Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Muundo upi wa Muungano unafaa?

  • Serikali 1

    Votes: 81 23.3%
  • Serikali 2

    Votes: 22 6.3%
  • Serikali 3

    Votes: 241 69.5%
  • Sijui

    Votes: 3 0.9%

  • Total voters
    347
  • Poll closed .
acheni upuuzi kwani muundo wa serikali2 ndo unaoifanya ccm ibaki madarakani?........,ukawa wehu tukama wehu wa majalalani na bado mmeshindwa kuwashawishi wananchi wawape nchi mmeona mkimbilie kwenye muungano na mtakufa vibudu hatuwapi nchi vichaa kiufupi imekula kwenu
l
kwanza umepiga kura yako humu jf? ucpopiga unawaangusha wenzio wa LUMUMBA. hebu angalia hapo juu kura zinavosomeka basi na nyie msiosikia ndio mnapata jibu lenu.
 
Serikali 2 ndo mpango mzima! Tukiendekeza 3 Serikali ya Muungano itakuwa haina hata ardhi (ardhi si suala la Muungano) na itakuwa ombaomba kwa nchi washirika kwa kuwa haina vyanzo vya mapato vya kwake!

Tupe sababu zako siyo za kuambiwa, hizo tumeshazisikia!!!
 
Ni kiasi gani cha fedha kitatumia kuendesha serekali hii ya 3. Nchi inashindwa hata kumaliza tatizo la madawati milioni moja na laki 3 yanayotkwa katika shule za msingi, inatoa madawati lakini moja tu kila mwaka. Tutakua tunakuza uchumi au kuudololesha? Serekali 3 is a way out f muungano, tume ingesugest 1 kila nchi ikaongozwa na waziri mkuu ningeunga mkono lakin kuongeza serekali ya tatu ni kuwaongezea mzigo watanzania. Na asilimia kubwa ya watakaobeba mzigo huu ni watu wa bara na si visiwani.
 
me binafsi nna mawazo ya serikali tatu! Lakini naona serikali tatu zinapiganiwa zaid na hiv vyama pinzani vilivyo ungana ''ukawa'' naelekea kufikiri kwamba kuungana kwa hvyo vyama ni kuunganisha sera zao pia... Na sera za chama fulani kimsingi ni mawazo yaliyojengwa toka chini na mengine yakiwa pinzani na tofauti toka chama kimoja na kingine...sasa endapo hzo serikali tatu zitapatikana na ukawa wakabahatika kuchkua nchi bila shaka kila mtu katka kundi lile atadai masuala yake yaliyokubaliwa wakat wa kuunganisha vyama yatimizwe...na kutokana na spirit ya watu na vyama vyao bila shaka kuna baadhi ya mambo hayata wezekana kirahisi na hatimaye kuvunja ukawa '' uwepo wa mahakama ya kadhi ikiwa ni kitu kimoja wapo'' kwahyo tunaopenda serikali tatu ni vema tukafikiria na huko pia ili kuona mambo yanakuaje!
 
Wadau naomba ufafanuzi juu ya umuhimu wa mfumo wa serikali tatu na hasara zake pia umuhimu na hasara za mfumo wa serikali mbili,vitu ambavyo huleta mgogoro ndani ya Bunge maalum la katiba.tafadhari naomba mnijibu nipate kuelewa.
 
Ni kiasi gani cha fedha kitatumia kuendesha serekali hii ya 3. Nchi inashindwa hata kumaliza tatizo la madawati milioni moja na laki 3 yanayotkwa katika shule za msingi, inatoa madawati lakini moja tu kila mwaka. Tutakua tunakuza uchumi au kuudololesha? Serekali 3 is a way out f muungano, tume ingesugest 1 kila nchi ikaongozwa na waziri mkuu ningeunga mkono lakin kuongeza serekali ya tatu ni kuwaongezea mzigo watanzania. Na asilimia kubwa ya watakaobeba mzigo huu ni watu wa bara na si visiwani.

