Kura zingekuwa na maana, masikini asingeruhusiwa kupiga

Baada ya Mababu kuuwawa kipi kilifuata?
Acha kuendekeza Siasa ila kama unamanufaa ya moja kwa moja sio mbaya ila eti una uchungu na chama na eti uzaendo achana nayo.

Mimi mzazi wangu aliwahi kuwa kwenye moja ya hivyo vyama ile kindakindaki ila alipokufa tulirithi nguo tu mi najua nini nasema siasa dunia nzima ni mchezo wa kifala kwetu sisi wajanja mnaweza mkawa pamoja na mwanasiasa mwenye ushawishi ambaye anatingisha serikali mkapigwa kwa ajili ya maneno yake mkafa kwa kupigania sijui mabadiliko mwisho wa siku mwenzenu anafanya makubaliano na hiyo hiyo serikali anakula mkate na asali na kulipiwa bills kibao we mwenzangu unatafuta fimbo ya kutembelea na kuanza kuomba visenti.

Angalia Raila kenya DlakamA Mozambique Late Tshanglai zimbabwe nk.
 
Kama siasa haikuingizii pesa, achana nayo. Uzalendo wa bure hakuna siku hizi.
 
Kwako wewe na sio kwangu
 
Yaan ukiamua kuachana na siasa utakua unawapa ushindi walioa sababisha wew uwaze ivyo, ujue Chama kina walafi wa madaraka, mafisadi, watesaji na wasiolitakia mema taifa ila ndani ya Chama humo humo kuna wazalendo, wapenda haki wanaosimamia misingi ya sheria bila kutanguliza maslahi binafsi.

Usiogope kijana wala usikate tamaa pale unapoona mawazo yako hayaendani na uhalisia, endelea kupigana vita hata kwa kuandika humu JF kuwakumbusha watu yale maono mema unayoyatamani kuwepo kwenye ulingo wa siasa. Kiuhalisia kuna mabadiliko makubwa kwenye mifumo ya kiutawala duniani kote ndomana unaona nchi nyingi haziko sawa. Usife Moyo, piga kura, changia mijadala, elimika na elimisha ila la msingi zaidi pambana na matatizo yako binafsi..
 
Walimu ndo wamekufikisha hapo you have to give them the respect.
 
Safi kabisa kwa uzi msafi wenye ujumbe mzito.

Nyuzi kama hizi miaka hii hazipatikani hapa JF 😎.

CC Dr am 4 real PhD Monetary doctor
 
Kile unachokiona sivyo unavyokiona naomba tuishie hapo.
 
Unamdanganya mwenzio ili arudi kupoteza muda na takataka za CCM kama walivyonipotezea mimi muda wangu??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…