shida siyo uzalishaji, shida ni usambazaji
kimsingi demand ya umeme Tz ni ndogo kuliko supply
shida ni miundombinu ya usambazaji
imagine, ikishenya mvua, tayari ushakatika
kukiwa na upepo tayari ushakatika
mara transfoma ndogo, inakata kata fuse kila mda
mara mti limedondokea nyaya, mara nyoka kashotisha nyaya
mara nguzo kuoza na kadhia tele
Nishati Lutheran (DKK) Investment ya Ijangala, Makete Yaingiza Umeme KW360 Ktk Gridi ya Taifa
MRADI WA UMEME KW360 WAKAMILIKA
Wakazi 4,500 kunufaika na umeme wa gridi Makete, Njombe Tanzania. Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Nishati Lutheran (DKK) wakati wakiwasha mitambo ya umeme wa mradi huu uliokamilika.
Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Ijangala, kijiji cha Masisiwe, wilayani Makete, Mkoa wa Njombe, wakamilika .
Hayo yamebainika wakati wa ziara iliyofanywa na viongozi wa juu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Janet Mbene, Machi 15 2023 mwaka huu.
Akiwa ameongozana na mmojawapo wa Wajumbe wa Bodi, Florian Haule pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy, Mwenyekiti amekiri kufurahishwa na kuridhishwa na kazi nzuri ya utekelezaji wa Mradi huo ambao REA unaotarajiwa kuzalisha kilowati 360 za umeme pindi utakapokamilika.
Pamoja na pongezi, Mwenyekiti ameeleza kuwa anaamini kukamilika kwa Mradi huo unaotekelezwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na kufadhiliwa na REA pamoja na wadau wengine, kutatoa hamasa na kuchochea makundi na asasi mbalimbali za kijamii kuiga mfano wake hivyo kuwezesha umeme vijijini kuenea kwa kasi zaidi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu REA Mhandisi Hassan Saidy amekiri kuwa imani aliyoiweka kwa Taasisi hiyo ya Kanisa na kukubali kufadhili Mradi huo haikupotea bure kwani Mradi umetekelezwa kwa wakati na viwango vilivyotarajiwa.
“Katika hali ya kawaida, unatoa hela unaogopa kidogo, lakini niliwaambia matarajio yangu ni kwamba watafanya vizuri katika utekelezaji wa mradi huu wa nishati kama ambavyo wamefanya vizuri katika sekta za elimu na afya. Nawashukuru hawajaniangusha na nimefarijika sana,” ameeleza.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Mkurugenzi Mtendaji anayesimamia Mradi huo, Mdiakonia Elikana Kitahenga pamoja na Msaidizi wa Askofu KKKT Dayosisi ya Kusini Kati, Mchungaji Mathayo Sanga, wameishukuru REA kwa ushirikiano na mchango wake mkubwa tangu kuanza utekelezaji wa Mradi huo.
Wamesema, REA imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Mradi unatekelezwa siyo tu kupitia ufadhili wa fedha bali pia kwa viongozi na wataalamu wake kutembelea Mradi huo mara kwa mara kujionea maendeleo yake.
Mradi huo utakapokamilika na kuanza uzalishaji, unatarajiwa kuuza umeme huo kwa Shirika la Umeme Tanzania ili uingizwe kwenye gridi ya Taifa ikiwa ni Mkataba maalumu baina ya pande hizo mbili.
REA, ikiwa ni taasisi inayoshughulika upelekaji nishati vijijini, hutumia mbinu mbalimbali za kutekeleza kazi hiyo ikiwemo kufadhili vikundi au hata watu binafsi wanaojihusisha na uzalishaji nishati vijijini ili kutimiza azma ya serikali inayolenga kuhakikisha maeneo ya vijijini yanafikiwa na nishati bora
Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Ijangala, kijiji cha Masisiwe, wilayani Makete, Mkoa wa Njombe, uko katika hatua za mwisho kukamilika. Hayo yamebainika wakati wa ziara iliyofanywa na viongozi wa juu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakiongozwa na Mwenyek
UJUE MRADI WA UMEME WA MAJI TULILA - RUVUMA TANZANIA
Mtazame mtawa wa Shirika la Mtakatifu Agnesi Chipole Jimbo Kuu la Songea Sr.Veritas Ndumbili OSB akielezea mradi wa umeme wa maji wa Tulila ambao upo kwenye maporomoko ya maji ya mto Ruvuma ambao unamilikiwa na watawa hao.Mradi huo wenye uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati tano ndiyo uliomaliza tatizo la mgawo wa umeme katika mji wa Songea
Source : Songea TV
Chipole, Songea
DARAJA LA CHIPOLE SONGEA
Hatimaye Watawa wa Shirika la Chipole wilayani Songea wameridhia maombi ya muda mrefu ya wananchi kuruhusiwa kulitumia daraja lililokuwa limefungwa kwa zaidi ya miaka mitatu kutokana na kile kilichoelezwa na watawa hao kwamba baadhi ya wananchi walikuwa wakilitumia vibaya daraja hilo na kuhatarisha maisha yao
Serikali ikiendesha miradi mikubwa kama hii huwaga inapinga ushindani na huo ndio mwanzo wa huduma mbovu angalia hata DART kwasababu hawana mpinzani wanajiamulia watakalo lakn kama kungekuwa na Free competition aisee Tanesco,DartDawasa zingekuwa Chali kitambo sana
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.