Serikali kupitia waziri wake wa Tamisemi Mh Mchengerwa imetutangazia kusainiwa kwa mikataba ya ujenzi wa Barabara za halmashauri za jiji la DSM.
Maoni ya wananchi wengi wanaonyesha kutokuamini uhalisia wa jambo hili kwani inaonyesha ni kila mwaka kumekuwa kukitolewa ahadi nyingi ambazo zimekuwa hazitekelezwi. Wengi wanahusisha taarifa hii na suala la uchaguzi unaosubiriwa wa serikali za mitaa.
Binafisi huwa ninamuamini sana Mama yetu hasa kutokana na imani yake thabiti mbele ya mwenyezi Mungu. Ningekuwa na nafasi ya kumshauri ningemshauri yeye binafsi kutokukubali watendaji wake kutoa ahadi kwa ajili ya mafanikio ya kisiasa. Ni vema kuwaeleza ukweli wananchi.
IWAPO TAARIFA HII YA UJENZI WA BARABARA ITAKUWA NI YA KWELI NA UTEKELEZAJI WAKE UKAFANYIKA KWA WAKATI LITAKUWA NI JAMBO JEMA SANA.
ISIWE NI DANADANA, MARA SIJUI MICHAKATO, MARA UPEMBUZI YAKINIFU, MARA MKANDARASI AMESHINDWA VIGEZO HIVYO ANATAFUTWA MWINGINE. AU UKUTE WANALETA MAGARI MAWILI MATATU YA UJENZI NA KUWEKA BANGO KUUUUBWA LA UKANDARASI HALAFU INAPITA MIAKA MITATU HALI IKIWA HIVYOHIVYO.
AU INAFANYIKA KAMA BARABARA YA MBEZI MAKABE, MSAKUZI KWENDA MPIJI INAYOJENGWA KM 1 KWA KILA BAADA YA MIAKA MIWILI. YAANI MWENDO WA KOBE.