Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Waziri Mkuu aunda Tume ya watu maalumu 21 - Nov 22, 2024

Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Waziri Mkuu aunda Tume ya watu maalumu 21 - Nov 22, 2024

Ni hatari sana.

Tatizo kubwa zaidi lililopo Tanzania ni kwamba Hakuna mamlaka madhubuti za kudhibiti viwango na ubora wa Majengo pamoja na ubora wa bidhaa zingine mbalimbali.
Watanzania tunaishi kwa nguvu ya Mungu tu peke yake.
Kwani ni mara ya kwanza? Likitokea tukio kama hili utasikia imeundwa kamati na matamko ya kila aina. Sku mbili tatu kila mtu kasahau. Dalili za uongo wa nyani hizi.
 
Mambo
Mambo mengine tuwe tunajiwajibisha ,wewe unajenga jengo bila kufuata standards ,unasubiri nani awajibike kama sio wewe kwanza kuwajibika ,kama si udumavu wa akili ni nini ?
Au hizo standards walioziweka ni wapumbavu , mtu hata mafundi anaitumia ni wahuni tu wa mitaani ,wewe unategemea nini hapo ?
Siyo kila mtu ana busara kama hizi, hapo ndipo inapokuja serikali na kanuni pamoja na sheria. Ni kwa nini tunajengea nyumba zetu kuta na kuweka walinzi? Kwa nini hatusubiri watu wajiwajibishe wenyewe na kuona kuwa kuiba ni jambo baya?
 
Taarifa zinadai kuwa kuna watu wengine ndani ya jengo hilo lililokuwa linakarabatiwa, huku wananchi wa Kariakoo wakiendelea na juhudi za kuwaokoa waathirika baada ya ghorofa kuporomoka katika mtaa wa Congo na Mchikichi.

 
Huzijui codes za mwisho wa mwaka siyo?
Time ni Mindset tuu ya eneo fulani.. We unapo ita mwaka wa Mwisho mwarabu ana kalenda yake mchina ana kalenda yake Korea kaskazini hivyo hivyo. Na kuna ambao hawana hizo kalenda pia.

Hizo Codes ni zipi sasa? Tunashindwa kuwa waangalifu na maswala muhimu tunasingizi mwaka wa mwisho?
Matukio mangapi yametoke nje na mwisho wa mwaka jee utayaitaje hayo?

Ni sawa na mtu anae Amini ajili barabarani sababu ni shetani mara majini. Huu ni ujinga ambao tukiendelea ushika hatutawadhibisha wazembe tukitupia lawama sehemu ambazo sio kweli.

Uzembe ndo chanzo cha matatizo mengi Barani Afrika sio sababu ya muda au kalenda.
 
Mambo
Mambo mengine tuwe tunajiwajibisha ,wewe unajenga jengo bila kufuata standards ,unasubiri nani awajibike kama sio wewe kwanza kuwajibika ,kama si udumavu wa akili ni nini ?
Au hizo standards walioziweka ni wapumbavu , mtu hata mafundi anaitumia ni wahuni tu wa mitaani ,wewe unategemea nini hapo ?
Mkuu; Uko sahihi kwa upande wa mwenye nyumba(Tajiri) lakini ujue sio wote Mtajiri wamejaliwa Pesa na Uelewa katika mambo ya Kitaalam e.g. Umuhimu wa kuzingatia viwango katika Ujenzi. Ndo mana kabla ya kujenga nyumba huwa zipo taratibu za kuzingatiwa kutoka Mamlaka za Ukaguzi na Uidhinishaji Ujenzi wa majengo (Serikali)na uidhinishaji au kutoa kibali ujenzi ufanyike na pia mamlaka hizo hufanya ukaguzi kwa kila hatua ya ujenzi na kutoa certificate. Hizo Mamlaka ndizo zenye DHAMANA ya usalama wa jengo husika na Hutumia Kodi zetu kutekeleza wajibu wao huo. Hao ni Waajiriwa Serikalini ni Watumishi wa Umma. i.e. Ni vijana wetu na tunawalipa kwa kodi zetu.
Kwa mantiki hiyo sio vyema sana kumwita mwenye jengo kuwa anaudumavu wa akili ilhali amewaamini wenye Taaluma husika (vijana wetu)ambao waliidhinisha kazi iendelee. Hao Wataalam waidhinishaji ndio wanatakiwa wawe Na.1 WAWAJIBISHWE kwanza halafu ndo ufuatiliaji wa kina ufanyike kuwabaini na wale wengine wote waliohusika katika UZEMBE huo nao pia wawajibishwe ikiwa ni pamoja na huyo mwenye jengo (Hata kama kulikuwa na kitu kidogo TAKUKURU watajua hilo.
Pole nyingi kwa waathirika wa Tukio hilo - Ndo nchi yetu hii vituko haviishi ila tunaumia.
 
Back
Top Bottom