Kupigwa billioni 75 ni ujinga au upumbavu? Tutaendelea kukubali kufanywa kichwa cha mwendawazimu hadi lini?

Kupigwa billioni 75 ni ujinga au upumbavu? Tutaendelea kukubali kufanywa kichwa cha mwendawazimu hadi lini?

Tafakari upya msimamo wako wa kupigia chapuo CCM

Serikali ya CCM imetufikisha hapo na hatuna la kuifanya. Tukiwa na serikali inayowabikika kwa wananchi inakuwa na guts za kutofanya makosa ya kuigharimu nchi.

Hatukuanza leo kulipishwa hayo mabilion. So long as tunaendelea na CCM haitakuwa mwisho wa kulipishwa hayo mahela.

Leo tunamlaumu JPM kwa kudhani ndo tumeshaliadress tatizo. JPM ni zao la CCM na hata huyu wa sasa anayetuingiza mkenge maradufu naye ni zao la chama chetu kilichopoteza dira.

Inauma, lakini tuanze kuuishi ukweli
Nilikuwa najiuliza mbona wateule wake wanamsifia sn maza? nimepata majibu
 
Hii kesi imefufuliwa na wanaume wapige pesa then maza wa mwambie anaupiga mwingi na majina mazuri mazuri huku wanapiga pesa za umma, umewahi kuona wapi kesi kubwa kama hii inaendeshwa kwa miezi 2? kuna kesi ya ubunge ambayo haina maslahi kwao leo ina miaka 2 haijulikani hata mwisho wake.

Hatuna sera bora na hatujui tunataka wawekezaji au sisi wenye tujikwamue tuwe wawekezaji wa kwanza kabla ya mgeni
 
Nani alaumiwe mkuu kama sio ccm. Mmoja apokee wawekezaji mwingine aje wafukuza. Unategemea nini?
CCM siyo mtu, haiwezekani kuilaumu. Huko mahakamani haiendi CCM.
Tulaumu watu wanaofanya haya maamuzi na watajwe hadharani ili wananchi tuwaachie au tuwahukumu. Siyo kila siku kutaja kitu kisichoonekana eti ccm.
 
CCM siyo mtu, haiwezekani kuilaumu. Huko mahakamani haiendi CCM.
Tulaumu watu wanaofanya haya maamuzi na watajwe hadharani ili wananchi tuwaachie au tuwahukumu. Siyo kila siku kutaja kitu kisichoonekana eti ccm.

Nani anachagua mwanasheria mkuu wa serikali, ni chama gani kinaunda serikali na washirika wake. Uozo wa hii nchi ma ccm havikaii mbali
 
Ujuha na ulimbukeni wa CCM ndio umetufikisha hapa na bado tutaendelea kulipa gharama. Uwizi na upigaji dili ndio wanachoweza. sheria zipo kwanini hawafuati sheria na utaratibu. Jamaa wamepata hela ya bure bila kuwekeza chochote na bado tusubiri la DPW linakuja.
 
Kwanza tukalipa kwa siri tozo ya Simbion na kununua kwa siri mitambo ya Richmond/Dowans/Simbion sasa ni mali yetu!.

Kila dege zetu zinaposhikiliwa kwa kukazia hukumu fulani, huwa tunalipa kisiri siri, ndege zinaruhusiwa maisha yaendelee
 
Billion 75 dadeki 🤔
HIz ni shule kadhaa kaliiii za serikali kiwango cha english medium kwa kila mkoa Tanzania Nzima.Sio chininya shule 20 zilizokamilika kwa kila mkoa watoto wetu wakasoma kwa angalau kulipa ada ya 150,000/= kwa mwaka ili kuzifanya ziendelee kuwa bora.

Hizi ni hospitali kail za kiwango cha kati zenye huduma zote muhimu kwa kila kijiji Tanzania nzima.Hospital moja moja kwa kila Kata nchi nzima yenye mahitaji yote ya muhimu.

Lakin cha kusikitisha pesa hii inaenda mfukoni mwa watu watatu tuuu out of more the 60Millions people in the whole fu*cking repulic
 
Tujisahihishe kama ambavyo amewahi kuandika baba wa Taifa ili tusirudie makosa ambayo yatakuwa yanatugharimu kama Taifa.
Huwezi kujisahihisha Kwa bunge butu linalopokea na kupitisha Kila kitu toka serikalini bila kuhoji wala kurekebisha. Huwezi kujisahihisha kama Una Spika ambaye ni Msemaji wa serikali.
 
Tuwaulize wanazi Lucas mwashambwa ChoiceVariable haya mahela yanatolewa kwenye vote ipi ya bajeti.

Maana wao wanaijua seeikali kuliko hata waliomo ndani ya serikali
Kwani Mimi ndio nahusika na mikataba? Ipo ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Kabudi hao ndio Wana majibu.

Nalaani uhuni huu maana niliandika Hadi mada kupinga.

Kwamba Mafungi yapi yanatumika.kulipia inaweza kuwa fungu la mengineyo maana lipio.
 
Back
Top Bottom