Kupigwa billioni 75 ni ujinga au upumbavu? Tutaendelea kukubali kufanywa kichwa cha mwendawazimu hadi lini?

Kupigwa billioni 75 ni ujinga au upumbavu? Tutaendelea kukubali kufanywa kichwa cha mwendawazimu hadi lini?

Kwahiyo hao CCM yote haya hawayajui sio...
Hayo ya chama cha Mapinduzi umesema wewe. Kwanini roho yako inapenda sana Negativity? Ukisikia Tanzania imepatwa na jambo baya unafurahi kwenye moyo wako? Haya ushauri wako ni nini?
 
MFUMO WA UONGOZI WA NCHI YETU NI MBOVU, MFUMO WA KUCHAGUA VIONGOZI NI MBOVU, UTARATIBU WA KUTEUA VIONGOZI NI MBOVU NA HATUNA MIHIMILI MITATU ILIYO HURU NA INAYOJITEGEMEA. BUNGE NA MAHAKAMA SIYO MIHIMILI INDEPENDENT, MHIMILI INDEPENDENT NI SERIKALI NA CHAMA TAWALA AMBAO KIONGOZI NI MMOJA.
 
Mnajaza bungeni makada wa chama, wanasheria wa Tz wote wameja wale wenye strong connection na vigogo wa CCM, kweli utegemee ufanisi katika sekita yoyote.

Hizo $30m bado nyingi zitalipwa kosa kubwa ni kuruhusu mtu kama JPM kua Raisi wa nchi hi bado wataendelea kulipia hayo makosa.
Ni ujinga bado, kuendelea kulaumu juu ya JPM ambaye mpaka anaondoka miaka yake 6, makampuni haya haya yanayolipwa sasa, ndiyo hayo yaliosistishiwa leseni zao mwanzoni kabisa mwa utawala wa JPM na hayakufungua kesi wala nini

Tuwe tunajiuliza na tutumie akili zetu kubalansi mambo!

Kwa nini iwe leo, kwa nini isiwe kipindi cha Mwendazake na ndiye aliyesitisha kazi za makampuni hayo??

Tanzania inahitaji Shirika la kijasusi strong mfano wa enzi za JPM, tuachane na vijana wa UVCCM wanaharibu uchumi wa nchi yetu
 
CCM siyo mtu, haiwezekani kuilaumu. Huko mahakamani haiendi CCM.
Tulaumu watu wanaofanya haya maamuzi na watajwe hadharani ili wananchi tuwaachie au tuwahukumu. Siyo kila siku kutaja kitu kisichoonekana eti ccm.
Nchi hii ni “totalitarian state”. Rais ndio kila kitu. Ndiye mwenyekiti wa chama tawala (CCM) chama kilichomuweka madarakani. Ndiye mwenye maamuzi ya mwisho ndani ya serikali na ndani ya CCM. Mamlaka na madaraka yake ni kamili (absolute power).

Hakuna ufisadi mkubwa wa “tens of millions of USD” unaoweza kufanyika na kufanikishwa bila yeye kuhusika au kuruhusu. Hivyo serikali inapokuwa kimya kwa hujuma ya kiwango hicho nalo ni jibu la “kikubwa”.

CCM inazidi kuwa msiba wa taifa!
 
Mkiambiwa serikali ya Ccm imeshashindwa kuongoza hii nchi na haitakaa iweze tena hata ikikaa madakani milele unakaza fuvu wakati hali iko wazi kwenye kila sekta ni shida tu.Ukiona mapambio ni mengi kuliko kukosoana na kuchukua hatua jua iko shida kubwa kwenye huo uongozi.Watu wanapiga kila mahali na tunaona ni sawa tu wakati changamoto ziko kila kona ambazo zingeweza kutatuliwa hizi pesa tunazozifuja kila leo.
 
Back
Top Bottom