Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Muundo upi wa Muungano unafaa?

  • Serikali 1

    Votes: 81 23.3%
  • Serikali 2

    Votes: 22 6.3%
  • Serikali 3

    Votes: 241 69.5%
  • Sijui

    Votes: 3 0.9%

  • Total voters
    347
  • Poll closed .
Serikali tatu,miaka mingapi ya Muungano huu watu wanalalamika?bota tatu kuondosha mjadala.
 
Kira mtu aende kufanya kazi zake za kujiongezea kipato.mjadala unakoelekea hakuna nia njema kwa walio wengi walioko bungeni.wanaopinga serikali tatu kuwa itaongeza garama mbona kila siku nchini hapa tanzania kila kukicha wanaongeza vitongoji.vijiji.kata.mitaa.tarafa.wilaya.na mikoa.? Rakini mbona wanakazana kuifuta historia
Ya Tanganyika.wote wanaojifanya wanataka uwazi walete mkataba wa muungano bungeni.
 
Nadhani mjadala huu unatupeleka mbali na mijadala yenye tija kwa maisha yetu ya kila siku.Mambo ya madini,uwekezaji,ubinafsishaji wa masharika ya umma,haki kamili ya raia,uhuru wa kutoa mawazo, kuabudu na mengi mengine.

Kwa maoni yangu mimi.Mjadala huu wa serikali ngapi zinafaa sio swala lenye manufaaa bali madhara kwa raia walio wengi.Kwa wakati huu ni wakati wa kuimarisha EAC,na sio kujaribu kujitenga,kubaguana,wakati sote ni Waafrika wamoja,ni binadamu na zaidi ya yote,wahenga walisema "Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu"Sisi hao hao tunaowafundisha watoto wetu juu ya umoja,ndio hao hao tunaowafundisha kutengana na kubaguana.Naomba tuache,Mungu hakuweka mipaka,aliweka Dunia na binadamu,dini zetu hata za asili zinatufundisha upendo,leo tunakwenda wapi?
Kama ni kwenda mbele basi leo hii tungekuwa tunafikiria juu ya Serikali Moja,Africa Mashariki moja,Afrika moja,na dunia moja kama ilivyo.
La pili sisi kwa mila zetu za ki-Afrika zote tunaogopa laana,na kwenda kinume na wosia wa marehemu.Tunaheshimu sana wosia wa wazee wetu.Wazee hawa wawili walioasisi muungano huu,walishatoa wosia,hawapo tena,si hekima kuvunja wasio huo,tutajiletea laana mbaya,na mauaji mabaya sana!Walikuwepo,tungekataana nao wakati ule ule!Nyerere na Karume.Tumeona katika maisha yetu au kusikia yanawapata wale wanaoachiwa laana pale wanapokwenda kinyume na wosia,usiombe yakukute ndugu yangu!
Hekima ututawale badala ya uchu wa madaraka,na kulazimisha kufanya tu kwa sababu tuna nguvu au akili!
Samahani kwa watakaokwazika.
 
Ifike mahala tuwe wawazi kwa kupiga kura kwa wananchi kwa kuuliza swali la kuchagua kwamba unataka muungano uwe na sirikali ngapi? (A) 1 (B) 2 (C) 3 ( ) Baada ya hapo kura za nji nzima zitahesabiwa na kutolewa matokeo. Kama ulinzi utakuwa mkali pasitokee kuchaka chua mawazo ya wananji wote yatapatikana. Wapiga kura wawe watanzania wote 18+ years wenye timamu akili.
 
3.Serikali tatu


Ili kuweza kumbukumbu sawa iliyozikwa makusudi na hvyo kuweza kurejesha histori sahihi ya Watanganyika na hvyo kujenga upya heshima, utu na kutaminiwa kulikotukuka kwa watu wa bara.

Kupunguzia mzigo mzito kwa walipa kodi wa tanganyika kwa zanzibar imekuwa mzigo mzito kwa walipakodi wa Tanganyika.

Kuleteleza usawa kwa kila upande katika nyanja zote za kiuchumi, kijamii na hata kiutamaduni lakini pia kisiasa.

Kutengeneza mwazo mzuri wa kudhibiti kuenea kwa kasi kizazi cha KI-ZANZIBAR ndani ya aridhi ya Tanganyika ambacho kimekuwa kikienea kwa kasi ndani ya aridhi ya Tanganyika kwa kwa mikoa iliyokuwa mbali sana na ukanda wa pwani na hivyo kuwapelekea kufaidi watakavyo matunda na mazuri lukuki ya Tanganyika huku wakikosa shukrani Kwa WATANGANYIKA zaidi ya kebehi, dhihaka, matusi e.t.c



MUUNGANO WA SERIKALI 3 NDO MWAFAKA KWA KUJENGA USAWA NA HAKI SAWIA KWA KILA UPANDE WA NCHI WASHIRIKA!!!!!!!!!!!!.
 
