Youngblood
JF-Expert Member
- Aug 1, 2014
- 19,433
- 56,810
Habari zenu,
Kwakweli kama wote mnavyojua kijana Diamond Platnumz ni moja ya vijana wapambanaji sana katika nchi hii,ni wale vijana waliotoka from the bottom huko chini kabisa na wakafanikiwa kupata mafanikio makubwa kutokana na juhudi binafsi.
Kinachonishangaza sasa ni trend kubwa ya Watanzania hasa vijana kumchukia huyu ndugu yetu hata bila sababu za maana kabisa badala ya kujifunza kutoka kwake.
Mbaya zaidi Watanzania tumejikita kumfanya ashuke pale alipo au aonekane hana chochote wala lolote, ukipita mitandaoni huko huoni hata wanaompongeza kwa mafanikio yake, wengi utaona wanapambana kumshusha inasikitisha sana, nakumbuka hata mimi mwenyewe kuna kipindi mkumbo huo ulinipitia kutokana na habari za mitandaoni, lakini nikagundua ni majungu tu.
Vijana wa Kitanzania tuache Majungu na fitina tuchape kazi, umbea hauna posho, hatuwezi kufanikiwa kwa kipiga majungu bila kupambana.
Asanteni.