Kupitia mafanikio ya Diamond Platnumz nimegundua Watanzania wengi wana roho mbaya

Kupitia mafanikio ya Diamond Platnumz nimegundua Watanzania wengi wana roho mbaya

Kweli hii dunia kila mtu na mtizamo wake.

Binafsi mtu aisiyesimamia haki ni adui yangu tu hata kama aliwahi kufanya mazuri mengi kiasi gani.
Acheni unafiki wenu wa akina Kigogo!! Mnampiga kupigania haki huku mkiwa mmejificha kwenye fake IDs?!! Wanafiki aina yenu mngekuwa mnamaanisha mnachoongea yale maandamano ya Mange Kimambi ya April 26 yangejaza watu barabarani lakini hakuna aliyejitokeza halafu leo mnajifanya wapigania haki!! Yaani wakati nyie "mnapigania" haki huku mkiwa mmejificha kwenye fake IDs, mnataka mwenzenu atoke front bila bulletproof jacket?!
 
Wengi hawajamsamehe, ...niliwahi kumshauri kupitia koment za humu JF kwamba awaombe radhi watanzania.... kwani yeye anawahitaji kuliko wanavyomuhitaji, inawezekana hakuisoma ile komenti yangu.

"Hajachelewa".
Nb. Watanzania wa mitandaoni ndio watanzania halisi wanaojielewa.
Tabia ya binadamu yoyote akishakuwa na hela huangalia wa kumshauri na huchagua ushauri pia
 
Tabia ya binadamu yoyote akishakuwa na hela huangalia wa kumshauri na huchagua ushauri pia
Mdharau mwiba, mguu huota tende,....kwani kusema naombeni radhi watanzania niliowakwaza anapungukiwa nini.?

..au haoni kitakachotokea baada ya hii sumu kidogo kusambaa mwili mzima?
 
Youngblood naomba niseme haya machache

Mti wenye matunda ndio hupopolewa mawe. Kuchukiwa ni ada ya mwanadamu. Hapa duniani kila kitu kina uwili! Kukiwa na wanaokupenda basi wanaokuchukia hawakosekani, kukiwa na wanaokusifia basi wanaokukosoa hawakosekani pia.

Watu duniani kote hufurahia mabaya ya mtu kuliko mafanikio yake na ndio maana habari mbaya za watu huvuma kwa kishindo kuliko habari zake nzuri.

Diamond kijana asiye na elimu lakini mwenye mafanikio makubwa naye ana mapungufu yake..hakuna mkamilifu la hata mmoja chini ya jua.

Chuki kubwa kwa Diamond ukiachana na ile ya wivu wa wasanii wenzake na vijana washindwa wengine. Imekolezwa na yeye kuambatana na KAYAFA. Mtu aliyetajwa kwa ukatili upendeleo na roho mbaya! Kumbuka ukiwa karibu na waridi nawe utanukia lakini pia ukiwa karibu na harufu mbaya nawe utanuka!

Uzuri wa Diamond anajitambua nakuitambua nafasi yake katika jamii hivyo hazipi nafasi chuki zinazomuandama kwa namna zote.. Ukimya ni silaha maridadi sana kwa haters. Kamwe usijaribu kujibishana na hater kwakuwa hiyo ndio nafasi pekee anayoitafuta kukuumiza na kupunguza machungu yake, mnyamazie azidi kuumia.

DIAMONDS ARE FOREVER!
Hii issue ya Chuki kisa Kayafa naipinga labda kama inafanywa kichaka cha kujifichia kwa wale wengine lakini kimsingi wote sio kikwete wala Samia ambao mnawasifia sasa hawakuwa karibu na Kayafa ila kwasasa ndiyo mnawapigia vigeregere.
 
