Hoja gani unazojenga wewe uliejaa na ushindani, chuki na jazba against wazanzibari. Hoja ya Maggid hainihusu nimeleza zamani mtazamo wangu juu ya muungano tatizo la wanavijiji kama wewe umejaaliwa na kitu kimoja sawa na mtikila, uchoyo, chuki na simanzi kwa wenye asili zisizo za kiafrika. na hutafikia hapa, utaendela kuchukia hata ndugu zako wa damu soon baada ya kukuacha mkono kwa kujuwa true colour zako na kujificha katika utanganyika wakati mtazamo wako umebebwa zaidi na matashi yako ya ubaguzi. nakubali hapa si mzalendo wala zanzinet, kule kuna ustaarabu wake na dasturi za kuheshimu mawazo ya mwengine sio kujifanya mjuaji na ego zisizo na muelekeo na ndio maana ukapata jukwaa humu la kuendekeza hujuma zako za kibaguzi. umeona wapi mtu mzima mwenye akili zake na kujitia ujuzi mkubwa wa elimu aseme duniani nzima Tanganyika ndio iliobeba wazanzibari wengi, inaonekana kabisa mapungu ya upeo wako wa kufiokiri na pia upofu katika discussion ya intellectual level. msimamo wangu haujabadilika, ni mkataba kama nilivyotoa maoni yangu, mwenye kauli ya mwisho ni wananchi wote sio elite ya wachache wanaondeleza ubabe na matusi against jamii ya wengine. narudia tena hakuna wa kumfukuza yeyote popote katika dunia hii ya leo, endelea na jukwaa la pumba na kuhamasisha watu kuchukiana, ujuwe tu kawaida ya watu wa aina yako hawataishia hapo, na ndio tunayoyaona sasa hadi mabomu kuripuana kwa immaturity ya siasa. hakuna katika dunia ya leo atakaethubutu kutomtendea haki mwengine wa pande yoyote kwa kukosekana kwa muungano, kuendeleza mabishano na mtu mwenye mawazo kama yako ni aibu kwa taaluma yangu. gurupu lako na yule mtikila hakuna tafauti, na sumu yenu ya ubaguzi haitakwisha hapo mutakulana wenyewe kwa wenyewe, na ishara zinaonekana sasa. Upande wa hoja za Magid, still, hata kwa mfumo wa serikali tatu anaousema yeye na shivji nitaupinga kwa maoni inapofika siku, na wewe katoe maoni yako ya kuvunja muungano, hebu kuwa na heshima ya kukubali kiutafautiana. Ujuwaji ndio unaokufanya ukadharau mawazo ya wengine, na ulimwengu wa demokrasia haukufai. Labda nikwambie tena huna wala hutaweza kumfukuza, kumdhuru au kumfanya chochote mzanzibario katika muungano huu, ujao au hata ukivunjika, dunia ya sasa si ya watu wa aina yako ya savimbi wanaochochea ugomvi baina ya watu kwa chuki binafsi, na sawa kwa wazanzibariu, hakuna atakaeweza kumfukuza, kumdhuru au kumfanya chopchote mtanganyika katika muungano huu, ujao au hata ukivunjika, achane exaggerations zenu kwa mambo yasiokuwapo. Ulimwengu utakusuteni kwa ubinfu wa mawazo mabaya against wengine kwa vile mitazamo yenu haiendani.
Hoja yako ni mkataba. Kama znz wanataka mkataba, mkataba huo ni wa kitu gani? Pili, nani kasema znz wanaTaka mkataba? Je umeheshimu mawazo ya wale wasiotaka mkataba? Majibu tafadhali
Kuhusu chuki, kwani Watanganyika walipochomwa moto kule znz kwasababu ya Utanganyika hilo lilikuwa jambo jema?
Kama unaamini kuwa hata muungano ukivunjika watu hawatafukuzana, iweje basi usimini kuwa watu watafukuzana endapo ndani ya muungano si kuwa wamefukuzana bali wamechomwa moto, si kwa ugaidi, ufisadi au wizi bali kwa Utanganyika! Nani aliwachoma moto na je wale waliochomwa moto unadhani wanajisikiaje.
Niambie kuna chuki gani mtu akikwambia urudi znz ukapumue? Sindicho mnachokitaka kila siku!!
Kile unachokiita chuki, kwa upande mwingine ni ukweli. Hivi si kweli kuwa wanafunzi 1000 wa Tanganyika walikosa udhamini kwasababu udhamini huo ulienda kwa wanafunzi 1000 wa znz? kueleza hilo ni chuki? je lilitakiwa liwe siri?
Je, si kweli kuna sheria inamnyima haki Mtanganyika kufanya kazi znz bila kuwa na sheria inayonyima mznz haki ya kufanya kazi za mtanganyika ambaye amezuiwa znz ? Hapa kuna chuki gani? si ukweli au ilitakiwa iwe siri ili mtu aonekane mwema!
Zamani hukuwasikia Watanganyika wakisema jambo hadi wznz wakalalamika kuwa ni kwa vile wanafaidika na muungano.
Leo wanasema let them go, wengine ondokeni, hapo unadhani wanaongozwa na nini? Hulioni hilo, na anayekwambia kuwa ndivyo ilivyo ndiye mwenye chuki au aliyepanda mbegu ya chuki kutoka visiwani?
Kuhusu la mkataba, hilo ni baadhi ya maoni ya wznz. Wengine wanasema serikali 3, wengine 2.
Ukweli unabaki kuwa hakuna Mtanganyika anayejua mkataba ni kitu gani kwahiyo katika meza ya majadiliano hilo halipo unless ujibu hoja nilizokuuliza ili kutushahwishi tuelewe mkataba kama ulivyoelewa wewe.
Endapo hutaweza kujibu basi tafadhali kaa kimya kwasababu hatuwezi kuheshimu mawazo ya mtu asieyaheshimu mwenyewe kwa kuelewa anaongelea nini.
Kwa hoja ya Maggid, kuanzia tume inaundwa hoja yangu ni kura ya maoni kwa wznz. Wakitaka kupumua basi tukutane EAC au SADC au AU. Lau haliwezkani basi serikali 3 kwa taabu sana na kila mmoja abebe gharama zake
Nisichokbaliana nacho ni serikali 2 au hilo duduwasha linaloitwa mkataba. Tunataka kujenga taifa hatuhitaji mikataba.
Nadhani utajikita katika kujibu hoja zaidi kuliko jazba. Hata munkari ukipanda haisaidii kwa sababu siku na muda ukifika mbivu na mbichi zitajulikana. Faraja unazozieleza ni kuituliza nafsi kwa woga lakini ukweli unabaki pale pale.
Woga wako ndio walio nao wznz wengine na ndicho chanzo cha mkataba, mahusiano n.k. Mnajua mwisho wa muungano ni mwanzo wa kitu gani. Chuki mliyoipanda dhidi ya Watanganyika itawarudi tu. Unanisingizia mimi sijachoma moto mtu kwasababu ya eneo analotoka, sina chuki, chuki ni wazanzibar wanaowakimbiza Watanganyika na viberiti.
Napenda wznz wakapumue