Youngblood naomba niseme haya machache
Mti wenye matunda ndio hupopolewa mawe. Kuchukiwa ni ada ya mwanadamu. Hapa duniani kila kitu kina uwili! Kukiwa na wanaokupenda basi wanaokuchukia hawakosekani, kukiwa na wanaokusifia basi wanaokukosoa hawakosekani pia.
Watu duniani kote hufurahia mabaya ya mtu kuliko mafanikio yake na ndio maana habari mbaya za watu huvuma kwa kishindo kuliko habari zake nzuri.
Diamond kijana asiye na elimu lakini mwenye mafanikio makubwa naye ana mapungufu yake..hakuna mkamilifu la hata mmoja chini ya jua.
Chuki kubwa kwa Diamond ukiachana na ile ya wivu wa wasanii wenzake na vijana washindwa wengine. Imekolezwa na yeye kuambatana na KAYAFA. Mtu aliyetajwa kwa ukatili upendeleo na roho mbaya! Kumbuka ukiwa karibu na waridi nawe utanukia lakini pia ukiwa karibu na harufu mbaya nawe utanuka!
Uzuri wa Diamond anajitambua nakuitambua nafasi yake katika jamii hivyo hazipi nafasi chuki zinazomuandama kwa namna zote.. Ukimya ni silaha maridadi sana kwa haters. Kamwe usijaribu kujibishana na hater kwakuwa hiyo ndio nafasi pekee anayoitafuta kukuumiza na kupunguza machungu yake, mnyamazie azidi kuumia.
DIAMONDS ARE FOREVER!