Hivi hayo mabilioni yanayoibwa kila wakati, yakidhibitiwa hayatoshi kununua hayo madawati? Je hao wabunge wanaojadili mambo ya Tanganyika wakati hayawahusu (siyo ya muungano), posho wanazolipwa kwa muda huo zikiondolewa hatuwezi kila mwaka kununua idadi fulani ya madawati?
Unasema kuwa mzigo wa serikali tatu watakaoubeba ni wa-bara (watanganyika), je kwa sasa mzigo wa muungano unabebwa na nani?.
Nawashangaa sana wanaokataa serikali tatu wakati hata miundo ya vyama vyao ni wa kiserikali tatu yaani Makamu mwenyekiti Zanzibar, makamu mwenyekiti bara (Tanganyika) na mwenyekiti Taifa, hivyo hivyo kwa makatibu wakuu. Hapa tofauti ni majina tu. Waweza kusema Waziri mkuu Zanzibar (na mawaziri-serikali yake), waziri mkuu Tanganyika (na mawaziri-serikali yake), na rais wa jamhuri ya muungano.
Tusing'ang'anie jambo ambalo litafeli ndani ya muda mfupi Malalamiko ya kero za serikali 2 yamekuwapo kwa muda mrefu na hayakuweza kupata suluhisho katika mfumo huo; na mawazo kuwa suluhu ni serikali 3 yamekuwapo kwa muda mrefu licha ya kupigwa vita na watawala. Ebu tusome busara za Mwalimu wakati akijenga hoja ya kukubali mfumo wa vyama vingi licha ya kuwa vilikataliwa na asilimia 80
 
Kama tunataka kudumisha muungano basi tuwe na serikali 1 tu, mean that Zanzibar isiwe nchi bali mkoa kama mikoa mingi ila kama hiyo ni ngumu basi tuwe na serikali tatu na wala si mbili kama ccm wanavyotaka kutuaminisha.
 
Serikali moja, along with mfumo wa majimbo kama ilvyoainishwa hapa (Devolved system of govt may just be what Tanzania needs - Letters - www.theeastafrican.co.ke)
Lakini kama ni serikali tatu, basi hiyo ya muungano isiwe hafifu kama ilvyo kwenye rasimu. Kwa mfano, iwe na mamlaka ya kukusanya kodi zote za muhimu (PAYE, VAT etc).
Sababu moja inayopuuzwa lakini ni ya msingi sana, ni hilo swala la Shirikisho la Afrika Mashariki. Shirikisho la Tanzania haliwezi kuexist ndani ya Shirikisho la Afrika Mashariki (it is impossible to have a small federation within a larger one!)
 
Serikali 3 is the best option kwa upande wangu.

Serikali mbili ni kuendeleza kero za muungano na pia katiba ya Zanzibar ya sasa ni tatizo kwa muundo uliopo.

Serikali moja itakuwa vigumu ku-manage kuiendesha.
Serikali moja itakuwa ngumu kivipi? in my opinion tatu zitakuwa ngumu zaidi kumanage. nchi ni moja na serikali ni moja!
 
Kama tunataka kudumisha muungano basi tuwe na serikali 1 tu, mean that Zanzibar isiwe nchi bali mkoa kama mikoa mingi ila kama hiyo ni ngumu basi tuwe na serikali tatu na wala si mbili kama ccm wanavyotaka kutuaminisha.

Zanzibar isiwe mkoa bali iwe ni jimbo, along with mikoa mingine ambayo pia itakuwa majimbo chini ya mfumo wa serikali kama ule wa kenya au afrika kusini au uingereza!
 
Muungano ni muunganiko wa vitu viwili au zaidi na kuunda kitu Kimoja.Hivyo Serikali moja ndo jibu sahahi.
 
Articles of unio zinasema Tanzania ni moja...inabidi tuuwe mipaka Tanzania iwe moja tu
 
Napendekeza tuwe na Serikali moja ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama tulivyo na serikali za mitaa, basi Zanzibar wabaki na serikali yao ili wasipoteze historia yao.
 
Back
Top Bottom