Tanzania kumekuwa na tatizo kubwa la ajira. Njia moja ya kuondoa hilo tatizo ni kwa watu kutafuta kazi za kufanya online, yaani mitandaoni. Kazi zipo nyingi. Mfano, waweza pata kazi ya kutafsiri website ya kampuni au mtu kwa Kiswahili au kutafsiri kitabu. Unafanya online malipo yanakuwa kwa njia ya PayPal hata kwenye simu yako ya mkononi, hata mwajiri au mnunuzi awe Ulaya au Marekani
Pia, mtu waweza chora hata katuni, ramani za nyumba n.k ukauza online. Au, ukajitungia wimbo wako wa kienyeji binafsi nyumbani kwako bila hata kwenda studio, ukauweka kwa mfumo wa video au audio ukauuza online kwenye maduka kibao ya online.
Tatizo kwa Tanzania haijaruhusu matumizi ya kupokea pesa kwa njia ya PayPal ambapo mtu aki-click tu kununua bidhaa yako, pesa yako inaingia chapchap kwenye PayPal account yako.
Kenya walisharuhusu; vijana wengi hushinda mitandaoni wakitengeneza pesa wakiuza bidhaa zao, viwe vichekesho