Kusajili dini ni kinyume cha Katiba ya nchi kifungu namba 19

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
Serikali haina mamlaka ya kusajili dini ni kinyume cha katiba ya nchi kifungu cha 19 hiki hapa nanukuu

19.-(1) Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imani
na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtu
kubadilisha dini au imani yake.
(2) Bila ya kuathiri sheria zinazohusika za Jamhuri ya
Muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza
dini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu ya binafsi, na
shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya
shughuli za mamlaka ya nchi

Mfano Hii dini serikali itataka kuisajili? au inamlenga nani Kwenye huo usajili?

Huyu ni yehodaya yupi ? Yule wa enzi za JPM au
 
Mi ningekuwa rais ningefuta dini zote za ajabu ajabu kama za akina masanja. Ningebaki na uislamu na ukatoliki tu
 
Haha ha kwa hiyo ungebakiza dini za watu weupe tu ulizoletewa na wakoloni wa kiarabu( Uislamu) na wakoloni wa kizungu (katoliki) , za waswahili wenzio hutaki!!! Una nywele za kizungu au kiarabu wewe mwenzetu nini?

Uwii mbavu zangu mimi wacha nicheke
 
Mi ningekuwa rais ningefuta dini zote za ajabu ajabu kama za akina masanja. Ningebaki na uislamu na ukatoliki tu
Kwa hiyo ungekuwa AYATOLLAH kiongozi mkuu wa dini kwenye nchi wakati katiba inatamka wazi kuwa serikali haina dini

Kwa hiyo ungefuta pia dini ya uhindu ungeufuta wahindi wasiabudu ngombe wanayoabudu ubaki uislamu na ukatoliki pekee!!!!! ha ha ha soma katiba kwanza

CHeki mwenyewe wahindu wakiabudu ngombe

Serikali haina mamlaka ya kusajili dini ni kinyume cha katiba ya nchi kifungu cha 19 hiki hapa nanukuu

19.-(1) Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imani
na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtu
kubadilisha dini au imani yake.
(2) Bila ya kuathiri sheria zinazohusika za Jamhuri ya
Muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza
dini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu ya binafsi, na
shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya
shughuli za mamlaka ya nchi

Mfano Hii dini serikali itataka kuisajili? au inamlenga nani Kwenye huo usajili?

Kinachosajiliwa sio dini bali ni Taasisi ya Kidini. Mf Taasisi inayomiliki Kanisa au Msikiti.

Kwa hiyo usipotoshe.
 
Waziri wa mambo ya ndani kasema wazi kwenye huo uhakiki jumuiya za kidini hazitahusika wamebadilisha

SIMBACHAWENE: MABADILIKO YA HADHI YA VYETI VYA USAJILI WA JUMUIYA KUHUSISHA JUMUIYA ZA KIJAMII PEKEE BADALA YA TAASISI ZA KIDINI _ Na Mwandishi Wetu, MOHA.
_
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema zoezi la mabadiliko ya hadhi ya Vyeti vya Usajili wa Jumuiya kutoka kuwa vya kudumu na kuwa vya kuhuishwa kila baada ya miaka 5 kwa sasa litahusisha Vyama vya Kijamii tu badala ya Taasisi za Kidini.

Awali, zoezi hili ambalo limeanza Agosti 16, 2021 lililenga kuhusisha Taasisi za Kidini na Jumuiya za Kijamii, lakini kwa sasa zoezi hili litahusisha Vyama vya Kijamii pekee hadi hapo Serikali itakapoamua Vinginevyo.

Waziri Simbachawene ameyasema hayo katika Kikao chake na Viongozi wa Mabaraza ya Kidini na Mashirikisho ya Dini mbalimbali Nchini kilichoketi jijini Dodoma leo.

“Tumeona kuwa ni vyema kwa sasa zoezi hili likahusisha Jumuiya za Kijamii 8,851 tu na halitahusisha Taasisi za Kidini, hadi pale Serikali itakapoamua vinginevyo”. Alisema Simbachawene.

Uamuzi wa Kutohusisha Taasisi za Kidini, umekuja baada ya Kikao baina Waziri wa Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi na Viongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kidini kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijijni Dodoma.

Waziri Simbachawene aliongeza kuwa, jumla ya Vyama vya Kijamii 8,851 ndizo zitakazohusishwa katika zoezi linaloendelea hivi sasa, kupitia Ofisi ya Msajili wa Jumuiya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Kwa upande wake Msajili wa Jumuiya, Emmanuel Kihampa alisema kufuatia mabadiliko hayo, Vyama vyote vya Kijamii nchini Vinaagizwa kufika katika Ofisi ya Msajili wa Jumuiya iliyopo Ghorofa ya 11 katika Jengo la Kambarage Jijini Dodoma, kwa lengo la kuhuisha usajili wake na kupatiwa vyeti vipya vya usajili.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Wailsamu Tanzania (BAKWATA), Shekhe Hamis Mataka alimshiukuru Waziri pamoja na uongozi wa Wizara kwa kukutana na viongozi wa dini katika mkutano huo.

“Leo tunafuraha, Waziri upo, Naibu Waziri, Katibu Mkuu pamoja na Msajili wetu, hii inatusaidia hata migogoro mbalimbali yakidini inayokusumbua mheshimiwa Waziri kwa kukutana huku kunakusaidia endapo itatengenezewa njia kupitia kukutana katika umoja huu,” alisema Shekhe Mtaka

Source:Wiziri Simbachawene: Usajili sasa utahusu vyama vya kijamii pekee siyo taasisi za dini
 
Serikali haina mamlaka ya kusajili dini ni kinyume cha katiba ya nchi kifungu cha 19 hiki hapa nanukuu

19.-(1) Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imani
na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtu
kubadilisha dini au imani yake.
(2) Bila ya kuathiri sheria zinazohusika za Jamhuri ya
Muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza
dini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu ya binafsi, na
shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya
shughuli za mamlaka ya nchi

Mfano Hii dini serikali itataka kuisajili? au inamlenga nani Kwenye huo usajili?

Ulikuwa mwimba mapambio hodari mnoo,ni bora kama umefika mahali umekumbwa na kichefuchefu,kwa yale ambayo mwanzo uliona hayakugusi wewe hivyo ukawa unashangilia kwa sauti kuu,tushirikishane,ni mmoja wa wanakondoo uliyeguswa na hoja ya usajili kila mi5,au kipo pia cha tozo au yapo mengine pia.?
 
Waraka mpya huo hapo Dini hazitahusika kwenye uhakiki

1629391169034.png
1629391351151.png
 
Mi ningekuwa rais ningefuta dini zote za ajabu ajabu kama za akina masanja. Ningebaki na uislamu na ukatoliki tu
Sio dini ni Madhehebu.

Kuna KKKT, Pentekoste, SABATO, Angliacan....hizi zinaendeshwa kwa mfumo shirikishi. Wana viongozi wao wanaochaguana kuendana na katiba zao.

Shida ipo huku kwa kina Mzee wa upako....Yeye ndio kila kitu, akiwaataka watu wakagaregare kwenye mafuta hakuna wa kumpinga.
 
Mi ningekuwa rais ningefuta dini zote za ajabu ajabu kama za akina masanja. Ningebaki na uislamu na ukatoliki tu
Mbona ungekoma unakutana na hawa wafuasi wa Yesu mswahili sijui ungeanzia wapi kuwafuta!!! wenyewe na Yesu wao mswahili sio myahudi

Back
Top Bottom