Kupeleka 1.2 Trilion kwa ajili ya kuibomoa na kuijenga Muhimbili ni kumuhujumu Rais Samia

Kupeleka 1.2 Trilion kwa ajili ya kuibomoa na kuijenga Muhimbili ni kumuhujumu Rais Samia

Kama hajielewi watafanya wao watakao.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Nafasi ya kumshauri Rais, ni nafasi adhimu inayobeba dhima kubwa kwa Taifa. Wananchi wanayo matarajio kuwa wenzao waliopata fursa ya kuwa washauri wa Rais wao, wanafanya hivyo kwa weledi, uadilifu na uzalendo wakitanguliza maslahi ya Taifa Mbele.

Siamini hata kidogo kwamba wizara ya afya ya nchi yetu haina wataalumu mahiri wenye ujuzi wa kutosha wa mahitaji ya huduma za afya nchini na nini viwe vipaumbele ili kufikia ustawi wa kweli katika kutoa matibabu bora kwa wanachi wetu, kabla ya kuanza anasa za kutafuta Joint Committee certification.

Wanaopigia debe mpango huu wa kupeleka 1.4T kuibomoa na kuijenga tena Muhimbili wanatuamisha kuwa jambo hili ni muhimu ili kuipa hospitali yetu ya Taifa hadhi ya kimataifa na kuiwezesha kupata Joint Committee certification ya kimataifa ambayo kwa Hapa Tanzania ni Agakhan Dar es salaam tu ndio wanayo. Hoja inajengwa kuwa kwa kufanya hivi nchi yetu itaimarisha medical tourism.

Wazo hili linaweza kuwa zuri ila sidhani hata kidogo kuwa hicho ndio kinachotakiwa kuwa kipaumbele chetu kwa sasa kama tunalengo la kuboresha huduma zetu za matibabu kwa wanachi. Nitaeleza sababu kama ifuatavyo:

Uwekezaji huu hautatusaidia kupeleka huduma karibu na wanachi. Katika tiba, magonjwa yote ya dhalula yanayoweza kuua "TIME" ndio factor kubwa kuliko zote kuokoa maisha. Kuwa na huduma bora sehemu moja tu, ambayo haiwezi kufikiwa ni sawa na huduma hiyo kutokuwepo kabisa. Tujiulize, mwanachi anayetokea Mara, Katavi, Kigoma, Rukwa, akipata Heart Attack, JKCI inatakuwa na maana gani kwake? **** tutalitazama hili kwa uhalisia wake sidhani kama tutamshauri Rais avunje JKCI iliyopo ili tujenge nyingine wakati tunahospitali zetu za mikoa tulizoziboresha na kuajiri wa taalamu hazina vitendea kazi.

Uwekezaji huu hautatatua tatizo la msongamano mkubwa wa wagonjwa Muhimbili na Taasisi zilizo chini yake. Hili halihitaji akili kulitambua kama tutajiuliza tukiwa na dhamira njema, kwanini kuna msongamano mkubwa pale Muhimbili? Jibu ni wazi, hospitali zetu za Amana, Mwananyamala na Temeke zimeshindwa kukidhi mahitaji ya wagonjwa. Ni vyema tukawa wakweli kwa nafsi zatu, Muhimbili inazidiwa kwasababu kunawagonjwa ambao hawakupaswa kwenda pale ila wapo pale kwasababu ya uduni wa hospitali zetu za wilaya na mikoa. Suluhu ya hili tatizo ni kuboresha huduma huko chini wanakotokea wagonjwa wanajazana Muhimbili.

