Kupinga Serikali Tatu; Natofautiana Na Profesa Issa Shivji...

Nguruvi3, Nakubaliana nawe kwa baadhi ya hoja ulizozitowa kuhusu Muungano huu na nakubaliana nawe kuwa serikali tatu haziepukiki.
Kwanza nafikiri utakubaliana nami kuwa kushindwa kwa Jumbe na G55 hakuletwa na mtu mwengine yeyote bali Nyerere katika harakati zake za kunusuru kizawa chake (Muungano). Pia utakubaliana nami kuwa sababu za harakati hizi mbili zilikuwa tofauti kwani wakati Jumbe sababu yake ni kule kubaini kuwa alidanganywa na Nyerere kwa uchu wake (jumbe ) wa madaraka. G55 sababu zao zilikuwa ni kulipa dharau walionyeshwa na Salmin (Komandoo) na kauli yake ya "kutingisha kibiriti". ukiangalia sababu zote mbili hazikuwa na nguvu za wananchi, lakini hili la sasa ni kuwa wananchi wenyewe wameshabaini kuwa kunahitajika mabadiliko.
Kuhusu Issa Shivji na wasiwasi wake si chengine bali ni yaleyale ya maslaha binafsi, Shivji, CCM bara, CCM Zanzibar na wazanzibari wachache wenye kumiliki mali Bara wote wanaangalia maslaha yao binafsi. Shivji anaamini kuwa ameshajijenga Bara na anaogopa kuvunjika kwa Muungano ( anajuwa vilivyo kuwa mpaka sasa nia hasa ya muungano kwa upande mmoja( Bara) haipo. CCM bara wanajuwa kuwa kujitenga kwa Zanzibar kuna maana ya kupoteza madaraka na pia wagombeaji wa chaguzi wanajuwa kuwa watapoteza ngome muhimu katika harakati za kura za maoni (hasa wakijitangaza kuwa wanauinga mkono serikali 3, jambo litakalowakasirisha CCM zanzibar). CCM zanzibar wao masilahi yao ni kuwa fedha zote za uhai wao kichama zinatoka Bara hivyo kutofautisha serikali ni kuenda kwenye utengano (wanajuwa kuwa hakuna nia thabiti ya Muungano hivyo serikali mbili ni turufu. Na ukija kwa wenye mali kule Bara sababu zao ziko wazi na hofu yao Watanganyika wataamuaje ikiwa sasahivi kila wakati wako midomoni?
Sasa hili la kutumia nafasi na miundo mbinu ambayo itawafanya wananchi wazidi kuchanganyikiwa nsdio silaha yao makundi haya na hapo utapat sababu kwanini Shivji na wenziwe wanafanya wanachofanya.
 
Mkuu hapa nakupa salute

 
Ndugu Majid swala la serikali tatu bado ni kizungumkuti kingine ambacho waZanzibar hawataki kusikia. Unajua wazenji wanataka kuona bendera yao ikipepea pale UN. Wanaamin maisha waliyonayo sasa hiv nimagum ukilinganisha kabla ya muungano, Lakin tujiulize tena kwa Tafakuri kubwa saana 1) Nani alimuua Karume na kwa nini 2) unadhani muungano ukivunjika Zanzibar itabaki kuwa Zanzibar ama itatokea Unguja na Pemba! 3) Ni kwa nn Kambarage aliutaka muungano kwa udi na uvumba na alilaani atakae uvunja???? 4) ni kwa nn baada ya kumfukuza sultani na zanzibar kupata uhuru yule mwanamapinduzi Okello alitimuliwa!. Tutafakari nadhani kuna jambo muhimu sana na sio hiz blah blah sijui garama sijui ujinga gani.. Mr Majid hebu fuatilia hata baadh ya hayo machache nadhan twaweza pata mwanga.

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Shivji anatumika kwa matakwa ya magamba.

Prof. Shivji nimemshangaa sana, sidhani kama yale ni maoni yake binafsi bila chembechembe za magamba. Hivi kama tukiungana na nchi ya tatu let say Kenya, serikali zitakuwa 3 kwa maana Zanzibar na Kenya watakuwa na za kwao, na ya Jamhuri?, Je tukiungana afrika mashariki yote serikali zitakuwa 5? yaani kila nchi itakuwa na serikali yake na ya Jamhuri isipokuwa Tanganyika! Huu utakuwa wendawazimu! Mi nadhani Prof. SHIVJI ni vizuri kustaafu kila kitu maan utaanza kuharibu sifa nzuri uliojijengea katika Jamii! SISI WANANCHI TUNATAKA SERIKALI TATU Jaji WARIOBA amekusanya na kuwasilisha mawazo yetu.
 

Serekali tatu labda ni maoni ya wananchi wa tanganyika,huku zanzbr maoni yetu ni mamlaka kamili ya z'br ikifuatiwa na muungano wa mkataba,kinyume na hapo kaunganeni na kenya.
 
Kwa yeyote aliesoma rasimu kwa nia safi akaielewa utakubali kabisa kuwa Serikali tatu hazikwepeki. Sababu iko wazi kabisa kuwa hatuna Muungano bali tuna ushirikisho la mambo 12 ya nchi 2. mambo mengine yooooote kila nchi kivyake. Sasa huwezi ukasema serikali ya moja isimamie mambo hayo 12 na ya nchi mojawapo, halafu nyingine ijisimamie yenyewe kwenye mambo yake. Hii inchi inayojisimamia lazima itaona kuna fursa ambazo huyu anaesimamiwa na Muungano anazipata chini ya kapeti kidhuluma dhuluma, na inakuwa sio rahisi kuisimamia hiyo serikali maana mipaka ya kiutendaji haieleweki. Kwa hiyo moja futa Zanzibar ibakie serikali moja [Muungano uvunjike papo hapo] kitu ambacho bara hawawezi kuthubutu kufanya au Serikali tatu, ili serikali ya SHIRIKISHO aka Muungano iweze kuwa wazi na kudhibitiwa na hizo za nchi shirika. CCM haitaki serikali tatu lakini Rais anataka ndio maana ametoka Baraka tuendelee na mjadala sasa kazi kwao, kimewageukia wakawashawishi wananchi wapige kura ya hapana.
 
