Kupost mafanikio yako mtandaoni sio tatizo. Jamii inahitaji kuona mafanikio, sio malalamiko tu

Kupost mafanikio yako mtandaoni sio tatizo. Jamii inahitaji kuona mafanikio, sio malalamiko tu

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
KUPOST MAFANIKIO YAKO MTANDAONI SIO TATIZO. JAMII INAHITAJI KUONA MAFANIKIO, SIO MALALAMIKO TUU

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Watu wengi wameaminishwa kuwa kupost mafanikio yao ni kujisifu au kujionyesha. Wengine Wana negative mind, Mila potofu zinazokaribiana na shirki kuwa ukipost unaalika vijicho, roho ya husda na ulozi. Kwamba ukipost mambo yako yataharibika.
Lakini ukweli ni tofauti kabisa.

Kupost mafanikio yako ni kutoa mwanga wa matumaini kwa wengine. Ni kuwaambia watu kuwa inawezekana. Ni kuwapa nguvu wale wanaopitia changamoto waamini kuwa kesho inaweza kuwa bora.

Tatizo si mafanikio kupostiwa tatizo ni ile propaganda inayotaka kuifanya jamii izoe giza la malalamiko, kushindwa, na kukata tamaa. Kila siku tunaona watu wakisambaza sumu ya maisha magumu, hakuna pesa, kila kitu ni shida… na polepole hiyo inakuwa “normal”. Inaingia katika akili za watu.

Ukiwapa watu moyo utaitwa motivational speaker kwa namna ya kukukejeli. Lengo ni kuacha Ile nguvu hasi ibaki katika vichwa vya watu ndani ya jamii.

Jamii isiyopenda kuona mafanikio haiwezi kufanikiwa. Jamii inayoficha mafanikio ni jamii ambayo itaendelea kubaki gizani na katika shimo la umaskini Milele.

Kwa watu wenye Akili, mafanikio huonyeshwa waziwazi. Lakini watu wajinga mafanikio hufichwa. Kisha matatizo huwekwa hadharani.
Wakati wenye akili huyaficha matatizo na kuyatafutia ufumbuzi na utatuzi.

Kwenye familia, Baba na Mama wakizoea kutaja taja Matatizo na shida huunda fikra kwa watoto za Matatizo na shidashida. Unapozungumzia matatizo na shida mara kwa mara unatengeneza malalamiko na kushindwa. Wakati wanaozungumzia mafanikio hutengeneza uwezekano na Ushindi.

Kama mtibeli, Mbobezi wa masuala ya saikolojia na social intelligence nitakupa mfano wa katika Vita. Case study ni Vita ya Iran Vs Marekani ft Israel. Mara zote utasikia Kila nchi ikitaja mafanikio na ushindi kuliko Kushindwa. Wakati mwingine hutumia propaganda kuutaja ushindi. Lengo ni kuhamasisha na kuleta positive energy kwa Wapiganaji na wananchi.

Moja ya Sababu ya Maendeleo ya uchagani ni pamoja na kanuni ya kutoficha maendeleo na mafanikio. Wao huyaonyesha mafanikio na maendeleo waziwazi nyumbani na hiyo huwatia hamasa vijana wadogo kutafuta zaidi.
Mchaga akijenga nyumba ikiisha huita ndugu jamaa na Rafiki kufurahia pamoja.
Mchaga mtoto akifanikiwa Kila hatua labda ni kiwango Fulani cha elimu huweka sherehe na kusherehekea. Hii inawapa jamii nyingine hamasa.

Elewa
👉 Mafanikio yanaposhirikishwa na kupotangazwa yanazalisha hamasa
👉 Hamasa inaleta juhudi
👉 Juhudi zinazaa mafanikio mengine

Lakini vipi mafanikio yakifichwa?
Matokeo Yake ni jamii kupoa na kupoteza hamasa.

Hivyo usiogope kupost mafanikio yako.
Huenda post yako ndiyo itakayompa mtu nguvu ya kuendelea kupambana.

Ni utapeli na propaganda za watu waovu kusema usiposti furaha yako au mafanikio yako. Huo ni uchoyo. Kama ulikuwa hujui.

Kwamba mmefunga harusi, unafurahia ndoa na mkeo na mumeo onyesha kwa watu ili vijana wengine wajifunze na wapate moyo kuwa kumbe inawezekana. Kumbe ndoa ni furaha. Watu wabaya hupenda habari mbaya na huchukizwa kuona habari njema.

Ukiona MTU yeyote ambaye anasema usiposti wala usitangaze mafanikio yako. Na anaumizwa na kuona mafanikio ya wengine yanayopostiwa ujue huyo anamoyo wa ubaya, uchoyo na wivu wa kichawi.
Yeye akiona mabaya ndio huchekelea.

Umenunua gari mpya. Posti.
Umejenga nyumba posti.
Umemaliza shahada posti.
Umepata watoto posti.
Umenunua kiwanja posti.

