Kaka
C.T.U the bottom line ya hii thread yako ni kuwa WANAWAKE TUJITAMBUE. Mwanamke napaswa kuitambua thamani yake kwanza kama binadamu pili kama mwanamke. Tukilitambua hili ni wazi kuwa itasaidia sana kuepuka 'mitungo ya kizembe na ile ya kujitakia' - mfano kuleweshwa kwa kuwa tu unapenda offer, kujifanya too much uzungu - kama ulivyoiweka kumingle na kila mtu hata usiyemjua vema. Pili ingawa ni vigumu kujua undani wa mwanaume anayekutokea kama kweli anakupenda kweli au anakutaka kukukomoa lakini yatupasa kuwa na subra na
kumwomba MUNGU maana ukiwa ni yule wa yes kwa kila anayekutamkia neon basi hutapona. Tuwasaidie na wenetu wa kike kuwaelewesha wajitambue. Hiyo ya Martial arts, nimeanza kuifanyia kazi maana naona mbinu yangu ya kuwa natembea na tindikali inawezanipeleka segerea bure mana ishakuwa kosa la jinai