Kupendwa sana na mtu ambaye humpendi ni moja ya kero ambayo haisemwi

Adela popote ulipo unisamehe, nakumbuka ulivyonipenda kwa dhati, nakumbuka ulivyolia mbele yangu kwa uchungu.

Nilijaribu kuwa muwazi kwako kuwa nikikubali tuwe na uhusiano nitakuumiza bure...kumbe nilitia petrol kiberiti...ulilia sana lkn haikubadili kitu.

Nimejifunza kuepuka mapenzi yakumhurumia mtu kwani ni matesi ya kesho.
Kabisa bora mtu ajue,shida anakuwa anajipa matumaini kwamba huenda kuna siku utampenda,fyuu sitaki hata kukumbuka
 
Huwa najitahidi kuwa muwazi kama najua sina future naqe au sijakuelewa hata sijisumbui kukupa matumaini
 
Mahusiano yana mengi sana.

Kuna nyakati unakuwa na mtu anayekuonesha mapenzi ya dhati, anakufanyia kila kitu lakini haum'feel kabisa. Unajaribu kumkasirisha ili labda akasirike akuache lakini wapi, kila kosa lako analisamehe na mara nyingine yeye ndo anakuwa anaomba msamaha kwa makosa yako.

Unajaribu kupunguza kumjali ili pengine umfanye na yeye aanze kukaa mbali na wewe lakini haitokei hivyo. Atalia atalalamika lakini bado atabaki na wewe. Unatamani umwambie muachane lakini unakuwa unamuonea huruma. Unabaki kuendelea kupata mapenzi motomoto ambayo hauyahitaji na huku siku zikisonga ukiomba lolote litokee muachane...
Hili tatizo mtu ambaye hajalipitia hawezi kulielewa.
 
Unakua katika usalama zaidi wa akili, afya na uchumi wako unapokua katika mahusiano na mtu ambaye yeye ndie anakupenda kuliko ambae wewe ndie unampenda.

Achana na upumbavu wa soulmate na maigizo unayoyaona kwenye tamthilia za wafalipino, otherwise you wil learn the hard way.
 
Hakuna mahusiano ya wote mkawa mnapendana sawa hakuna kitu kama icho mkuu. Hata huyo ulienae unaedhani unampenda kumbe nae anampenda mwingine.
Kuna limoja lazima liwe kolo.
Hapo dem wake ni kolo ila nae akienda kwa mwingine yeye ndo anakua kolo huku dem mpya akitafuta nae chimbo jipya ili nae awe kolo
 
Mahusiano yana mengi sana.

Kuna nyakati unakuwa na mtu anayekuonesha mapenzi ya dhati, anakufanyia kila kitu lakini haum'feel kabisa. Unajaribu kumkasirisha ili labda akasirike akuache lakini wapi, kila kosa lako analisamehe na mara nyingine yeye ndo anakuwa anaomba msamaha kwa makosa yako.

Unajaribu kupunguza kumjali ili pengine umfanye na yeye aanze kukaa mbali na wewe lakini haitokei hivyo. Atalia atalalamika lakini bado atabaki na wewe. Unatamani umwambie muachane lakini unakuwa unamuonea huruma. Unabaki kuendelea kupata mapenzi motomoto ambayo hauyahitaji na huku siku zikisonga ukiomba lolote litokee muachane...
Halafu mkiachana na ww unampenda mwingine, ila yeye hana habari na wewe
 
Nyie mbuzi kila siku mnalia lia humu kuwa siku hizi hamna upendo wa dhati!! Kumbe mnapendwa ina mnapenda changamoto!!🤣🤣🤣
Basi na mnyooshwe tu.
Umekula nini kwani wewe?

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Back
Top Bottom