Stephen Ngalya Chelu
JF-Expert Member
- Oct 31, 2017
- 8,252
- 18,335
Mahusiano yana mengi sana.
Kuna nyakati unakuwa na mtu anayekuonesha mapenzi ya dhati, anakufanyia kila kitu lakini haum'feel kabisa. Unajaribu kumkasirisha ili labda akasirike akuache lakini wapi, kila kosa lako analisamehe na mara nyingine yeye ndo anakuwa anaomba msamaha kwa makosa yako.
Unajaribu kupunguza kumjali ili pengine umfanye na yeye aanze kukaa mbali na wewe lakini haitokei hivyo. Atalia atalalamika lakini bado atabaki na wewe. Unatamani umwambie muachane lakini unakuwa unamuonea huruma. Unabaki kuendelea kupata mapenzi motomoto ambayo hauyahitaji na huku siku zikisonga ukiomba lolote litokee muachane...