Kupigwa Marufuku Makanisa ya Kilokole, Gwajima amjibu mkuu wa mkoa wa Arusha, ni mtoto wa Dawa

kuna hekima gani kwa kiongozi wa dini kumuita kiongozi wa serikali(ambaye ni kiongozi wa watu wa dini zote na wasio na dini)JINI MTU?Ni hekma za kabila gani hizo kumuita kiongozi jini au mtoto wa dawa?Inawezekana kwamba amefanya utafiti na amejiridhisha kwamba ni mtoto wa dawa lakini sio hekima kumtangazia kila mtu,na kama anamtangaza kuwa ni mtoto wa dawa bila utafiti wowote hapo amekosea zaidi kwa principle ya "NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK"
 
Acha kuchanganya mambo kiongozi. Tunaemjadili hapa ni mtu anayejitambulisha kwa jamii kama kiongozi wa dini, mtu anayehamasisha maadili na tabia njema. Kwa nafasi yake hayuko sawa kabisa kuongea sentesi zenye viwango vya chini kabisa tena nyepesi za udhalilishaji na zisizozungukwa na busara. Maana tunaamini bibilia humbadilisha mtu na kuwa muungwana sio kwa utaratibu wa huyu. Ninasema na kwa nia njema kabisa
 
Kwa uzoefu wake Gwajima anafahamu kuwa ni shetani na watoto wake ndio wanapingana katika pilika za kufanya kazi za mungu. Sasa akatokea mtu akajiingiza kwenye 18 bila hata kuangalia na wengine atamuelewaje? Gwajima atamfananisha na nani? Hata hawa jamaa akimuita kiongozi flani Kafiri sababu tu mkristo, hiyo sawa
 
Hauna adabu,acha watu waabdu km wanavyo taka
 
Na je kama kweli huyo mkuu katumika kama mototo wa dawa, kauli ya Gwajima ni sawa? angetumia njia ipi ili ujumbe ufike (waswahili wasema mwake mwake). Kuna msitari kwenye biblia unasema kuwa "mpumbavu utamjibu kutokana na upumbavu wake" (siukumbuki) vinginevyo hatakuelewa. Gwajima anapenda kutumia staili hiyo kuwajibu kwa jinsi anavyowaona hao. Nakumbuka namna alivyomuongelea speaker aliepita, DAA.
 
Iwapo kila mtu ataongea na public kwa mujibu wa uzoefu wake bila hata kupima matokeo ya kile anachoongea itakuwa vurugu,na matokeo ya kutenda kwa mujibu wa uzoefu mara nyingi ni kujikuta unajigonga kwenye sheria na kujeruhiwa.
Yako mambo ameyasema hapo naungana nae,mfano kabla ya kufika hatua hiyo zipo baa kwenye makazi ya watu zina usumbufu may be kuliko hayo makanisa,lakini kwa hili la kumuita binadamu mwenzio jini nadhani amepotoka.
 
Kamuita mtoto wa dawa sio jini. ukimwambia ajitete atasema watenda zambi wote anawaita ni watoto wa shetani. Mkuu katenda zambi ya upendeleo, kaacha kule anakoshiriki kagusa kwingine.
 
Hauna adabu,acha watu waabdu km wanavyo taka
acha hisia na kupanic bila sababu, tunamwabudu Mungu kwa roho na Akili.
huko mtaani kuna wapagani,wasioamini Mungu,Watu wa kila aina. Hakuna mtu aliyemkataza mwenzake kusali.

Kama ushauri wa RC hukuuelewa fuata basi hata huu wa yesu.
mathayo 6:1-8
1wafaLME 19:11-13
1KORINTHO 14:33
 
Wakuu hapa suala la msingi ni Sauti hatarishi kutoka katika vyanzo tofauti tofauti. Je, tunatambua kuwa vyanzo vya sauti kwenye mazingira ya nje havitakiwi kutoa Sauti zaidi ya 60 hadi 65dB ?
 
Hahahaaaaa Mungu ana kazi ya ziada kama wamwabuduo ndo wako hivi..Mungu hufurahi kuabudiwa na wanyenyekevu...
 
Nimekupata mkuu. Tusonge mbele!
 
Wewe utakua mwislam una hide identity
 
Kila siku kuanzia saa 10 hadi 11 alfajiri kuna kelele za.adhana lakini kwa kujua ni hitaji la imani za watu hakuna anayejali. Kulikoni huyu mtoto wa dawa?
Huyo hakika ni mtoto wa dawa
 
Askofu Gwajima amesema aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo aliwakatalia walokole kufanya matamasha ya mkesha kwa madai kuwa wanapiga kelele.

Gwajima amesema Gambo ni " mtoto wa dawa" au Jini mtu nasi baada ya kusikia kufuru zake tulimlaani na kumshtaki mbele za Mungu wa mbinguni.

Maendeleo hayana vyama!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…