Kupigwa Marufuku Makanisa ya Kilokole, Gwajima amjibu mkuu wa mkoa wa Arusha, ni mtoto wa Dawa

Kupigwa Marufuku Makanisa ya Kilokole, Gwajima amjibu mkuu wa mkoa wa Arusha, ni mtoto wa Dawa

Baada ya mkuu wa mkoa wa arusha kusema kuwa makanisa ya walokole yadhibitiwe kwa kuwa wanapiga kelele (Makanisa ya kilokoke kudhibitiwa)

Gwajima ameamua kumjibu mkuu huyo

Amesema kuwa Tanzania ni nchi huru kila mtu ana haki ya kuabudu, muda wowote na wakati wowote

Amesema kuwa waumini wa madhehebu ya kilokole wako milioni, kwa hivyo huwezi kuwazuia.

Apinga agizo hilo la mkuu wa mkoa wa Arusha
Huyu mkuu wa mkoa ameyataka mwenyewe. Acha Gwajima amlipue.
 
Ni haki ya msingi kwa kila raia kuishi bila bugudha. Uhuru wa kuabudu usiwe kigezo cha kwenda kinyume na Sheria na Kanuni zinazomlinda mwananchi kutokana na Uchafuzi wa Mazingira ukijumuisha matumizi hatarishi ya sauti.
 
Kila siku kuanzia saa 10 hadi 11 alfajiri kuna kelele za.adhana lakini kwa kujua ni hitaji la imani za watu hakuna anayejali. Kulikoni huyu mtoto wa dawa?
 
Baada ya mkuu wa mkoa wa arusha kusema kuwa makanisa ya walokole yadhibitiwe kwa kuwa wanapiga kelele (Makanisa ya kilokoke kudhibitiwa)

Gwajima ameamua kumjibu mkuu huyo

Amesema kuwa Tanzania ni nchi huru kila mtu ana haki ya kuabudu, muda wowote na wakati wowote

Amesema kuwa waumini wa madhehebu ya kilokole wako milioni, kwa hivyo huwezi kuwazuia.

Apinga agizo hilo la mkuu wa mkoa wa Arusha
Awazuie na hawa waliouza kengele kila siku wanaita watu wa kuita
 
kwingineko duniani: Gwajima acha ubishi tanguliza busara
Pastor Gets Jail Time for Noisy Church
Gospel church fined because singing and preaching was too loud for neighbours
California Church Threatened With $500 Per Day Fine After Gospel Choir Accused of Excessive Noise — but They’re Fighting Back
Church Noise – Welcome to the Church of Noise
Is this Louisiana church's service too loud? Yes, authorities say
Oakland church gets warning after neighbors complain of choir noise

inabidi kuwa na kiasi,
waislamu wanawaita wenzao waje kuswali sioni shida. Mabar yapigwe marufuku au wawekewe limit ya sauti,
Kuhusu walokole inabidi wawe na kiasi, Kama unamuomba na kumsifu Mungu wako aliye sirini kuna haja gani ya kupaza sauti kwa wasiohusika. Tena saa nane usiku masaa kadhaa non stop.

Mkuu wa mkoa amekuwa biased kwa kusahau wapaza sauti wengine, hii haiwafanyi walokole wanaopiga kelele sana usiku kuwa na uhalali wa kuwazuia wananchi wengine wasilale. Hekima inahitajika. Sheria iwekwe yenye limit ya sauti. na ukivunja uwe ni mlokole,muislamu,disko,mdundiko mimi kama jirani nikushtaki unilipe fidia ya kunisumbua usiku nishindwe kupumzika kesho nifanye kazi kwa ufanisi offisini.

Pia bibilia inawataka watu wa dini kuwaheshimu viongozi wa serikali hata kama wanamapungufu. kumuita muwakilishi wa rais kwa kejeli mtoto wa dawa au kumfananisha na jini Mungu hakubaliani na udhaifu huo. Hapo mtumishi kateleza atutake radhi.
Amtake radhi au atutake radhi
 
