limekuwepo miaka mingi. mawodi ya Sewa haji hayakidhi tena matakwa ya leo kwenye hospitali yenye hadhi ya aina hiyo