Mkuu utakuwa umejiozesha ndoa ya mkeka ukiruhusu jiko kuwaka ndani ya room yako ya kibachelor.
Mi niliwahi kuoa pre mature kwa visa vya kujipikilisha nikiwa msimbe kama unavotaka kufanya wewe!
Kosa nililolifanya ni kumuomba aje anipikie!
Tulipigiana simu kuoneshana ufunguo ulipo nikiwa kazini, kurudia ebhanaee!
chumba nilikipotea kilivyosafishwa na msosi uliopikwa!
Kesho yake nilikakataa asiondoke na ikawa ndiyo chanzo Cha ndoa yangu ya bila matarajio.
Mwanaume yeyote ukifanyiwa mambo niliyoyataja, lazima 'urogeke', huwa hamna ujanja tena!
Nenda ukale kwa nama ntilie huko, usiruhusu jiko kuwaka ili kujiepusha na ndoa zisizotarajiwa.
Ukianza tu kukarangiza kwa mikono yako huko kwenye mapango, lazima utavamiwa tu kusaidiwa kazi hiyo hata na watu usiowatarajia, ambao kwao hiyo ni fursa!