Nguruvi3, Nakubaliana nawe kwa baadhi ya hoja ulizozitowa kuhusu Muungano huu na nakubaliana nawe kuwa serikali tatu haziepukiki.Maggid, nadhani utasikia rai yangu ya wewe kushiriki mijadala na si 'kutupa' kitu na kukimbia.
Kuna utata sana wa serikali 3. Aliyekuwa rais wa znz Aboud Jumbe alijiuzulu kwa sakata hilo.
Wznz waksema ameonewa.
G55 ilikuja na pendekezo hilo kama ilivyokuwa kwa tume ya Nyalali, Kisanga na Warioba(tume ya kwanza).CUF kina sera ya serikali 3. Profesa Shivji amekaririwa mara nyingi akitaka serikali 3.
Inashangaza wale waliokubali serikali 3 ndio hao hao wanaoonyesha mashaka nayo akiwemo Prof Shivji.
Prof Shivji ni mzanzibar na ametoa elimu ya znz katika muungano. Kama raia au msomi anayo haki ya kujiunga na taasisi kama maridhiano au Uamsho bila tatizo au kujificha.
Kisichopendeza ni kujificha nyuma ya uprofesa ili kuendeleza ajenda za akina Uamsho .
Hapa natofautiana naye sana na nabaki kumuheshimu sana.
Ukisoma mapendekezo yake, anasema mambo ya nje na uraia yasiwe ya muungano kama wanavyodai wale wa mkataba wa muungano.
Prof anashangaa kwanini Polisi lisiwe jambo la muungano wakati huo huo akitaka znz huru kama walivyo akina Maalim na Jussa.
Ukiondoa Uraia na uhamiaji hakuna serikali ya shirikisho. Rais wa shririkisho hawezi kuwepo kama hakuna raia na hapo Prof Shivji anaunga mkono hoja ya kuvunja muungano kiufundi.
Profesa anasema mapendekezo yaliyopo yatampa rais wa Tanganyika nguvu kubwa kwasababu ana eneo kubwa.Prof haelezi nguvu ya kiuchumi itakayotokana na mchango wa Tanganyika katika serikali kuu.
Kwamba kuwe na usawa hilo haliwezekani isipokuwa kama znz itakuwa na mchango sawa na Tanganyika.
''with great power comes responsibility''
Prof anasema wznz wengi wanataka mamalaka kamili. Juzi tu kulikuwa na kikao cha kamati ya kushughulikia kero za muungano chini ya Gharibu Bilal na Makamu wa pili wa rais Idd Seif alisema kuna.Ingawa sikubaliani na kamati hizi lakini kuna kitu kinachoonekana hapo.
Kinachoonekana ni kuwa wanaotaka mamlaka kamili ni wapemba ambao nadhani Prof Shivji ana sympathize nao kwa kusema ni wengi.
Lau isingekuwa hivyo akina Gharib na Idd Seif wangeungana na akina Jussa na Maalim kutaka mamlaka kamili.
Hofu ya profesa ni kuvunjika kwa muungano. Hapa amejificha tu katika usomi lakini ukweli ni kuwa hasimamii muungano.Znz imevunja katiba ya muungano mara zaidi ya 10, profesa hakuwahi kuonya kuwa kuna hatari ya kuvunja muungano.
Leo ujio wa Tanganyika anaona hatari hiyo! Ukimsoma vizuri profesa, anaunga hoja ya muungano wa mkataba lakini nafsi inamsuta
Ndugu yangu Kobelo, federation haiwezekani kwasababu znz inataka iwe znz kwa maana kuwa haitaki kutoa kuwa sehemu ya federation. Haikubali kupoteza utambulisho kama ilivyofanya Tanganyika.
Na mwisho wale wanaosema hawataki muungano wa serikali 3 inabidi waende mbali na kusema wanataka ipi?Wakisema mbili, je watawatendea haki Watanganyika.Wakisema moja je znz wapo tayari kutoa sehemu ya uhuru na mamlaka yao?
cc.JokaKuu, Jasusi, Mwanakjiji, Kichuguu, Mchambuzi
Kwanza nafikiri utakubaliana nami kuwa kushindwa kwa Jumbe na G55 hakuletwa na mtu mwengine yeyote bali Nyerere katika harakati zake za kunusuru kizawa chake (Muungano). Pia utakubaliana nami kuwa sababu za harakati hizi mbili zilikuwa tofauti kwani wakati Jumbe sababu yake ni kule kubaini kuwa alidanganywa na Nyerere kwa uchu wake (jumbe ) wa madaraka. G55 sababu zao zilikuwa ni kulipa dharau walionyeshwa na Salmin (Komandoo) na kauli yake ya "kutingisha kibiriti". ukiangalia sababu zote mbili hazikuwa na nguvu za wananchi, lakini hili la sasa ni kuwa wananchi wenyewe wameshabaini kuwa kunahitajika mabadiliko.
Kuhusu Issa Shivji na wasiwasi wake si chengine bali ni yaleyale ya maslaha binafsi, Shivji, CCM bara, CCM Zanzibar na wazanzibari wachache wenye kumiliki mali Bara wote wanaangalia maslaha yao binafsi. Shivji anaamini kuwa ameshajijenga Bara na anaogopa kuvunjika kwa Muungano ( anajuwa vilivyo kuwa mpaka sasa nia hasa ya muungano kwa upande mmoja( Bara) haipo. CCM bara wanajuwa kuwa kujitenga kwa Zanzibar kuna maana ya kupoteza madaraka na pia wagombeaji wa chaguzi wanajuwa kuwa watapoteza ngome muhimu katika harakati za kura za maoni (hasa wakijitangaza kuwa wanauinga mkono serikali 3, jambo litakalowakasirisha CCM zanzibar). CCM zanzibar wao masilahi yao ni kuwa fedha zote za uhai wao kichama zinatoka Bara hivyo kutofautisha serikali ni kuenda kwenye utengano (wanajuwa kuwa hakuna nia thabiti ya Muungano hivyo serikali mbili ni turufu. Na ukija kwa wenye mali kule Bara sababu zao ziko wazi na hofu yao Watanganyika wataamuaje ikiwa sasahivi kila wakati wako midomoni?
Sasa hili la kutumia nafasi na miundo mbinu ambayo itawafanya wananchi wazidi kuchanganyikiwa nsdio silaha yao makundi haya na hapo utapat sababu kwanini Shivji na wenziwe wanafanya wanachofanya.