KURA: Je, ni nani kati ya Freeman Mbowe na Tundu Lissu anayefaa zaidi kuiongoza CHADEMA kwa Sasa?

Je, ni nani kati ya Freeman Mbowe na Tundu Lissu anayefaa zaidi kuiongoza CHADEMA kwa Sasa?

  • FREEMAN AIKAEL MBOWE

    Votes: 124 18.2%
  • TUNDU ANTIPAS LISSU

    Votes: 559 81.8%

  • Total voters
    683
  • Poll closed .
Dj Mbowe ameshalamba asali vya kutosha toka anaitwa kijana na mpaka sasa anajiita kijana,tufanye inatosha aende sasa kucheza na wajukuu na tunashukuru kwa mema yake na mabaya tutamsamehe kama akitaka kuachia kwa hiari ila asije akajichanganya ili wahuni tuchukue kinguvu hakuna rangi hatoacha iona.
 
Mbowe anafàa sana ,sema kitu ambacho unatakiwa ukijue ni kwamba confrontation politics kwa nchi yetu haifai sababu raia ni waoga mfano wa kuku wa kienyeji .Pale kiongozi wa chama anapotekea amekamatwa basi kiongozi atateseka peke yake raia hawaoneshi mshikamano kwa kuonesha kashi kashi kama vile raia wa Kenya kuishinikiza serikali imuachie kiongozi wao badala yake watu wanakuwa keyboard worrior huku kiongozi akiteseka yeye na familia yake . Uwoga kwa wanachama kutokuwa na moja na viongozi wao kuna wafanya hata viongozi ku dance kwa step wanapofanya mapambano . Lisu ni sawa anaweza confrontation politics lakini jua ya kwamba huyu familia yake ipo ulaya yeye anachofanya ni kuchafua chafua lakini sio kwa lengo la dhati ,yeye anacho taka ni ili kupata political mileage ya watoto na mke wake waishi ulaya ukitambua ya kwamba huyu anatambulika kama mkimbiziwa kisiasa .
 
Kama tuihubiri DEMOKRASIA ya kweli Nchini,
Tusisite kumwambia ukweli Mbowe asisite kuachia kijiti Cha uongozi Kwa wengine.
Kama aliaminiwa na waasisi waliomtangulia yeye hana budi pia kuwaamini wengine pia
Kwa maslahi mapana ya Chama na Taifa kiujumla TUNAENDA NA LISSU
 
Nadhani hofu yao kubwa nikukikabidhi chama kwa mamluki.
Ngoja muda utasema
 
ONYO
TEAM KUTOKA MTAA WA LUMUMBA NAOMBA MKAE MBALI MAANA HII SHOW ,NYIE ENDELEENI NA SHOW YENU ALIYE SEMA MWANACHAMA MWENZENU WA BUKOBA YA KUTUTEKA NA KUTUUA ILI MWISHO WENU NDIO HUYU
TALM.
 
HiviNadhani hofu yao kubwa nikukikabidhi chama kwa mamluki.
Ngoja muda utasema
Ni kweli na wanahoja ya msingi
Na hata Mimi binafsi namuona Lissu kama anaumamluki fulani hivi
Lakini mbowe pia ana kaudikteta Fulani
Shida ni kwamba Kwa Kuwa mbowe ameonyesha kuuza chama Kwa watawala na chama kimepoteza mvuto basi hana budi kumwachia mwenzie
 
Pigakura moja tu,

Kwanza, Gusa jina la Unayedhani anafaa kuiongoza CHADEMA kwa Sasa,

Pili, Bonyeza sehemu imeandikwa "Cast Vote"

Mwisho unaweza kuacha ujumbe wa kikampeni kwa wachangiaji wanafuata.
Wewe umepiga?
 
Huu mnyukano ni balaa aisee
 
Pigakura moja tu,

Kwanza, Gusa jina la Unayedhani anafaa kuiongoza CHADEMA kwa Sasa,

Pili, Bonyeza sehemu imeandikwa "Cast Vote"

Mwisho unaweza kuacha ujumbe wa kikampeni kwa wachangiaji wanafuata.
Pigakura yako
 
Mbowe yuko soft sana kwa maCCM. Right now we need confrontational politics....eye to eye politicking
Huwezi kushindana na dola kwa kupayukapayuka siasa sio uwanaharakati CDM kilikuwq chama cha uharakati sana ila Lowasa aliwafunza thatwhy uliona matokeo yake
Serekali haswa hizi za kiafrika ukijidai una mdomo sana unapotezwa na hakuna chochote utakachofanya
Ok let's say Lisu amepewa kiti then aje na mataamko yake atatulizwa tu itatoka amri hakuna harakati za kisiasa hadi uchaguzi na hakuna mikutano ya ndani wala nje utafanyia wapi siasa zako
Ukileta ujuaji unachezea kesi hadi unafia jela au mahakaman
 
Haya ni mawazo yako na yatabakia kuwa yako
 
Chadema bado inamhitaji Mbowe kwa nyakati hizi. Wanaharakati kupewa Chama kwa nyakati hizi itawawia ngumu kufanya kazi kutokana na miongozo ya vyama vya siasa chini ya Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa.
Kama Lisu hafai kwa sasa,Ina maana CHADEMA mwanzo walitaka Watanzania wampe uraisi mwanaharakati ,lakini mwanaharakati asiefaaa kuwa Mwenyekiti anafaa kuwa raisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…