Uwekezaji huu unahujumu moja kwa moja jitihada za Rais Samia na serikali yake ya awamu ya sita kuzijengea uwezo hospitali za mikoa. Kwa ambao hamjabahatika kutembea nchi hii, niwape tu taarifa kuwa uwekezaji mkubwa umefanyika kujenga hospitali za rufaa za mikoa. Ukienda Katavi, Mara, Singida, Manyara n.k miundombinu ya Hospitali za mikoa iliyopo itakushangaza, mahospitali makubwa, mazuri ya kisasa ila hatuna vifaa. Kama kweli nyinyi washauri wa Rais mnampenda kweli mama yetu simngemshauri hata anunue mitambo ya MRI na Cath Lab kwenye hizi hospitali zatu tupate Mama Samia Cardiac units nchi nzima? Je, hii sio njia bora yakumjengea Rais wetu legacy bora itakayogusa maisha ya wananchi wote? Kama tumeweza kuanzisha dialysis centers kwenye hizi hospitali zote, tumejenga emergency departments mpaka hospitali za wilaya hili linashindikana vipi?

Kama shida ni hospitali yenye majengo mazuri kupata international accreditation kwanini tusiitumie Mloganzila? Kuna hospitali nzuri nchi hii kwa majengo kuliko Mloganzila? Kuna ulazima gani wa kuibomoa Muhimbili ya sasa huku tukiwa tunauhitaji wa maboresho nchi nzima?

Ni vyema kama nchi tukawa na utaratibu wa kufanya coordination ya jitihada za Serikali. Katika awamu hii ya sita kupitia mpango wa Samia scholarship tumesomesha madaktari bingwa na madaktari bingwa bobezi. Kama rasilimali zote tutazirundika Muhimbili hawa wataalamu tunaoendelea kuwazalisha watafanya kazi wapi?

Maoni yangu ni wazi huu mpango sio kipaumbele cha Taifa kwa sasa. Mwenyezi Mungu amsaidie Rais wetu kuling'amua hili.

Kwani yeye hajui. Di ni pesa za Mama au wamekpiga bao bila yeye kutambua?
 
God forbid I should not add a word on this. Period
Doesn't make sense!
You must be overwhelmed by the sense of promoting yourself to be seen by those you erroneously think hold your personal interests to allow you think straight!
 
Kwani yeye hajui. Di ni pesa za Mama au wamekpiga bao bila yeye kutambua?
Yeye aende kwa Mchengerwa; ambaye ndiye waziri anayeweza kumtimizia hayo anayoyatamani yeye.

Sasa hapa hajui kwamba anamjumuisha hata huyo Mkwe katika hujuma anazozifikiri yeye?
 
Ana hujumiwa au hana uwezo ,kubalini tu elimu mbali mbali hastahili hata kua mjumbe wa nyumba kumi.
 
Ila huyo Rais ndio mwakilishi wa wananchi! Kuna ubaya gani akitajwa? Mbona tuna fedha za mama, goli la mama, scholarship za mama, kwanini na hii hujuma isiitwe ya mama?
Samia Suluhu Hassan hana uwakilishi wowote kwa wananchi ambao anawaogopa na kuwatawala kwa mabavu.
Akili yako inakuwa kama imejaa matope.

Huwa sina lembalemba na watu wa aina yako.
 
Samia Suluhu Hassan hana uwakilishi wowote kwa wananchi ambao anawaogopa na kuwatawala kwa mabavu.
Akili yako inakuwa kama imejaa matope.

Huwa sina lembalemba na watu wa aina yako.
The sooner you accept your reality, the sooner you will make peace with yourself. Sasa hivi unaogozwa na Samia, na ndiye anayeamua kodi ulizolipishwa ww zitumikaje. Kumtusi au kutomtambua Samia hakutamtoa kwenye urais. Ni vyema tukashirikiana naye kujenga nchi yetu kwa maslahi yetu sote.
 
How come yo know "my reality" and not be aware of your own terrible situation?
The sooner you accept your realit
How can it be, for you to know "my reality" without first being aware of your own sorry state of affairs?

Hayo ya kodi na matakataka mengine jambazi yeyote anao uwezo wa kuyafanya kama anavyofanya yeye ambaye ni mhalifu. Hilo halimpi kinga ya kutambulika hivyo na kuwajibishwa ipasavyo na waTanzania

Kwa hiyo upo hapa kupambania kupata sehemu ya hayo anayokusanya?
 
Back
Top Bottom