Kikanuni hutakiwi kuposti au kusema mipango na mikakati yako. Hiyo ni siri ya jeshi na siri ya ushindi.
Ila kuposti ushindi wenyewe sio tatizo.

Ingawaje usiposti kwa majivuno au kiburi kuwananga ambao hawajapata. Bali unaposti kama sehemu ya ushuhuda na shukrani kwa Mungu na kutangaza kuwa Mafanikio yapo wala sio uongo. Na yanawezekana.

Narudia,
Usiposti mipango, ndoto, malengo na malengo. Kwani hayo ndio MTU anaweza kukuhujumu. Lakini mafanikio unaweza kuposti.

Kuhusu kushindwa baada ya kuposti.
Inaweza kutokea ukaposti mafanikio yako alafu ukaanguka.
Iko hivi hutaumia kama ulifanya kwa Nia Njema. Kama ulifanya kwa kuwatia waliochini moyo, kuwapa hamasa, hutaumia.
Lakini kama ulifanya kwa kujionyesha, kwa kiburi na majivuno hakika utaumia sana.

Kingine kutokuposti haimaanishi hautashuka. Kushuka kupo tuu
Pia. Kama wewe moyo wako ni wakiburi hata usipoposti ukishuka na kuanguka utaumia tuu na kuona aibu na fedheha kwa watu hata kama hukuwahi kuposti kokote.

Mwisho kabisa, vijana msione haya kuposti mafanikio yenu. Tangazeni mafanikio yenu. Ni sehemu ya kutangaza habari njema ya Mungu. Ni matokeo ya kufanya kazi. Moja ya mahubiri makubwa ni kutangaza mafanikio.
Wakati shetani mahubiri yake ni kutangaza kushindwa na habari mbaya.

Kufikia hapo sina la ziada.
Nawatakia Sabato Njema

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Na wanaozungumzwa ni wenye mafanikio na sio wanyonge 😎

Imekua desturi watu wakiambiwa waache kuposti mafanikio yao kisa kuna wenye wivu au wataumiza wengine. Huo ni uhuni na kuendekeza Giza.

Wewe badala uhamasike ati unaumia mwingine akipost mafanikio. Naye anaacha kuposti ili usiumie😂😂
 
Unawajua Waswahili wabongo? Is not about what you attained in life ila hawawezi kuvumilia kuona unafanikiwa ktk macho yao

Hawawezi kukuroga ila unakuwa una trigger jealous with no reason

Hizo fikra ndizo zinatakiwa ziwe eliminated ndani ya jamii.
Jamii nyingi za Kiafrika haziendelei kwa sababu hii.
 
Hizo fikra ndizo zinatakiwa ziwe eliminated ndani ya jamii.
Jamii nyingi za Kiafrika haziendelei kwa sababu hii.
Yes ila lazima ujue njia sahihi za kuishi na watu wanaokuzunguka

Privacy is power

Unaweza kuwa fuckedup with no reason .

Na hii haipo Africa dunia nzima

Unachopata is nothing ila unachofanya baada ya kupata pesa matter most .
 
Yes ila lazima ujue njia sahihi za kuishi na watu wanaokuzunguka

Privacy is power

Unaweza kuwa fuckedup with no reason .

Na hii haipo Africa dunia nzima

Unachopata is nothing ila unachofanya baada ya kupata pesa matter most .

Privacy ipo kwenye malengo, mipango, mbinu na mikakati.
Kwenye matokeo hakunaga privacy

Mfano, Kulombana ni privacy.
Mimba inaweza kuwa privacy na nusu sip privacy Kwa sababu inaonekana.
Watoto sio privacy Kwa sababu ni matokeo
 
Mafanikio yako ni mabadiliko kwa wengine
I used to think the same ila mambo kama HAYO unabidi kufanya tayari upo secured

Hauwezi ukawa unakaa na jamii ambayo 99% ni masikini then una expose ur accomplishment

Uje utakuwa fuckedup soon as possible

Hapa sizungumzii kurogwa NO nazungumzia kufanyia hujuma ambazo ni mbaya.

Ndo maana ukiona umeshafanikiwa tafuta mazingira safe ukaishi huko yenye watu wanaojitambua

Hakuna njia yoyote uta motivate masikini ili na yeye afanikiwe

Haipo zaidi zaidi uta trigger jealous
 
Naunga mkono hoja , masikio yetu wamatumbi yapo tayari kusikia negative kuliko positive , ukiwaeleza jinsi unapitia shida utaona wanavyo kuhurumia , utasikia Mungu akutie nguvu siku moja utafanikiwa , ila ukishafanikiwa , ukiwaonyesha mafanikio wana nuna mara anaringa mara ngoja ataona akavyofilisikia .

Ukizipata mtu asikupangie namna ya kuzitumbua gademit :
 
Back
Top Bottom