Idugunde,
TRA na Wizara ya Fedha wanastahili pongezi kwa kutanua "
wigo" wa walipa kodi. Maana waTanzania wengi walikuwa hawapo ktk kumbukumbu za TRA hivyo waTanzania wa wachache wa kundi hili
Mamlaka ya Mapato Tanzania - Mapato ya watu binafsi ndiyo walikuwa wanabinywa.
Sisi
Tanzania tuko milioni 55, walipa kodi ni milioni 2.2 lazima tufike mahali tujiulize, kwa hiyo utaona kwamba kuna mahali tumeshindwa,” amehoji Magufuli : source :
Nukta | Sababu za Tanzania kutokuwa na mapato makubwa ya kodi
Nchi za wenzetu mabeberu kila kitu kinacholipiwa serikali lazima ikusanye kodi ili kuweza kulipia huduma za jamii, usalama, ulinzi , elimu, kujenga miundo-mbinu na kysaidia maendeleo ya kimataifa (misaada).
www.monitor.co.ug
Only 1 million Ugandans are paying taxes, says URA

Monday June 14 2021. fina01pix. The number of registered tax payers in the tax register is 1.7 million people but not all
Nchi nyingi za kiAfrika watu wake wazima wengi hawalipi kodi, mfano kwa Uganda ripoti ya mwaka 2021 mwezi Juni inaonesha watu 1,700,000 ndiyo wanalipa kodi kati ya watu 48,000,000. Hivyo watu 1.7million wanawabeba watu wa Uganda 48 millioni, mamlaka ya Ukusanyaji Kodi Uganda URA inasema hii ni asilimia ndogo sana.
Tukirejea kwetu Tanzania ni muhimu TRA na wizara ya fedha chini ya Dr. Mwigulu Nchemba watuambie ni waTanzania wangapi wachache wanaowabeba mzigo wa wengi wenzao na familia zao ili wajifahamu kuwa kodi kama hii ya kupitia voucher za simu zinawafanya na wale wengi wasiolipa kodi kushiriki kuchangia fuko la kodi ili kuwezesha mahospitali, shule, barabara, meli na treni wazitumiazo wachangie ujenzi na uendeshaji wake.
Nadhani mkoloni hakukubali watu wazima na familia zao mijini na vijijini wasilipe kodi, na ndiyo maana tunasoma na kusimuliwa kazi kubwa ya MaDC ilikuwa kukusanya kodi hadi walisaka watu vijijini na kukamata kuku na mayai ya waTanganyika wakaenda kuyapiga mnada ili kupata kodi ya kuendesha serikali alisema Mzee Stephen Masatu Wasira katika kipindi cha Zumari cha Azam TV kilichorushwa mwezi Juni 17 2021.
Hii kodi ya voucher za simu ni ya kistaarabu na isiyo na bughudha kama kodi ya kichwa kukamata kuku na mayai au kulazimishwa kwenda kuwa manamba kukata mkonge mbali na mikoa yao kwa miezi sita ili waweze kupata mshahara wa kulipia kodi ya kichwa ya Jerumani au Mwingereza kufuatana na simulizi za mababu zetu waliokuwapo enzi za utawala wa kikoloni.
Tuhahitaji kuwa kila mwaka tufahamu watanzania wangapi watu wazima wamechangia kiasi gani cha kodi moja kwa moja kufuata na vipato vyao wawe wafugaji, mama ntilie, wafanyakazi wa umma, machinga n.k na kodi hiyo inachangia asilimia ngapi ya mapato ktk GDP.
Pia makampuni ya madini, simu, viwanda n.k wamechangia kiasi gani cha kodi ya kampuni Corporate tax.
Mwisho taarifa za kodi zingine za VAT, miamala n.k ambazo siyo za moja kwa moja .
Mwisho serikali ituambie imetumia kiasi gani ktk usalama, ulinzi, elimu, afya na miundo-mbinu kwa kutumia jedwali rahisi kila mtanzania ajue kiasi gani kimetumia na hii itawapa morali watanzania kulipa kodi zaidi maana matumizi yake yapo wazi ya serikali kuu na serikali za mitaa.
Mfano wa taarifa kwa watu wa Marekani juu ya kodi yao :
These four categories—national defense, Social Security, healthcare, and interest payments—account for roughly 73% of all federal spending, as
Figure 2 shows. The remaining 27% wedge of the pie chart covers all other categories of federal government spending: international affairs; science and technology; natural resources and the environment; transportation; housing; education; income support for the poor; community and regional development; law enforcement and the judicial system; and the administrative costs of running the government.
Figure 2. Slices of Federal Spending, 2014. About 73% of government spending goes to four major areas: national defense, Social Security, healthcare, and interest payments on past borrowing. This leaves about 29% of federal spending for all other functions of the U.S. government. (Source:
https://www.whitehouse.gov/omb/budget/Historicals/)