Kurasa tatu za Tamko rasmi la Kanisa Katoliki kuhusu kuruhusu ubatizo kwa wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja

Kurasa tatu za Tamko rasmi la Kanisa Katoliki kuhusu kuruhusu ubatizo kwa wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja

Hakuna ktiu hapa naona Mungu wanayemwamini anaenda na mabadiliko ya nyakati anabadilika. I was born in a Catholic family, sijawahi kukana wala kuhama dhehebu ila niliacha kuamini katika dhehebu langu toka nilipoanza kusoma na kujiuliza amswali ambayo hakuna ambaye aliwahi nipa majibu ya kueleweka.
Huyu papa huyu ... nahisi siku za mbele utatokea mpasuka kama wa anglican
You're not alone
 
Mimi kkkt, ila Kwa yanayoendelea duniani ninazidi kukazia msimamo wangu kua hizi dini zililetwa Kwa sababu maalumu. wanajua wao. Naamini Mungu yupo....na nitaendelea kuamini hivo ila dini hizi mhh! Swali dogo...kama Mungu ni mmoja, kwanini x aone dini ya y sio sahihi? Kwanini tunalumbana kwamba dini yangu ni Bora kuliko Yako?Israel Leo anaua hovyo wasio na hatia vitani tena makusudi na wanafurahia wazi kufanya hivo....wakristo wanaona sawa, eti Taifa la Mungu😠waislam wanateteana wao Kwa wao, wakristo wanaona haiwahusu. serious???ushetani tunaona ni sawa.😭😭😭.....DINI ZILILETWA KUTUTENGANISHA. watenganishe uwatawale period.
Dini zimeanza miaka mingi sana ila ajabu kila kinachofanyika sasa hivi tunataka kukihusisha na kuanzishwa kwa dini ambazo zilianza karne hizo.
 
Ninachokijua ni kwamba viumbe vyooote, ikiwemo mashoga, vimeumbwa na Mungu. Na hua anasema anawapenda sana.

Kingine ninachokijua ni kwamba Mungu ni mjuzi na muweza wa vyote, hivyo ukiona anaruhusu jambo fulani kuwepo, basi ujue ana sababu zake za msingi sana zisizochunguzika. Kazi ya Mungu haina makosa.

Nakubaliana na Pope Francis....
Aisee
Kijana uwe makini na mitazamo yako.
 
Wasabato wamekuwa wamchongo

Ukiwauliza wanasema wanaenda na wakati

Kuna msabato wakati naishi Buhongwa

Alikuwa ananidai kodi ya miezi mitatu,laki 180k

Nikajaribu kumpa siku ya sabato asubuhi

Nikajua atavunga,

Alizisundika mfukoni chaaap
Hahaaaa
 
Ufafanuzi kidogo, shahidi wa ndoa ni nani??

Mfano sisi tunaohudhuria kanisani wakati ndoa inafungishwa kisha swali linaulizwa kuna mtu ana pingamizi au kuna shahidi wa aina nyingine

Sooner or later, utasikia na kufungisha pia tunaruhusu

Hakika kanisa la Sabato litabaki kuwa msingi mkuu wa imani ya kweli ya Kristo maana hawa wengine sasa[emoji17]

Walianza Anglikana sasa Roma, ngoja tuone walutheri na wengineo itakuwaje
Yaani huwa nawashangaa Saba ndugu zetu nyinyi. Mbona mnapenda kujikweza sana. Kila kitu sabato sabato sabato. Kwani ulisikia FPCT au EAGT wanafanya hayo mambo ya ushoga.
Kila ajidhaniaye amesimana aangalie asianguke. Katoriki wameimba wimbo wa kanisa takatifu moja la mitume kwa miaka mingi kwa mbwe mbwe nyingi lakini angalia wanapoelekea Sasa hivi.

Huo mpasuko wao siyo mdogo na utawa cost big time. Hapo bado maaskofu wa Africa hasa Kenya, Zimbabwe na Nigeria bado hawajatoa tamko lao kuhusu huo waraka.

Usione hao wa Brazil wameanza hapo moto bado.
 