Saikolojia yako wewe ndo hatari zaidi kufikiria kwamba watu waliofanikiwa huwa hawana habari na watu walio nyuma yao kuelekea walipo wao(moja ya sababu ya matajiri kubaki kuwa matajiri ni kuwaangalia waliopo nyuma yao wanafanya nini)

Wanaojua kinachowakosesha raha WCB juu ya mmakonde ni WCB wenyewe na machawa wao isipokuwa sisi wengine tunaangalia tu game pande zote mbili jinsi zinavyoenda bila ushabiki maandazi tunaona upande upi unaoteseka

Ukiwa shabiki maandazi huwezi kuona wasanii wengine ni wazuri au wana mafanikio,ushabiki maandazi ndo utakufanya useme harmonize anajitutumua na hana mafanikio lkn ukirudisha utimamu wa akili huwezi kusema hivyo....siamini kwamba saikolojia yako inakwambia mimi namaanisha hapa harmonize amefanikiwa zaidi Diamond,simaanishi ivyo ila kijana harmonize mafanikio kimuziki anayo...wanaompenda Diamond wanamchukia Harmonize, wanaompenda Harmonize wanamchukia Diamond huo ndo ukweli japokuwa ni mchungu unatakiwa uupokee
Be specific and hit direct to the point, sababu hasa ni nini mpaka wewe ukaona baba muinua kipaji ana wivu na mwanae?
 
Nikiwa tajiri nikaa kimya na utajiri wangu na watu wakaona pia na juhudi zangu za kutafuta sidhani kama kuna mtu atanichukia au kuhangaika kunishusha ila tatizo litakuja pale nitakapo anza kujigamba Nakuanza kusema hapa "Hakuna Mwana JF tajiri kama mimi"
Kuna kitu kinaitwa wivu mkuu! Christian Ronaldo aliwahi kuulizwa mchezaji bora ni nani? Alijibu yeye na hakuna aliemchukia kisa kajisema yeye ni bora zaidi ya wengine wote
 
Wengi hawajamsamehe, ...niliwahi kumshauri kupitia koment za humu JF kwamba awaombe radhi watanzania.... kwani yeye anawahitaji kuliko wanavyomuhitaji, inawezekana hakuisoma ile komenti yangu.

"Hajachelewa".
Nb. Watanzania wa mitandaoni ndio watanzania halisi wanaojielewa.
Wa mitandaoni! Wanaoshinda mitandao ya kijamii ndo wanaojielewa?! Una masikhara sana.
 
Nikiwa tajiri nikaa kimya na utajiri wangu na watu wakaona pia na juhudi zangu za kutafuta sidhani kama kuna mtu atanichukia au kuhangaika kunishusha ila tatizo litakuja pale nitakapo anza kujigamba Nakuanza kusema hapa "Hakuna Mwana JF tajiri kama mimi"
Sijajua unaishi katika jamii gani ya watu🤔🤔🤔,
Nakuombea kwa Mungu ufanikiwe ujue walimwengu walivyo🙏🙏🙏
 
Mdharau mwiba, mguu huota tende,....kwani kusema naombeni radhi watanzania niliowakwaza anapungukiwa nini.?

..au haoni kitakachotokea baada ya hii sumu kidogo kusambaa mwili mzima?
Hakuna wa kuomba msamaha na hakuna kitakachotokea , fight alone sio mtu akupanbanie , what a nonsense thought , nchi hii mataahira wengi ....
 
Wengi hawajamsamehe, ...niliwahi kumshauri kupitia koment za humu JF kwamba awaombe radhi watanzania.... kwani yeye anawahitaji kuliko wanavyomuhitaji, inawezekana hakuisoma ile komenti yangu.

"Hajachelewa".
Nb. Watanzania wa mitandaoni ndio watanzania halisi wanaojielewa.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
JF kunavichaa kweli, yani umemshauli Diamond ila hajasoma comment yako...?
Tena nsani ya jf🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Ndugu yangu ukiambiwa unamatatizo ya kisaikolojia utakataa...?
Au ndi madhara ya mitandao,
Nnachoshindwa kabisa kukuelewa unasema ulimshauri ndani ya jf🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Habari zenu,

Kwakweli kama wote mnavyojua kijana Diamond Platnumz ni moja ya vijana wapambanaji sana katika nchi hii,ni wale vijana waliotoka from the bottom huko chini kabisa na wakafanikiwa kupata mafanikio makubwa kutokana na juhudi binafsi.

