Kura za kanda ya ziwa huwa zinatoa maamuzi makubwa kwenye uchaguzi mkuu hapa nchini. Mwaka 2010 watu wa kanda ya ziwa waliikataa CCM dhidi ya upinzani

jamani Hospitali za kata zinajengwa,shule za secondari kila kata, high school kila wilaya. barabara za juu kwa juu zinajengwa. madaraja yapo yanajengwa kila mikoa. tukubali kuongozwa na mtu yeyote ili mradi atufanyie kazi wananchi na sio kujali uimarishaji chama tuu. tupo na tunaenda vizuri sana sasa tuache kumlaumu kiongozi tulaumu wafanyakazi wasio retire imprest ambao wapo wengi sana. wewe angalia ktk mashilika ya umma kama bosi akifiwa utakuta shilika linaingia ghalama za mazishi kwa gharama kubwa sana mpaka utaona mahoteri yanakodiwa kufanya catering!
 
Ndugu yenu jiwe alikuwa na nafasi ya kuleta uchaguzi huru na haki, katiba mpya kwa sababu alikuwa mzalendo, ila tamaa ya kutaka kutawala milele ilipomuingia akaanza kuisigina katiba iliyopo na kuandaa mazingira ya kutawala milele.
 
Mgombea yeyote atakayebeba falsafa za JPM kwa dhati, ataungwa mkono na Watanzania wengi, siyo Kanda ya Ziwa pekee.
Kama Jpm alikua anakubalika na Watanzania asingeharibu uchaguzi 2020.
 
Falsafa ya huyo dhalimu ilikuwa kuteka na kushinda kwa kupita bila kupangwa. Uzuri hata majizi ya msoga line wanajua kura halali zilikuwa ni kiasi gani, na huyo dhalimu hakupata kura zozote za maana huko kanda ya ziwa mnakotishia nako wanaume.
Eti majizi ya msoga line😅😅
 
Ndio unatakiwa utambue kuwa kura za kanda ya ziwa huwa zinatoa maamuzi ya kuweka dola.

KUra hazitoi kiongozi, kwa sasa kiongozi anaamuliwa na raisi aliyeko madarakani na genge dogo lijiitalo system. Tuliona haya kwa macho yetu 2020. Subiri uone chaguzi zijazo kama zitakuwa na idadi ya kuridhisha ya wapiga.
 
Muda haudanganyi, tungoje wakati ufike. Binafsi nangojea ushindi wa kishindo.
 
Wingi wa watu na wajinga wengi
 
Falsafa ya uonevu, uuaji, upendeleo wa kanda ya ziwa ndo watanzania wataunga mkono? Labda wasukuma tu ila watanzania tumekataa falsafa zozote zile za uonevu hatuzitaki kabisa,,
Hapa umeongea [emoji106]
 
Ujinga tu, mbona 2020 alipita kwa kulazimisha na wizi wa kura? yule alikua mkabila, mbaguzi mkubwa na alikua anaenda kusambalatisha nchi kabisa. walau sasa tunapumua maana wengine tulionekana kana kwamba hatuna haki wala siyo watanzania. Mama ana nyooosha kwelikweli!
 
Ndio unatakiwa utambue kuwa kura za kanda ya ziwa huwa zinatoa maamuzi ya kuweka dola.
Kwa hiyo mtafanyaje nyie wakabila wakubwa? Mtaunda chama chenu cha kikabila muweke Rais?

Rais wa Tanzania anaamuliwa na kamati kuu ya CCM, sio kanda ya ziwa
 
Falsafa ya uonevu, uuaji, upendeleo wa kanda ya ziwa ndo watanzania wataunga mkono? Labda wasukuma tu ila watanzania tumekataa falsafa zozote zile za uonevu hatuzitaki kabisa,,

kuna mauaji mengi kama sasa?? actually sasa hakuna security kabisa watu wanauliwa hovyo kila siku na kuzingizia wamejinyonga wakat wamenyongwa!!….
tofautisha na political crack down na mauaji!!… mauaji n haya tunayoyaona leo
 
Falsafa ya huyo dhalimu ilikuwa kuteka na kushinda kwa kupita bila kupangwa. Uzuri hata majizi ya msoga line wanajua kura halali zilikuwa ni kiasi gani, na huyo dhalimu hakupata kura zozote za maana huko kanda ya ziwa mnakotishia nako wanaume.

ulikuepo katka kuhesabu na kuratibu upigaj kura!! au ndo unajitekenya na kucheka mwenyewe
 
Watake wasitake ni lazima wamchague membe au rizione kama raisi wao, eakileta fyoko tuu hicho kidaraja, ferry na lami vyoote vinahamia bagamoyo na kusini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…