Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Muundo upi wa Muungano unafaa?

  • Serikali 1

    Votes: 81 23.3%
  • Serikali 2

    Votes: 22 6.3%
  • Serikali 3

    Votes: 241 69.5%
  • Sijui

    Votes: 3 0.9%

  • Total voters
    347
  • Poll closed .
Zilizoungana ni nchi huru mbili Tanganyika na Zanzibar na kufanya nchi moja Tanzania. Na kwa kuwa Zanzibar kwa katiba yao mwaka 2010 wanasema wao ni nchi, jibu ni jepesi sana inabidi Tanganyika nayo iwe huru.Tupeni serikali ya Tanganyika. Serikali tatu zinatosha kabisa
 
Ingependeza hivyo ila kwa mazingira ya sasa unadhani kunahata kanafasi kakuweza kurudi hapo??
Nafasi ipo ila nategemea na utashi wa kisiasa na uwazi katika kujadili masuala ya muungano. Viongozi wetu hasa wa kitanganyika siyo wawazi sana linapokuja suala la muungano. Ndio maana hata kwenye Tume ya Warioba wengine walipendekeza serikali tatu lakini sasa ni wanazi wa serikali mbili.
 
Mpango mzima ni tatu tu hz zingine kung'ang'ania ni mbili kwa masilahi Yao binafsi sababu ya mhimu someni katiba ya zanzibar inasemaje ile ni nchi na mipaka yake ss nn maana yake et mnasema serikal mbili wakati tayr Kuna tatu kikubwa ziboreshwe hz srrikali tatu
 
TATU serikali ya tanganyika ,ya zanzibar na ya jamhuri
 
Serikali tatu ndo suruhisho za kelo za muungano. Wazanzibary walishaamua hivyo katika maboresho ya katiba Yao na Zanzibar sasa ni moja ya nchi huru ndani ya muungano.
Viongozi wa ccm bara waache unafiki kwa kung'ang'ania ujinga wa kulishwa mapumba wakadhani ni mchele. Kwao wanaitaji kura za bule za raisi wa muungano katika mfumo kandamizi wa sasa hii hali watanganyika hawampigii kura raisi wa zenji.

Serikali tatu itasaidia kuinua uchumi wa kila nchi pasipo kuingiliana na kuwekeana misingi bora ya kukuza uchumi wa pamoja kwa kukubaliana na kuondoa manunguniko ya mkubwa kummeza mdogo au mkubwa kuonekana anamlisha mdogo kwa kila kitu.
 
Serikali tatu mpango mzima kama kuna mbadala ni moja tu vinginevyo ni wizi mtupu ukubali ukatae.
 
S3 majanga!! tuangalie hii: CUF itawale Zanzibar, CCM itawale Tanganyika, Serikali ya shirikisho itawale CHADEMA.. 'naamini ikiwa hivi hali ya hatari itatokea katika nchi yetu TZ. Tuwe makini wa TZ.
 
S3 majanga!! tuangalie hii: CUF itawale Zanzibar, CCM itawale Tanganyika, Serikali ya shirikisho itawale CHADEMA.. 'naamini ikiwa hivi hali ya hatari itatokea katika nchi yetu TZ. Tuwe makini wa TZ.

Fikiria Zanzibar full madaraka siku ya siku CUF imeongoza na muungano CCM au CHADEMA nambie kuna amani hapo. Mimi naamini mambo yote yanahitaji nia na malengo ila kama hakuna mambo hayo mawili hata ingekuwa moja majanga tupu. Natuache unafiki kusema tuna s2 wakati uhalisia ni tatu.
 
S3 majanga!! tuangalie hii: CUF itawale Zanzibar, CCM itawale Tanganyika, Serikali ya shirikisho itawale CHADEMA.. 'naamini ikiwa hivi hali ya hatari itatokea katika nchi yetu TZ. Tuwe makini wa TZ.

Basi kama tatu hesabu zako ndo hizo, tuwe na moja. Hao Tanzania visiwani wafute hiyo Zanzibar kama ilivyo huku bara. Kama ingekua moja hizi kelele zote usingezisikia mkuu.
 
Charles kikoti: maridhiano ndiyo njia pekee iliyobaki kufanikisha upatikanaji wa katiba mpya itakayodumu kwa miaka 50 ijayo japo kutakuwa na mabadiriko madogo dogo katika katiba hiyo ili kuendana na uhalisia uliopo.
 
Last edited by a moderator:
Wazo zuri ila tatizo langu ni kuwa je ikitokea watu wa Zanzibar hawataki muungano hali watu wa Tanganyika wanataka Muungano, ili tatizo litatuliwaje?
hakutakuwa na sababu ya kuendelea na mchakato wala fikra za katiba ya JMT ila kuuvunja Muungano. Katika hali iliyopo leo Wazanzibar wana kila sababu ya kutoutaka Muungano kwa sababu imeeleweka kuwa serikali ya Muungano ni serikali ya Tanganyika na tumelivaa kweli koti la Muungano japo tunakataa. Tukionyesha nia la kulivua koti hilo sidhani kama hawataukubali Muungano wenye fursa sawa kwa wote.
 
Muungano ni kama mkataba wa ndoa. Ni mwanandoa mpumbavu tu atakayekubali mkataba wa changu changu ,chako chetu. Ukiona msingi wa mahusiano ni kuridhisha wakwe au ndugu ndoa hiyo usanii tu na mazowea yamebaki .Raha ya ndoa kila mwanandoa aufurahie. Kama Muungano wetu sote tunaufurahia tumeshinda, Kama mtindo wetu ni chako changu;changu changu twapigana na ukuta :Tusubiri maumivu
 
Kuna mambo mengi sana hata kama si mwanasheria wala mwanasiasa yapo ktk muungano wetu. Kama watu wa kizazi cha sasa huwezi ukasema na wakashindwa kukuhoji. Pia ukihojiwa ukashindwa kutoa majibu hakuna atakaye kufuata. Kwamazingira ya Tanzania tuliyonayo sasa serikali zitufaazo ni tatu ikigoma moja itafuata kama moja haiwezekani basi ni kukubali muungano hakuna.
 
Back
Top Bottom