Kupost mafanikio yako mtandaoni sio tatizo. Jamii inahitaji kuona mafanikio, sio malalamiko tu

Kupost mafanikio yako mtandaoni sio tatizo. Jamii inahitaji kuona mafanikio, sio malalamiko tu


😄😄😄

Wewe unachojadili ndio kipo duniani. Ni mfumo uliowekwa na unanifaisha wachache hasa waovu na kutesa wengi.

Ila mfumo ninaoueleza nu mfumo unaotakiwa na unanufaisha jamii nzima.

Fikiria MTU akijiita maskini kwako na jamii it's okay.lakini akijiita tajiri kwako na jamii mnaona nongwa na tabu.

Huoni gap?
 
😄😄😄

Wewe unachojadili ndio kipo duniani. Ni mfumo uliowekwa na unanifaisha wachache hasa waovu na kutesa wengi.

Ila mfumo ninaoueleza nu mfumo unaotakiwa na unanufaisha jamii nzima.

Fikiria MTU akijiita maskini kwako na jamii it's okay.lakini akijiita tajiri kwako na jamii mnaona nongwa na tabu.

Huoni gap?
Waovu na wema wapi wengi hapa duniani ?
 
Unachoeleza ni mfumo uliodizainiwa ili kuificha nuru chini ya uvungu. Badala kuweka kwenye kianga.

Fikiria mtu kusema yeye ni maskini kwenye jamii hii ni okay lakini kusema yeye ni tajiri watu wanaona sio Okay.
Huo ni mfumo tuu.

Hiyo mifano uliyoitoa haibadilishi hoja Yangu. Na haifanyi hoja Yangu kuwa dhaifu.

Hao uliowataja wote wapo ndani ya mfumo na wanamawazo labda kama yako

Lakini mtu kuonyesha mafanikio yake hiyo ndio lilikuwa lengo la maisha.
Watu dhaifu ndo hujitutumua na kutafuta kuonekana kuwa matajiri na wasipopata sifa huumia.

Ila tajiri au mtu aliyefanikiwa hakuna haja ya kujitangaza utamjua mwenyewe

Umasikini na utajiri sio vitu vya kutangaza vitaonekana Kwa matendo.

Hata mtu mjinga anajua kuwa Tanzania ni masikini dhidi ya Taifa kama Marekani, hata TANZANIA ajionyeshe amefanikiwa
 
Mfanyie kitu gani SASA?
Vya kufanya ni vingi tu unapoanza kututambia na kutuonesha utajiri na mafanikio yako.

Washirikina na wachawi tutakuroga.

Tusiokuwa washirikina na wachawi tutaenda mpaka kazini kwako kukupikia majungu kwa bosi wako akufukuze kazi kwa kua unamuibia bosi ndo mana unafanikiwa.

Wengine wakipata upenyo watakuteka au hata kukuua watakuua.
Jamii inahitaji ukombozi.
Ukombozi wa nini?

Wa kwamba ukifanikiwa basi uoneshe mafanikio yako?

Nakuhakikishia mtu yoyote mwenye akili timamu hawezi kukushauri huo upumbavu.
Ndio maana waliofanikiwa mnawaita Wezi na wachawi kutokana na tabia zenu za husda na chuki.
Lazima tukuite hata kama tunajua sio mwizi na mchawi.

Kiubinadamu lazima roho ikuume unapoona mwenzio anefanikiwa kuliko wewe.

Ukitutambia unatuumiza zaidi lazima tutafute jinsi ya kukushusha tuwe sare.

Usidhani kina MO na Bakhresa ni wapumbavu wanajua wanachokifanya.
Kwamba mtu asionyeshe mafanikio kisa kuogopa watu wenye negative energy?
Unajua hiyo ilitokea wapi?
Achana na negative energy ambayo hipo kiimani zaidi.

Watu tutadili na wewe physically unapoanza kututambia mafanikio yako.

Tutaenda kwa bosi wako kukupikia majungu.

Kama una biashara zimekunyookea tutaanza kumshauri aliyekupangisha frame akuzidishie kodi au akufukuze sisi tutalipa hela kubwa kuliko yako.

Kwa kifupi ukifanikiwa na ukianza kutatambia mafanikoo yako uwe umejipanga sana.
Hiyo imetokea kwenye Jamii za kichawi na kishirikina.
Hapana sio kwenye jamii za kichawi na kishirikina tu.

Hii ni kwenye jamii zote duniani.

Iwe jamii ya kidini au kichawi wivu chiki na husda kwa aliyefanikiwa ni lazima.

Hii ni asili ya mwanadamu kuchukia mafanikio ya mwenzie.

Ukibaki low profile inapunguza mashambulizi huku wewe unaendeleza mambo yako na kuendelea ku accumulate wealth kimya kimya.

Ukitutambia na ki Toyota crown au ki IST chako lazima tutafute namna ya kukushusha.

Hii ni kwenye jamii zote.

Hata huko kwa wazungu mambo no hayo hayo.
 
Back
Top Bottom