Kuruhusu watu binafsi kuzalisha na kuuza umeme inaweza kuwa suluhisho la tatizo la umeme?

Hapa mita imeungua jana tumeambiwa mpaka Jumatatu
 
Shida ingekuwa usambazaji basi matatizo ya umeme yangekuwepo mwaka mzima. Lakini kiangazi tu kinapoingia unaona umeme unaanza kusuasua.
 
Na uzalishaji si mpaka uwe mkubwa

Kweli kabisa

Nishati Lutheran (DKK) Investment ya Ijangala, Makete Yaingiza Umeme KW360 Ktk Gridi ya Taifa​


MRADI WA UMEME KW360 WAKAMILIKA​

Wakazi 4,500 kunufaika na umeme wa gridi Makete, Njombe Tanzania. Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Nishati Lutheran (DKK) wakati wakiwasha mitambo ya umeme wa mradi huu uliokamilika.

Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Ijangala, kijiji cha Masisiwe, wilayani Makete, Mkoa wa Njombe, wakamilika .


View: https://m.youtube.com/watch?v=mqQ5NgCkdvw&
HISTORIA YA MRADI WA UMEME:

Tarehe Iliyowekwa: March 23rd, 2023




Hayo yamebainika wakati wa ziara iliyofanywa na viongozi wa juu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Janet Mbene, Machi 15 2023 mwaka huu.

Akiwa ameongozana na mmojawapo wa Wajumbe wa Bodi, Florian Haule pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy, Mwenyekiti amekiri kufurahishwa na kuridhishwa na kazi nzuri ya utekelezaji wa Mradi huo ambao REA unaotarajiwa kuzalisha kilowati 360 za umeme pindi utakapokamilika.

Pamoja na pongezi, Mwenyekiti ameeleza kuwa anaamini kukamilika kwa Mradi huo unaotekelezwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na kufadhiliwa na REA pamoja na wadau wengine, kutatoa hamasa na kuchochea makundi na asasi mbalimbali za kijamii kuiga mfano wake hivyo kuwezesha umeme vijijini kuenea kwa kasi zaidi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu REA Mhandisi Hassan Saidy amekiri kuwa imani aliyoiweka kwa Taasisi hiyo ya Kanisa na kukubali kufadhili Mradi huo haikupotea bure kwani Mradi umetekelezwa kwa wakati na viwango vilivyotarajiwa.

“Katika hali ya kawaida, unatoa hela unaogopa kidogo, lakini niliwaambia matarajio yangu ni kwamba watafanya vizuri katika utekelezaji wa mradi huu wa nishati kama ambavyo wamefanya vizuri katika sekta za elimu na afya. Nawashukuru hawajaniangusha na nimefarijika sana,” ameeleza.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Mkurugenzi Mtendaji anayesimamia Mradi huo, Mdiakonia Elikana Kitahenga pamoja na Msaidizi wa Askofu KKKT Dayosisi ya Kusini Kati, Mchungaji Mathayo Sanga, wameishukuru REA kwa ushirikiano na mchango wake mkubwa tangu kuanza utekelezaji wa Mradi huo.

Wamesema, REA imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Mradi unatekelezwa siyo tu kupitia ufadhili wa fedha bali pia kwa viongozi na wataalamu wake kutembelea Mradi huo mara kwa mara kujionea maendeleo yake.

Mradi huo utakapokamilika na kuanza uzalishaji, unatarajiwa kuuza umeme huo kwa Shirika la Umeme Tanzania ili uingizwe kwenye gridi ya Taifa ikiwa ni Mkataba maalumu baina ya pande hizo mbili.

REA, ikiwa ni taasisi inayoshughulika upelekaji nishati vijijini, hutumia mbinu mbalimbali za kutekeleza kazi hiyo ikiwemo kufadhili vikundi au hata watu binafsi wanaojihusisha na uzalishaji nishati vijijini ili kutimiza azma ya serikali inayolenga kuhakikisha maeneo ya vijijini yanafikiwa na nishati bora

 
UJUE MRADI WA UMEME WA MAJI TULILA - RUVUMA TANZANIA


Mtazame mtawa wa Shirika la Mtakatifu Agnesi Chipole Jimbo Kuu la Songea Sr.Veritas Ndumbili OSB akielezea mradi wa umeme wa maji wa Tulila ambao upo kwenye maporomoko ya maji ya mto Ruvuma ambao unamilikiwa na watawa hao.Mradi huo wenye uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati tano ndiyo uliomaliza tatizo la mgawo wa umeme katika mji wa Songea
Source : Songea TV



Chipole, Songea

DARAJA LA CHIPOLE SONGEA

Hatimaye Watawa wa Shirika la Chipole wilayani Songea wameridhia maombi ya muda mrefu ya wananchi kuruhusiwa kulitumia daraja lililokuwa limefungwa kwa zaidi ya miaka mitatu kutokana na kile kilichoelezwa na watawa hao kwamba baadhi ya wananchi walikuwa wakilitumia vibaya daraja hilo na kuhatarisha maisha yao

Source : Azam TV
 
Abasia ya Ndanda / Ndanda Abbey Mradi wa Umeme Wananchi wanufaika Nishati Saa 24 Bila Kukatika

Ndanda, Mtwara
Tanzania

Teknolojia ya umeme wa maji waokoa watu wengi mjini Ndanda mkoani Mtwara, kusini mwa Tanzania.


Source : DW KiSwahili
 
Tanesco hawataki mshindani elewa hilo Bora mkae bila umeme kuliko kutumia umeme mwingine usiokuwa wa Tanesco

Dunia inaenda kasi, this is 1970s anymore. Itabidi wakubali maana inaonekana wanashindwa ku deliver kwa viwango
 
Tatizo Mafisadi/Majizi wanatumia loophole hiyo Kupiga MAOKOTO ,yakisema waruhusu wazalishaje wa nje yatakufa NJAA.
 
Dunia inaenda kasi, this is 1970s anymore. Itabidi wakubali maana inaonekana wanashindwa ku deliver kwa viwango
Serikali ikiendesha miradi mikubwa kama hii huwaga inapinga ushindani na huo ndio mwanzo wa huduma mbovu angalia hata DART kwasababu hawana mpinzani wanajiamulia watakalo lakn kama kungekuwa na Free competition aisee Tanesco,DartDawasa zingekuwa Chali kitambo sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…