Muuza Kangala
JF-Expert Member
- Jul 21, 2021
- 1,242
- 4,813
Miaka ya nyuma baada ya hayati Benjamini Mkapa kuingia madarakani tulianza kusikia juu ya ukwapuaji wa pesa za umma uliofanyika. Moja ya watuhumiwa alikuwa ni Prof. Kighoma Malima ambaye alishafariki. Tukaanza kusoma kwenye magazeti kuwa alificha pesa nyiki huko Uingereza. Na baadae tuliskia serikali ilifreeze akaunti yake na kurejesha hizo pesa.
Sasa mkuu wa nchi kusimama hadharani na kutamka kuwa kuna mabil ya pesa yamefichwa China, maana yake anafahamu benki, akaunti na hata walioficha.
Serikali iyarudishe hayo mabil na wahusika walio hai wachukuliwe hatua. Zaidi ya hapo kuna lingine nyuma ya pazia.