Kupima wanafunzi wa kidato cha pili kwa kutumia division ni kuharibu mfumo wa elimu

FACT
 
na wanavyotangaza kazi kama poliisi kuwa ni ufaulu wa 4.28 basi mwanafunzi wa kidato cha pili akipata hiyo 4.28 anazembea akiamini form four atapata kam ahiyo ili ajiunge na jeshi
Ndiyo maana polisi kama unavyowaona hali zao, CCM inataka watu wajinga wajinga
 
Sikuizi sio rahisi kumpata kijana aliyeishia kidato cha pili.
kwani hamjui kwamba kidato cha nne ndiyo elimu ya msingi. Siyo la saba tena.

Mambo sasa hivi yanafanyika kisiasa kuficha uozo wa mfumo wetu wa ELIMU. Hakuna mzazi anataka kusikia mwanae amefeli. Na wanasiasa wanajua hili.

Kwa mfumo huu maana yake huwezi kusikia kelele za elimu duni, au kiwango cha elimu kimeshuka.
 
Mtindo huu unasababisha sifuri na division Four nyingi kwenye matokeo ya kidato cha nne.
 
Hatari sn
 
Ni mfumo tuu wa kutoa matokeo ,D mbili na F zote hazina tofauti yeyote na wastani wa D, tatizo kubwa shule hazina walimu wa kutosha
 
Kabla ya kufikia huku au sambamba na hili... Hivi kweli, wale wanafunzi wa "NguoKuchanika" unatungia na kuwafanyisha mtihani sawa na Feza au St. Francis ??
 
hata hao wachache waliopo hawaipendi kazi yao mkuu, ndio maana muda wa kazi unamkuta kwenye bustani yake ya vitunguu
Walimu wametengwa. Hakuna anayewajali.
Shule nyingi za serikali hazina utofauti na mahabusu!
Watendaji wanatenda bora liende!!
 
Siasa siasa tu kila mahali. Tunaua elimu kama utani. F 4 ya juzi eti wastani wa Chemistry ni 92% nacheka kwa sauti.
 

Hakuna wizara inayochezewaga kama elimu Tanzania. Yaani kila waziri akija, kila rais akija kila badiliko lolote la waziri hata kama ni wawili au watatu katika awamu moja ya miaka mitano au kumi anaweza au atakuja na mabadiliko yake, sera zake sijui hakunaga nwongozo wa elimu angalau wa miaka 10 au hata 20 huko.

Kila siku tume haziishi, kuna uhuni mwingi sana huko hadi kubadilisha masomo, mfumo wa ufaulu mitihani hiyo ,vitabu nk nk.halafu hao wanaobadilisha na kuuchezea mfumo wa elimu na wizara sasa wala hkuna hata mmoja ambaye mwanae anasoma katika shule hizo za serikali. Nasema tena hakuna awe rais, waziri sijui katibu wa hiyo wizara HAKUNA, wao wako saint saint academia huko international na kwenye curicullum za camridge huko ism ist na feza feza.

Sasa hiyo inaonyesha jinsi gani mfumo wetu ulivyotoboka na kudharaulika wao wapo kutengeneza sera za kuhesabu per diem na madawati. Kwa kuongezea pia ndio moja ya wizara inayoongoza kwa kujengwa na kubomolewa kama kuunganishwa na kutenganishwa na wizara ama idara nyingine.
So expect the unexpected.
 
Na huko shule za msingi watoe mitihani ya kujibu kavukavy ili kuchangamsha akili.
Hesabu mnaweka maswali ya kuchagua!
Vi woonder

Kuna mitihani Kama GRE na GMAT Mkuu maswali yote ya kuchagua na unaangukia pua Kama kawaida mtu mzima,uje na master yako degree yako
 
Hili ndo limeshindikana kabisa au tusubiri Zitto Kabwe atakapokuwa Waziri wa elimu? Yaani Tangu mwanafunzi anaanza la 1 mpaka form 6 Hakuna mahali anapimwa personal development mpaka afike chuo?

Kenya washaanza kitambo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…