Wasabato ni suala la muda tu,

Karibu makanisa yote ya kisabato sikuhizi wanaruhusu kuchonga nywele na ndevu wakiwemo wachungaji, mabinti wanaongia kanisani wamesuka na kuvaa magauni yanaypwachoresha makalio, mapaja, hips na vifua.

haba na haba hujaza kibaba.
Wengi wanajiunga na kanisa na wanatoka katika makanisa mengine ni ngumu kuacha mazoea yao kwa wakati mmoja lakini baada ya mida wengi huendana na misingi atleast kwenye suala la mavazi, lakini mengineyo ni ngumu kuzuia issue kama kusuka, lakini so far misingi ya kanisa inazingatiwa sana
 
Kanisa katoliki kwisha habar yake.

Unacompromise na shetani kwa hoja ya neema?

Subiri muone jeuri ya ibilisi kwa kumkaribisha ndani ya familia!!

Badala ya kukemea ushoga na usagaji, kanisa linaulegezea kwa kuunormalize?
Very true, huwezi sema watu wanaoishi pamoja wanaweza kuwa baba wa ubatizo and the like,

Ni kweli, Watu wote wanaruhusiwa kuja kanisani haijalishi ni wenye maovu gani maana kuna watu wana maovu mengi sirini, lakini haihalalishi watu walioamua kabisa kuishi pamoja na inajulikana kwa jamii halafu nawe uvunge kama hujui na kuruhusu vitu kama hivyo ilhali unajua kabisa status yao
 
As long as asili yake ni kwa watu weupe haliwezi kuwa salama, ni suala la muda tu.
Asilimia kubwa ya watu weupe wanakubali ushoga
Ni misingi ya kanisa ambayo mzizi mkuu ni biblia na sio kingine ndio maana itadumu daima unless Biblia ishuke nyingine

Ni kweli, watu wote wanakaribishwa kwa Mungu haijalishi ni mashoga, wauaji, majambazi, makahaba n.k sababu Yesu anabadilisha haijalishi mtu ni mwovu kiasi gani lakini haihalalishi mtu ambae kabisa ameamua kufanya maovu na kuishi kinyume na amri ya Mungu na anajua kisha atake kuendelea kupata huduma kama hiyo unless akiri na kuachana na suala hilo kisha aendelee na ibada
 
Yaani huwa nawashangaa Saba ndugu zetu nyinyi. Mbona mnapenda kujikweza sana. Kila kitu sabato sabato sabato. Kwani ulisikia FPCT au EAGT wanafanya hayo mambo ya ushoga.
Kila ajidhaniaye amesimana aangalie asianguke. Katoriki wameimba wimbo wa kanisa takatifu moja la mitume kwa miaka mingi kwa mbwe mbwe nyingi lakini angalia wanapoelekea Sasa hivi.

Huo mpasuko wao siyo mdogo na utawa cost big time. Hapo bado maaskofu wa Africa hasa Kenya, Zimbabwe na Nigeria bado hawajatoa tamko lao kuhusu huo waraka.

Usione hao wa Brazil wameanza hapo moto bado.
Tofautisha kati ya kujikweza na kusema ukweli, nimesema kanisa lina misingi mizuri ambayo inatokana moja kwa moja na biblia

After all sio mashindano ni kuendelea kumtukuza Mungu kupitia kwa mwanawe wa pekee Yesu Kristo hivyo ubarikiwe mtumishi.
 
kanisa lilitakiwa liwe straight, kila mabadiliko yaendayo kinyume na uumbaji wa MUNGU wayapinge, kanisa kukumbatia uasi mbele za Mungu maana yake ni kuleta kizazi kijacho kitachofanya kufuru mpaka ,madhabahuni, ni kweli kanisa halipaswi kuwatenga wenye dhambi, nata Yesu alikaa na wenye dhambi, lakini hakukaa nao na kuzurura nao tu kama washkaji bali aliwahubiria habari njema, aliwabadilisha mienendo na wote wakaijua njia ya Mungu, ila kanisa halihubiri wala kukemea ndo kwanza lina bariki, unaona papa anawatambua wapenzi wawili wa jinsia moja kama mume na mke na kama wazazi badala ya kukemea uasi huo na kuwahubiria kumrudia Mungu.
na wasiwasi mpinga kristo anaweza anzia vatican, maana papa haongozwi tena na roho mtakatifu bali utashi binfsi tu unaoathiriwa na mabadiliko ya dunia, utandawazi na maadili ya kisasa, huyu papa atatupoteza.
 
Back
Top Bottom