Mimi ni mkristo safi ila kuna baadhi ya makanisa yanaboa kwa kweli inabidi na Mkuu wa mkoa wa Mbeya naye atoe tamko.Kuna staff mwenzangu anaishi karibu na kanisa moja dogo yaani mbele ukumbi wa kanisa nyuma nyumba za kupanga.Wakianza kupiga kelele inabidi uondoke hadi wamalize.Mbona misikiti ipo hadi uswahilini lakini hii kero hakuna?
dawa ni ndogo sana,mwambie arudishe family kijijini kwa mda hata miezi 6,kisha anunua vifaa vya mziki vile heavy duty,aanzishe kakanisa hapo kwake,ka masela kujumuika na kumwabudu jah raasfari na kupiga miziki ya akina alpha blondy usiku kucha.
Watajisoti wao wenyewe
 
Tukiongea Uwazi Ni Kwmb, Kelele Zipo Kwa Dini Zote Na Sehemu Za Starehe.
Kwa Mtu Ambaye Anaishi Karibu Na Kanisa/Msikiti Anaonja Joto Ya Jiwe Ya Hizi Kelele.

Sheria Sio Kwmb hazipo, Zipo Muda Mrefu Tu Lakn Huwa Hazifuatwi Hata Kidogo Kutokana Na Kwmb Tz Bado Hatujawa Na Watu Ambao Wanaweza Kulipeleka Hili Mahakamani.

WANGEWEKA TARATIBU KAMA IFUATAVYO.
1. Kila Imani Ipeleke Kisheria Siku1 Au 2 Ambayo Inaabudu.

MFANO.
Waislamu Ijumaa.
Wakristo Jmosi&Jpili.

2. Siku Hizo Pekee Ndio Waruhusiwe Kuweka Vipaza Sauti Pamoja Na Siku Za Sikukuu Tu.

Kabla Ya Kufanya Hivyo, Wawashirikishe Wadau Ambao Ni Waumini Wa Dini Husika (Viongozi) Ili Nao Kutoa Maoni Yao Nini Kifanyike.

Kwa Kifupi Mimi Nilishawahi Kuishi Karibu Na Kanisa Kwa Zile Kelele Nilihama, Lakn Pia Nikaishi Karibu Na Msikiti Kukawa Na Kero Hizo Hizo Za Kelele.

Uwekwe Tu Utaratibu Hapo Maana Kama Mtu Kwa Moyo Wa Dhati Anahitaji Kusali/Kuswali Si Lazima Aitwe Kwa Kipaza Sauti Au Maombia Kwa Sauti Kuuubwa Kiasi Cha Kuwakera Wengine.

Wazo Langu Wadau.
Mbona unaandika kwa kuanza kila neno na herufi kubwa? Ndo swaga na kitambulisho chako hapa JF kama alivyokuwa Pdidy ama? Huchoki na kupoteza muda kubofya CAPS key mara kwa mara?

Samahani mkuu. I am just curious hasa ukizingatia kuwa we siyo mdot.com (kama hiyo picha ni yako na uko verified user). Otherwise all is well!
 
Kulinda uhuru wa kuabudu ni muhimu lakini ni vyema tulinde tusiingilie uhuru wa wengine. Uhuru wako unaishia pale wangu unapoanzia. Ni vyema tukajiwekea utaratibu wa misikiti, makanisa n.k vinapokuwa maeneo ya makazi tusikwazane. Leo mtu jirani yako anaokoka na kuanza kusali kwa Walokole then ndani ya miaka miwili anaamua kufungua kanisa lake ndani ya eneo lake anafunga spika kubwa ni mwendo wa mapambio na kukemea usiku kucha huku upande wa pili ni familia na watoto wadogo hawawezi kulala zaidi ya kushtuka muda wote. Ni jambo jema lakini lazima lifanywe kwa hekima.
 
yule ni kiongozi wetu watanzania sio arusha tu(muwakilishi wa rais), kumdhalilisha kwa maneno yasiyo na staha katukosea wote. Hatutake radhi.
mtumishi kateleza
Ukinikana mbele za watu namii ntakukana mbele za watu!!
Ivi hawa viongoz hawana washauri had wanakurupuka" hata kama alikua sahihi jinsi ya utoaji taarifa!!
Kwanza jina lake nani ili tujue tatizo lake
 
Mbona unaandika kwa kuanza kila neno na herufi kubwa? Ndo swaga na kitambulisho chako hapa JF kama alivyokuwa Pdidy ama? Huchoki na kupoteza muda kubofya CAPS key mara kwa mara?