Tukimaliza serikali tatu tunaanza mchakato wa Sera ya Majimbo, watakoma mwaka huu
 
SI kweli kwamba hapelekeshwi, ni kibaraka mzuri wa mtazamo wa mwalimu Nyerere wakati hata chama alichokiasisi yeye (Mwalimu) kimebadilika.
 
Prof kivyake yeye huwa anaongea tu anayaacha hakuna mbadala wake tumemzoea, siku hizi hata makala zake na matamko yake na michango yake naona ipite tu
 
Serekali tatu labda ni maoni ya wananchi wa tanganyika,huku zanzbr maoni yetu ni mamlaka kamili ya z'br ikifuatiwa na muungano wa mkataba,kinyume na hapo kaunganeni na kenya.

Tupige kura, ninyi mko wangapi na sisi Bara tuko wangapi. hamuwezi kuunga mkono Serikali tatu kwa sababu na ninyi itabidi mchangie kwenye serikali kuu ya shirikisho, siyo kama sasa hivi mnakula vya ubwete toka Serikali ya Jamhuri.

Vinginevyo, LIWALO NA LIWE kwani tunanufaika na nini toka Zanzibar? Kila mtua ashike kipande chake atambaye kwani wasio ungana kama Kenya, Uganda, Rwanda, Msumbiji, Malawi nk. tunawazidi nini zaidi ya ufisadi na uroho wa madaraka?
 
Sijui kama Majid alimuelewa Prof. Shivji. Prof hakupinga serekali tatu, alichokiongelea mwanzo mpaka mwisho ni haja ya kuipa mamlaka zaidi katiba ya serekali ya muungano basi
 
Usisahau kuwa wapo wahamiaji kule Zenji wakitoka Tanganyika, sasa status yao iwe vipi?
Ngekewa,

..wa-Znz ndiyo wenye mamlaka ya kuamua watafanya nini na wa-Tgk waliohamia huko.

..pia napendekeza wa-Znz wapewe ukaazi hata kama Zanzibar itaamua kuwarudisha makwao wa-Tanganyika walioko huko.

..mimi kwa upande wangu nadhani tukiweza kuli-handle vizuri, kwa ustaarabu na upendo, suala la wa-Znz walioko huku Tanganyika, then we will be fine moving forward.

..wengi wanazungumzia masuala ya Yugoslavia, Serbia, Bosnia, lakini tunaweza kujiepusha na yaliyotokea huko kama tutayashughulikia matatizo yetu mapema kabla hayajageuka kuwa uhasama wa waziwazi.

cc: Kubwajinga, Kibunango, Nguruvi3, Jasusi, GHIBUU, Foum Jnr, maggid
 
Last edited by a moderator:

Mbona sifikiri kuwa wananchi wana matatizo kwa mtu anaefuata taratibu na mwenendo wa wenzake waliowakuta.
Wazanzibari hawajawahi kuwa na matatizo na wenzao wa Bara kiasi kwamba uzalendo wa kizanzibari unajengeka miongoni mwa wahamiaji kutoka nje ya Zanzibar. Tatizo la kubaguwana mara zote unaletwa na viongozi wanapotumia uzawa kwa maslaha yao.

Kwa mfano wazanzibari walikuwa ndio wahudumiaji wa shughuli za kibiashara kwenye miji mingi Bara kabla ya wenyeji kuamuwa kufanya shughuli hizo baada ya kuona mafanikio ya wageni.Hali kadhalika kuja kwa wamachinga Zanzibar kumerahisisha shughuli nyingi ndogo ndogo zanzibar. Tatizo linakuja pale tabaka la viongozi linapowatumia wananchi kwa maslahi yao.
 
zanzibar wana eneo la ukubwa karibu sqm 2000 sawa na mji wa kahama tanzania bara wana eneo la ukubwa wa sqm karibu 800000 juzi juzi watu wameshituka kusikia mafao wanayolipwa viongozi wastaafu bado kuna gharama za uendeshaji wa serikali ambayo ni kiasi kidogo cha bajetikinatengwa kwa shuguri za maendeleo huku sehemu kubwa ikienda kwenye kulipa mishahara na gharama nyingine za kuendesha serikali ni heri tuvunje muungano kuliko kung'ang'ania muungano ambao unatutia umasikini nafikiri hili kenyata aliliona mapema ndio maana akakataa muungano
 
Serikali 3 jawabu tutapata serika mbili huru, Zanzibar huru na Tanganyika huru.
 
Kweli watanganyika mnapenda vya bure,mmezoea mawaziri wa muungano kuwafanya ndio hao hao watanganyika,mpango wa sasa ni kuwa kila moja ahudumie mawaziri wake na kila kitu chake,zanzbr ina kila kitu chake kwanini nyie muone taabu kuwa na vyenu?tukutane EAC na UN,zanzbr kwanza.
 

Mupige kura nyie kama nani?watanzania au watanganyika?rujisha tanganyika yako kwanza (kama una ubavu huo)ndipo uropokwe.
 

Kumiliki kitu kuna gharama na iwapo mnataka kuimilik Zanzibar basi msijali gharama. Nakubaliana nawe kuwa hiyo haja ya muungano hasa haipo hasa ilivyokuwa Tanganyika wameshagunduwa mafuta yao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…