Wanaotaka Serikali Mbili Et Wao Wapo Sahihi Na Siyo Wabinafsi Na Siyo Waroho Wa Madaraka Ila Kwa Mtanganyika Kudai Serikali Yake Et Ni Mroho,mbinafsi Na Ni Mchoyo!! Hv Kama Wao Wazanzibar Ni Wakarimu Sana Kwanini Wasiiue Serikali Yao Ili Ibaki Serikali Moja?Au Kama Muungano Wanata Iwe Ni Wa Serikali Mbili Kwanini Serikali Ya Zanzibar Isife Ili Ubaki Muungano Wa Serikali Ya Tanganyika Na Ya Muungano Wa Tanzania? Hebu Tufikiri Hvy.
 
Tumekuwa tukishuhudia mvutano mkali kati ya maoni ya wananchi kupitia tume ya Warioba kwa upande mmoja na mtazamo wa ccm kupitia kwa jk kwa upande mwingine juu ya muundo wa muungano. Ccm wanasema ili kumaliza kero ni kuwapa kile wanachotaka wazanzibar, sasa je, kuungana ni kugawana mambo ya muungano? Wananchi waliona mbali kwamba ni bora kila mshirika wa muungano ashughulikie mambo yake.🙂
 
Acha kuota bila kulala muungao lazima udumu kwa neema za bwana hakuna shetani yoyote atakayeweza kuuvunja muungano unamanufaa makubwa kwetu sote watanzania.
 
Tumekuwa tukishuhudia mvutano mkali kati ya maoni ya wananchi kupitia tume ya Warioba kwa upande mmoja na mtazamo wa ccm kupitia kwa jk kwa upande mwingine juu ya muundo wa muungano. Ccm wanasema ili kumaliza kero ni kuwapa kile wanachotaka wazanzibar, sasa je, kuungana ni kugawana mambo ya muungano? Wananchi waliona mbali kwamba ni bora kila mshirika wa muungano ashughulikie mambo yake.🙂
Nadhani jk hukumsikiliza umeokota maneno yako ulikoyatoa ukaja kuyabandika hapa hebu jitafakari vizuri uliyoandika hapa kweli ndiyo ambayo jk aliongea kama ulimsikiliza kweli.
 
Japokuwa sijaelewa ulichokiandika lakini shida kubwa ya huu Muungano ni upendeleo wa upande mmoja,Wanzanzibari.
1.Wao ruksa kuwa na serikali yao na nchi yao lakini sio kwa Tanganyika
2.Wao ni ruksa kutuamulia mambo yetu katika bunge la Tanganyika ambalo vile vile huitwa la JMT ,Kwa maana wakati wa mjadala wa mambo yasiyokuwa ya Muungano hawatolewe nje wanakiwemo na wanatufanyia maamuzi! Subutu yetu sisi tufanye hivyo upande wa pili.
3.Wao ni ruksa koungoza wizara zetu hata kama sio za muungano lakini kwa mtanganyika hawezi fanya hivyovupande wa pili.
4 Wao wana ruksa ya kuwa Raisi wa Tanganyika na sio vinginevyo kwa upnde wa pili.
5.Wao ruksa kimiliki ardhi Bara lakini sio mtanganyika kile visiwani.
 
Nadhani jk hukumsikiliza umeokota maneno yako ulikoyatoa ukaja kuyabandika hapa hebu jitafakari vizuri uliyoandika hapa kweli ndiyo ambayo jk aliongea kama ulimsikiliza kweli.

Yawezekana wewe ndo hukumsikiliza jk vzr, alisema kila kitu ruksa kwa wazanzibar.
 
Acha kuota bila kulala muungao lazima udumu kwa neema za bwana hakuna shetani yoyote atakayeweza kuuvunja muungano unamanufaa makubwa kwetu sote watanzania.
Muungano unaosimamia Zanzibar huru na Tanganyika huru hauepukiki. Hivyo Tanganyika huru kwa sasa haipukiki. Hata wapige mkwara ukweli ndo huo!
 
Samahani Mimi sina shule ila kama tuliweza kuvunja Azimio la Arusha kwa sababu ambazo walizijuwa wenyewe Leo hii watu wamechoshwa na Muungano wakubwa wanataka mawazo yetu iweje? Mtazamo wangu kila nchi iwe huru
 
Haya maccm ndiyo ving'ang'anizi wa muungano. Haya maccm maoga kuwaambia ukweli wazanzibar kuwa ndio chanzo cha kuvunjika muungano. Badala yake yanalalamikia Watanganyika hawataki muungano. Kama wana hoja waende Znz kufanya mkutano kama wa Mwembe yanga. Viva Tanganyikaaaaa!!
 
Baada ya miaka hamsini ya muungano ambao una serikali mbili ya muungano na ya zanzibar basi sasa ni wakati muafaka kupitia katiba mpya kurekebisha kidogo style ya serikali, kuwepo na serikali mbili lakini ziwe ya tanganyika na ya muungano hapo ndo kero zote za muungano zitaisha.
 
Ninacho shangaa Mimi watanganyika hawaitaki Tanganyika inapaswa tuwe wazalendo wa kweli tuache unafiki.
 
Back
Top Bottom