Wewe acha ufala!
Yesu, mitume na manabii wake hawakuwa WANAFIKI kama wewe. Kwenye upumbavu walikemea viongozi au wenyewe kwa wenyewe tena kwa maneno makali.
Nitakupa MIFANO michache;
1. Wewe na YESU nani Mtakatifu?! Yesu aliuona UPUMBAVU wa Mfalme Herode, mtu mkubwa kwenye nchi alipozuia INJILI, na akamfananisha na MBWEHA.
"Akawaambia (Yesu), Nendeni, mkamwambie yule MBWEHA (Herode), Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilika." - Luka 13:32
2. Wewe na Masihi wa Mungu, YEHU nani Mtakatifu?! Hakuona soni kumwambia ukweli Mfalme Yoramu juu ya UKAHABA wa kiroho wa mama yake aitwaye YEZEBELI.
"Ikawa, Yoramu alipomwona Yehu, akasema, Je! Ni amani, Yehu? Akajibu, Amani gani, maadamu UZINZI wa MAMA yako Yezebeli na uchawi wake ni mwingi?" - 2 Wafalme 9:22
Acha ufala, narudia tena. Umenikwaza, na mimi nimeamua kukupa za uso.
Mtu yeyote anayejifanya kuzuia kazi za Mungu, ni kama Mbweha tu.