Kinachonishangaza sasa ni trend kubwa ya Watanzania hasa vijana kumchukia huyu ndugu yetu hata bila sababu za maana kabisa badala ya kujifunza kutoka kwake.

Mbaya zaidi Watanzania tumejikita kumfanya ashuke pale alipo au aonekane hana chochote wala lolote, ukipita mitandaoni huko huoni hata wanaompongeza kwa mafanikio yake, wengi utaona wanapambana kumshusha inasikitisha sana, nakumbuka hata mimi mwenyewe kuna kipindi mkumbo huo ulinipitia kutokana na habari za mitandaoni, lakini nikagundua ni majungu tu.

Vijana wa Kitanzania tuache Majungu na fitina tuchape kazi, umbea hauna posho, hatuwezi kufanikiwa kwa kipiga majungu bila kupambana.

Asanteni.
Si kweli. Watanzania wengi wangapi? Umehoji wangapi na katika nini? Sijui kama wengi wana hata muda na huyo diamond wenu.
 
Watanzania wengi wanafurahia sana mafanikio makubwa aliyoyapata lakini wakati huo huo wanakerwa na yeye kuwa kimya kuhusu DHULUMA na UDHALIMU wa yule dhalimu mwendazake wakati huo huo aliweza kutoa sauti kukemea maovu ya Serikali ya Wanigeria. Kwa hiyo hitimisho lako kwamba Watanzania wanamchukia kwa mafaniko yake makubwa haliko ACCURATE.

Habari zenu,

Kwakweli kama wote mnavyojua kijana Diamond Platnumz ni moja ya vijana wapambanaji sana katika nchi hii,ni wale vijana waliotoka from the bottom huko chini kabisa na wakafanikiwa kupata mafanikio makubwa kutokana na juhudi binafsi.

Kinachonishangaza sasa ni trend kubwa ya Watanzania hasa vijana kumchukia huyu ndugu yetu hata bila sababu za maana kabisa badala ya kujifunza kutoka kwake.

Mbaya zaidi Watanzania tumejikita kumfanya ashuke pale alipo au aonekane hana chochote wala lolote, ukipita mitandaoni huko huoni hata wanaompongeza kwa mafanikio yake, wengi utaona wanapambana kumshusha inasikitisha sana, nakumbuka hata mimi mwenyewe kuna kipindi mkumbo huo ulinipitia kutokana na habari za mitandaoni, lakini nikagundua ni majungu tu.

Vijana wa Kitanzania tuache Majungu na fitina tuchape kazi, umbea hauna posho, hatuwezi kufanikiwa kwa kipiga majungu bila kupambana.

Asanteni.
 
Unafiki na tabia yake ya kulazimisha ku-monopolise soko la muziki.

Yaani inshort anapambana kujifanya Ruge part 2.
Ndugu yangu nnabahati mbaya sana kusoma comments zako hapa jf, ila naona ubadilishe hyo profile yako. maana naona unamuaibisha sana huyo jamaa tunajua kacoment yy kumbe n pumba zako, tafuta hata profile ya madenge
 
Nimeshaoa Mkuu.
 
Watanzania wengi wanafurahia sana mafanikio makubwa aliyoyapata lakini wakati huo huo wanakerwa na yeye kuwa kimya kuhusu DHULUMA na UDHALIMU wa yule dhalimu mwendazake wakati huo huo aliweza kutoa sauti kukemea maovu ya Serikali ya Wanigeria. Kwa hiyo hitimisho lako kwamba Watanzania wanamchukia kwa mafaniko yake makubwa haliko ACCURATE.
Me nazani tukifata hyo sababu, tutawachukia wazazi wetu, wachungaji na sehemu kubwa ya ndugu zetu katka jamii tunazotoka.

Na mbona kama hao wanaotoa hzo sababu ndio wanaomsaport Alli kiba, na wasanii wengi ktk bongofreva ambao walikuwa ktk mlengo mmoja na Diamond ktk kuisuport serikali...?
 
Back
Top Bottom