Hakuna wizara inayochezewaga kama elimu Tanzania. Yaani kila waziri akija, kila rais akija kila badiliko lolote la waziri hata kama ni wawili au watatu katika awamu moja ya miaka mitano au kumi anaweza au atakuja na mabadiliko yake, sera zake sijui hakunaga nwongozo wa elimu angalau wa miaka 10 au hata 20 huko.
Kila siku tume haziishi, kuna uhuni mwingi sana huko hadi kubadilisha masomo, mfumo wa ufaulu mitihani hiyo ,vitabu nk nk.halafu hao wanaobadilisha na kuuchezea mfumo wa elimu na wizara sasa wala hkuna hata mmoja ambaye mwanae anasoma katika shule hizo za serikali. Nasema tena hakuna awe rais, waziri sijui katibu wa hiyo wizara HAKUNA, wao wako saint saint academia huko international na kwenye curicullum za camridge huko ism ist na feza feza.
Sasa hiyo inaonyesha jinsi gani mfumo wetu ulivyotoboka na kudharaulika wao wapo kutengeneza sera za kuhesabu per diem na madawati. Kwa kuongezea pia ndio moja ya wizara inayoongoza kwa kujengwa na kubomolewa kama kuunganishwa na kutenganishwa na wizara ama idara nyingine.
So expect the unexpected.