Nadhani mjadala huu unatupeleka mbali na mijadala yenye tija kwa maisha yetu ya kila siku.Mambo ya madini,uwekezaji,ubinafsishaji wa masharika ya umma,haki kamili ya raia,uhuru wa kutoa mawazo, kuabudu na mengi mengine.
Kwa maoni yangu mimi.Mjadala huu wa serikali ngapi zinafaa sio swala lenye manufaaa bali madhara kwa raia walio wengi.Kwa wakati huu ni wakati wa kuimarisha EAC,na sio kujaribu kujitenga,kubaguana,wakati sote ni Waafrika wamoja,ni binadamu na zaidi ya yote,wahenga walisema "Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu"Sisi hao hao tunaowafundisha watoto wetu juu ya umoja,ndio hao hao tunaowafundisha kutengana na kubaguana.Naomba tuache,Mungu hakuweka mipaka,aliweka Dunia na binadamu,dini zetu hata za asili zinatufundisha upendo,leo tunakwenda wapi?
Kama ni kwenda mbele basi leo hii tungekuwa tunafikiria juu ya Serikali Moja,Africa Mashariki moja,Afrika moja,na dunia moja kama ilivyo.
La pili sisi kwa mila zetu za ki-Afrika zote tunaogopa laana,na kwenda kinume na wosia wa marehemu.Tunaheshimu sana wosia wa wazee wetu.Wazee hawa wawili walioasisi muungano huu,walishatoa wosia,hawapo tena,si hekima kuvunja wasio huo,tutajiletea laana mbaya,na mauaji mabaya sana!Walikuwepo,tungekataana nao wakati ule ule!Nyerere na Karume.Tumeona katika maisha yetu au kusikia yanawapata wale wanaoachiwa laana pale wanapokwenda kinyume na wosia,usiombe yakukute ndugu yangu!
Hekima ututawale badala ya uchu wa madaraka,na kulazimisha kufanya tu kwa sababu tuna nguvu au akili!
Samahani kwa watakaokwazika.