Kuruhusu Binti yako aolewe na kizee ni ishara umedharaulika na wewe ni Maskini wa Kutupa!

Bora mabinti zangu waolewe na hao vibabu kuliko hawa vijana wapumbavu wasiojielewa.Binti anaolewa na kijana mwenzake mimba ya kwanza tu kaachwa katelekezwa na mtoto wake hakuna cha matumizi wala nini.Bora binti yangu aolewe na mbabu

😀😀

Kwani hakuna vijana Bora?
 
Wewe hujiamini na unaitumia JamiiForums kutafuta self approval. Inaonekana una mashaka na chaguzi zako za maisha na hivyo ili kutafuta faraja ni kuiaminisha akili yako kwamba wengine wanakosea ili ujione uko sahihi.

Wakati unajiona mjanja kuoa mwanamke rilka lako wapo wanaokuona bwege lakini hawakwambii kwa sababu mambo yako hayawahusu. Watu walioridhika na maisha hawana muda wa kufuatilia mambo ya wengine ambayo hayawahusu.
 
Uzi upo makini sana.Bravos!Unaruhusu vipi binti yako wa miaka 23 aolewe na mbabuko wa miaka 49? Hideous! Haiwezekani.Hiyo ni "zereu" grade one!
 

Katika hayo uliyoandika upo kundi lipi?

Nazungumzia Saikolojia, sosholojia, na nature.
Wewe unazungumzia Uhuru wako wa kutoa Maoni Jambo ambalo sio kosa.
 
Ukijadili kwa namna yoyote ile ni mbaya

Saikolojia
Sosholojia
Mofolojia
Nature
Kote zinakataa
Kababu kalikomuoa binti katamsalimiaje baba mkwe au mama mkwe?
Je,atasalimia..."mambo"?U-hali gani?Shikamoo mdogo wangu?Imekaaje?Niambie!Tikee?Bonjour petit?Au atatumia lugha mama kupooza joto la maamkizi?
 
Katika hayo uliyoandika upo kundi lipi?

Nazungumzia Saikolojia, sosholojia, na nature.
Wewe unazungumzia Uhuru wako wa kutoa Maoni Jambo ambalo sio kosa.
Ni majibu ya saikolojia yako. Kisosholojia hakuna katazo la kuoa kwa kuzingatia tofauti kubwa kiumri. Hata hivyo mzazi ana mamlaka gani kama mtoto wake ameamua? Hujaeleza kwa data ni wangapi wanaolewa na wanaume wazee na kama kuna tatizo lolote linaloathiri jamii.

Kwenye jamii ya kitanzania unakuta binti wa miaka 20 anaolewa na kijana wa miaka 20 hadi 35+ ambapo mzazi wa binti anaweza kuwa na miaka 45 hadi 50+. Hivyo hoja yako ni ya kufikirika. Haina uhalisia ingawa hawakosekani lakini si kwa kiwango kikubwa cha kufanya uketi na kuandika as if ni tatizo kwenye jamii.
 
Kwenye suala la ndoa ili uwiano wa kiuchumi na kibaiolojia uwe na balance baina ya mwanaume na mwanamke basi ni sharti mwanaume amwache mwanamke miaka mingi kidogo. Nafikiri miaka 10-20 sio mbaya.
Huyo kijana hajui ..anataka sisi above 40 tumuoe mwanamke wa age ya bi mkubwa wake.....
 
Jomba kama hutaki binti yako aolewe itabidi uolewe wewe kwa niaba yake maana sasa hakuna namna. Saa nyingine fikiri kabla ya kuandika. Kuna mada zako huwa za kipumbavu sana. Hii umeandika ujinga mtupu.
Huyu kijana utoto unamsumbua kabisa ..yaani mimi mwanaume wa miaka arobaini nikaoe mwanamke wa miaka hamsini au sitini kama mama yake!
anashindwa kufahamu mwanaume wa miaka hamsini bado ana nguvu kabisa kama ajapata mtihani wa maradhi..ila mwanamke wa miaka hamsini au arobain unakuta kashafika hata ukomo wa hedhi.
 
Umeeleweka Ambiere
 

Can you validate claim yako kwa kutumia mfano wa Celine Dion? Mimi najua familia yenye pesa sana sana, na mtoto wao akaolewa na mtu wameachana 20 years!!!

Kuna wanawake sincerely are inzo adults kwa kupenda kabisa na sio pesa baada ya kuona Kuna chance ya utulivu inaotokana na utu Uzima!

Ingawa andiko lako laweza kuwa na uhalali kwa % fulani, lakini huo mtazamo sio kwa wote, ninakataa kabisa, Mimi mke wangu wa 2 tumeachana 17 years, ni muajiriwa wa serikali, mkaguzi, ana uwezeo, sioni kwamba Kuna kitu kafuata kwangu.

Nilimuoa akiwa na miaka 26 graduate ajaanza kazi, na Mimi nilikuwa na miaka 45, akapatq kazi, Mimi nikaenda nje ya nchi kwa mda, mda, nikawa namhudumiq kiasi, akaniambia ana mpango wa kununua kiwanja, nikamruhusu.

Kanunuq, kakopa, kasimamisha Boma, nikapauq na kufanya finishing, nimerudi Tanzania, hakuna shida yeyote, maana nyuma ni kama yake na kiwanja chake ( ingawa na Mimi Nina manyumba yangu!

I see a genuine love between us!
 

Kwenye suala hili la Ndoa na Mahusiano, ni vigumu Sana kumpangia Mtu aolewe na nani au amuoe nani.

Kila MTU mzima ana maamuzi yake binafsi kuhusiana na suala hili.
Mtoto akishafikia umri wa utu Uzima basi anakuwa yupo huru kujiamulia mambo yake yeye mwenyewe bila ya kushurutishwa au kushinikizwa, wewe mzazi wake, mlezi wake au ndugu zake mnabaki kuwa Washauri tu juu ya maisha ya Mtu huyo. Binti wa umri wa miaka 20 kama yeye mwenyewe kwa ridhaa yake ataamua kuolewa na Mzee mwenye umri wa miaka 80, basi wewe mzazi wake hutakuwa na uwezo wa kumzuia endapo kama binti mwenyewe ameridhia kuolewa.
 
Kwanza Mzee yeyote Hana uwezo wa kuja kujaribu kufukuzia vibinti vyako ati avioe. Anaanzaje! Hizo ni dharau za rejareja!
Ndugu mtibeli futa kauli yako. Jacqueline Ntiyabaliwe (maarufu kama Jacqueline Mengi ) anatoka familia ya vibopa (matajiri). Lkn aliolewa na mzee Mengi (mtu mzee zaidi ya babake Jacqueline).
 
Kuna waziri wa fedha(mwanamke) nchi fulani aliwahi kumpa bosi wake mtoto wake ili amuoe na huyo bosi ni mzee.
Ni kweli kabisa. Ila sijui kama bado huo uhusiano unahusiana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…