Kupima wanafunzi wa kidato cha pili kwa kutumia division ni kuharibu mfumo wa elimu

Kupima wanafunzi wa kidato cha pili kwa kutumia division ni kuharibu mfumo wa elimu

Ni mfumo tuu wa kutoa matokeo ,D mbili na F zote hazina tofauti yeyote na wastani wa D, tatizo kubwa shule hazina walimu wa kutosha
Shule zingine Zina walimu wa kutosha ila hawana mbinu za kiufundishaji, walimu wanafundisha kimazoea huku miyoni wajaa husda
 
Wangetumia mfumo wa wastani watoto wengi wangebaki kidato cha pili, serikali wajanja
Serikali wapo sawa kwa hilo maana maisha ya nje ya shule yanatumia vyeti hivyo acha wengi wapate vyeti vya kugombania ajira maana kazi nyingi zaidi ya sayansi haziitaji mtu alichosomea msingi na secondary.
 
Kutunga mtihani mmoja sawa na hizo shule sio tatizo mkuu, maana wote wanatumia sylubas moja tatizo ni katika hizo shule za serikali walimu wameshajikatia tamaa kabisa
Kwa hicho kigezo cha walimu kujikatia tamaa ni kwamba hao vijana hawafundishwi sawa na wenzao. Hivyo kuwaweka kwenye kapu moja na kuwapa mtihani mmoja si njia sahihi kabisa.
Ni ukatili wa hali ya juu!!
 
Shule zingine Zina walimu wa kutosha ila hawana mbinu za kiufundishaji, walimu wanafundisha kimazoea huku miyoni wajaa husda
Huwa hata huko mavyuoni wanapopikwa hawa walimu, wanapikwa kiaina tuu na matokeo yake ndio haya nae anawapika wanafunzi wake kwa style ya kuwapasha juu juu tuu
 
Back
Top Bottom