Mkuu naomba niweke mchango kidogo hapo kwamba bunge lilikuwa sahihi kutunga sheria inayo ruhusu migogoro ya uwekezaji kusikilizwa ndani ya Nchi. Kwani kulizingatia matumizi ya principle za private international law.
Mikataba ya kimataifa ya uwekezaji inayo husisha parties ambazo zinaongozwa na sheria za mataifa mawili au zaidi. Endapo Ikitokea mgogoro aidha kwenye mikataba na ikatokea kuna mabishano ya mahakama ya nchi gani itumike au sheria za Nchi gani itumike ndiyo vipengele vya private international laws vinaingia.
Kwenye private international laws kuna principle inaitwa Lex fori ambayo inaruhusu machaguo ya sheria na chombo cha usuluhishi kutumika pale migogoro inayohusisha pande za Nchi tofauti. Lex fori inaruhusu matumizi ya sheria za ndani za Nchi kutatua migogoro hiyo. Hapa ndipo sehemu ya msingi ya sheria ya kulinda maliasili na rasilimali za Nchi.
Pili kuna Lex loci contractus principle hii inaruhusu kuwa sehemu ambayo mkataba umesainiwa ndiyo sehemu ambayo mgogoro ukitokea mahakama ya sehemu husika itakuwa na mamlaka. Ndiyo maana Rais Magufuli alikuwa anasisitiza sana mikataba ya uwekezaji isainiwe hapa Tanzania. Kwasababu mkataba ukisainiwa hapa Tanzania mahakama kuu inakuwa na jurisdiction chini ya principle ya Lex Fori.
Kingine tunaangalia domicile au nationality ya watu au subject matter dispute ipo situated wapi. Mfano madini yapo Tanzania hivyo katika kipengele cha domicile nchi ya Tanzania itakuwa na haki ya kutumia sheria zake za rasilimali kutatua migogoro.
Tatizo linaanzia kwa Ma senior advisor na Advocates ambao hawana msaada wa kuishauri serikali ndiyo maana vitu kama hivi vinatokea.
Lengo la awamu ya Magufuli kupitisha sheria hiyo ya rasilimali ni kwasababu wanasheria wetu wana uwezo mdogo sana katika international litigation especially kwenye arbitration. Pia matatizo yanaanzia kwenye mikataba hasa kwenye kipengele cha Law applicable na jurisdiction.
wanasheria wetu huwa wana discuss mikataba na wawekezaji kwa uoga sana kwasababu aidha wanamaslahi 10% au wanapewa maelekezo ya kuuza rasilimali.
It was a wise decision kwa hayati Magufuli kupitisha sheria ile ila tatizo ni Kwamba hatuna watu wanaopenda Nchi yao.
Tatizo lingine ni ratification ya makubaliano ya kimataifa kama UNICITRAL,au Taasisi kama
- International Chamber of Commerce (“ICC”)
- London Court of International Arbitration (“LCIA”)
- International Centre for Dispute Resolution (“ICDR”)
- Swiss Chambers' Arbitration Institution (SCAI)
- Vienna International Arbitral Centre ("VIAC")
Mara nyingi wanasheria wetu hawajui procedure za huku kwetu hizi taasisi za Arbitration na kupelekea kushindwa kesi kizembe. Kama raisi Samia alivyo sema wanasheria wetu wakiwa kwenye hizo mahakama za kimataifa wanaogopa wazungu hasa macho yao.
Wito wangu ni kwamba serikali iweke kipaombele sana kwenye maliasili na rasilimali za Nchi kuliko kuwapa kipaumbele wawekezaji.
Na pia zitungwe rules of procedure chini ya sheria ya maliasili na rasilimali "Natural Wealth and Resources (Permanent Sovereignty) Act, 2017 (No. 5 of 2017). " Ambazo zitaongoza utatuzi wa migogoro na mahakama yenye mamlaka pamoja na sheria zitakazo tumika kati ya serikali na wawekezaji. Hii itasaidia sana kulinda rasilimali zetu na kuondoa rushwa, kupunguza gharama za kesi kuendeshwa nje ya Nchi.