Samahani mkuu. I am just curious hasa ukizingatia kuwa we siyo mdot.com (kama hiyo picha ni yako na uko verified user). Otherwise all is well!
Napenda Hii Style Mkuu Na Nimeizoea So Sioni Tabu.
Kila Kitu Changu Hapo Bro Sioni Haja Ya Kuficha ID Yangu Na Picha Coz Am Not A Criminal Na Nipo Jf Kujadii Na Kujifunza.
Pia Kutumia Jina Na Picha Halisi Huleta Nidhamu, Hekima Na Busara, Huwezi Kumtusi Mtu Ama Kuandika Habari Za Kichochezi Badala Yake Utajikita Kuielimisha Jamii Na Kujiimisha Mwenyewe.
Tupo Pamoja Mkuu.
 
Waelekezeni ndugu, rafiki na jamaa kuwa:
Uungwana zaidi ni kutumia ujuzi katika kusaidia wengine wenye matatizo, msongo na migongano ya ndoa kwa kuwa wamekaa kipindi kirefu bila kupata watoto - watumie dawa lishe kwa miezi miwili (2) mtafuteni mtalaam kwa simu +255788 628696
Sipo huko, tunazungumzia hoja ya Gwajima
 
kwingineko duniani: Gwajima acha ubishi tanguliza busara
Pastor Gets Jail Time for Noisy Church
Gospel church fined because singing and preaching was too loud for neighbours
California Church Threatened With $500 Per Day Fine After Gospel Choir Accused of Excessive Noise — but They’re Fighting Back
Church Noise – Welcome to the Church of Noise
Is this Louisiana church's service too loud? Yes, authorities say
Oakland church gets warning after neighbors complain of choir noise

inabidi kuwa na kiasi,
waislamu wanawaita wenzao waje kuswali sioni shida. Mabar yapigwe marufuku au wawekewe limit ya sauti,
Kuhusu walokole inabidi wawe na kiasi, Kama unamuomba na kumsifu Mungu wako aliye sirini kuna haja gani ya kupaza sauti kwa wasiohusika. Tena saa nane usiku masaa kadhaa non stop.

Mkuu wa mkoa amekuwa biased kwa kusahau wapaza sauti wengine, hii haiwafanyi walokole wanaopiga kelele sana usiku kuwa na uhalali wa kuwazuia wananchi wengine wasilale. Hekima inahitajika. Sheria iwekwe yenye limit ya sauti. na ukivunja uwe ni mlokole,muislamu,disko,mdundiko mimi kama jirani nikushtaki unilipe fidia ya kunisumbua usiku nishindwe kupumzika kesho nifanye kazi kwa ufanisi offisini.

Pia bibilia inawataka watu wa dini kuwaheshimu viongozi wa serikali hata kama wanamapungufu. kumuita muwakilishi wa rais kwa kejeli mtoto wa dawa au kumfananisha na jini Mungu hakubaliani na udhaifu huo. Hapo mtumishi kateleza atutake radhi.
Mtoto wa dawa ni mtoto wa kutengenezwa kwa mganga, hiyo hasikii wala haelewi, neno la MUNGU kwake ni moto, hataki hata kulisikia.
 
yule ni kiongozi wetu watanzania sio arusha tu(muwakilishi wa rais), kumdhalilisha kwa maneno yasiyo na staha katukosea wote. Hatutake radhi.
mtumishi kateleza
Na yule aliyedanganya Shinyanga akatimuliwa alitutaka radhi? Kiongozi akikosea arekebishwe, sema Lugha ya Gwajima hujaielewa. Viongoz wengine bila stail zao hawakusikii NG'O. kAMA KAZOEA KUROPOKA, ATAREKEBISHWA KWA STAILY ILEILE. Kiongozi ukitoa maamuzi yawe sawa kwa jamii yote usilalie upande mmoja. Kelele usiku wanaopiga wengi, weka muongozo kwa wote, HAPO NANI KATELEZA ATUTAKE RADHI
 
Mtoto wa dawa ni mtoto wa kutengenezwa kwa mganga, hiyo hasikii wala haelewi, neno la MUNGU kwake ni moto, hataki hata kulisikia.
lugha za dharau na kujikina kidini. hayo mambo mmemconsult na kuthibitisha hilo au mnatumia uhuru wa dini kupachikia viongozi sifa mlizokuwa nazo kabla ya wokovu
 
Kwani vilabu na mabaa na disko hazipigi kelele mbona ajapiga marufuku
 
Back
Top Bottom