PM again at his best with the same lengthy, old, classic, familiar, bizarre Tanzanian narrative. Anyway tunashukuru kwa kutiririka tena kuhusu “maajabu” tuliyoyazoea ya nchi hii.
Jibu kama sisi ni wajinga au wapumba wanalo mashabiki wa kejeli ya “tutashitakiwa MIGA”; “mzalendo wa kusimamia rasilimali za nchi”; “Chiba”, etc.
Rais mmoja wa CCM anaingia mikataba ya kifisadi ya kuhujumu nchi. Anashangiliwa kwa shangwe zote kama mkombozi wa nchi kiuchumi. Rais wa CCM anayefuatia anavunja hiyo mikataba na kubadilisha sheria zinazohusika. Anashangiliwa kweli kweli kama mkombozi wa nchi kwa kulinda rasilimali. Halafu nchi ikibanwa kwenye mahakama za kimataifa analipa madai kisirisiri na kulalamikia “wasaliti”. Rais wa CCM anayefuatia analipa kiroho safi na kwa uwazi madai yote yanayojitokeza kutokana na madhambi ya waliomtangulia. Hakuna maelezo yanayotolewa kwa wananchi wala hakuna anayewajibishwa.
What a charade!
Ujinga na upumba ni wa kudumu hadi siku uchawa kwa magenge ya viongozi wa CCM utakapokoma na kura za wananchi kuheshimiwa kwenye chaguzi zetu. Kama nguvu ya wananchi kuweka viongozi madarakani na kuwawajibisha haipo nchi itaendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu.