Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yani wiki moja unadhani umeijua dar es salaam?mada ni kuwaaga ndugu zangu,
tumeishi vizuri sana, nimejifunza mengi sana, nimefarijika sana na ukarimu wenu hasa kuanzia maeneo ya tabata relini, aroma, shule, bima, magengeni, liwiti, barakuda, mangumi, sanene, chama, sheli, segerea mwisho na segerea yote kwa ujumla wake...
wacha tu nirudi nyumbani labda tutaonana siku zingine huko mbeleni, maana milima kwa milima ndio haikutani lakini binadamu tunakutana...
mniruhusu tu niende tafadhali...
na tuombeane kila lililo jema, maana hakuna jambo dogo wala jepesi...
siwakilishi kundi lolote lile la watu, hususan ulowataja wewe, ispokua naongozana, naandamana na kuambatana na wale wanaohitaji maendeleo ya kweli kiuchumi kijamii na kisiasa na walio tayari kuungana nami katika kuinuana...Jamaa anawakilisha kundi la wabunge ambao muda huu dar hapakaliki.Wanarudi mikoani kuaanda "mazingira".
nakubali mkuu,Serikali Ipo Dar Es Salaam
Kama Huamini Kaa Morogoro Ujionee
ijumaa Wanatoka Dodoma Wanakwenda Dar Es Salaam, Halafu Jumapili Wanarudi Dodoma
Dsm ni miongoni mwa miji ya hovyo kabisa kwa binadamu kuishi.Kwasabb kili kitu kinapatikana hapa, mathalani elimu, afya, biashara, usafiri n.k..
hali ya hewa ni nzuri licha ya uzito wake wakati mwingine,
kila mtaa umechangamka na utamaduni, staili na tabia yake ya maisha.
haiwezikani eti kwa siku moja tu uzunguke dar nzima uimalize kama mikoa mingine, lahasha, itakuchukua zaidi ya wiki moja kuielewa dar ni ya tofauti sana na kwingineko 🐒
sasa ni rasmi narudi nyumbani, kwa baba na mama.
asante sana wana dar es Salaam kwa ukarimu wenu, nimeishi vizuri sana nanyi na sasa naenda kuchangamana karibu zaidi na ndugu zangu, jamaa zangu marafiki zangu na wanainchi wangu huko nyumbani, mkoani kwa baba na mama mzazi.
kwa muda mrefu nimekua nikiishi dar es salaam zaidi ya eneo ninalo paswa kuwako muda wote.
Sasa ni rasmi, narudi nyumbani na nitakuwako huo 24/7 nyumbani , ofisini na field, nyote mnakaribishwa..
kunako majaaliwa baada ya 2025, Tutaonana tena wana dar es salaama.. 🐒
Thank you Dar es Salaam..
Labda huko Mkoani kwenu Orkesment ndio kunafanya unawaza maisha ya Dar 😂😂😂Kwasabb kili kitu kinapatikana hapa, mathalani elimu, afya, biashara, usafiri n.k..
hali ya hewa ni nzuri licha ya uzito wake wakati mwingine,
kila mtaa umechangamka na utamaduni, staili na tabia yake ya maisha.
haiwezikani eti kwa siku moja tu uzunguke dar nzima uimalize kama mikoa mingine, lahasha, itakuchukua zaidi ya wiki moja kuielewa dar ni ya tofauti sana na kwingineko 🐒
sasa ni rasmi narudi nyumbani, kwa baba na mama.
asante sana wana dar es Salaam kwa ukarimu wenu, nimeishi vizuri sana nanyi na sasa naenda kuchangamana karibu zaidi na ndugu zangu, jamaa zangu marafiki zangu na wanainchi wangu huko nyumbani, mkoani kwa baba na mama mzazi.
kwa muda mrefu nimekua nikiishi dar es salaam zaidi ya eneo ninalo paswa kuwako muda wote.
Sasa ni rasmi, narudi nyumbani na nitakuwako huo 24/7 nyumbani , ofisini na field, nyote mnakaribishwa..
kunako majaaliwa baada ya 2025, Tutaonana tena wana dar es salaama.. 🐒
Thank you Dar es Salaam..
😀 hapana kwakweli,Unaenda kuwadanganya kuwa umerudi rasmi kijijini, utakula nao ugali wa muhogo na migebuka[emoji23] ukipata ubunge unarudi tena Dar.
Kila la kheri kiongozi
inaweza kua kweli kwa mtazamo na maoni yako,Dsm ni miongoni mwa miji ya hovyo kabisa kwa binadamu kuishi.
It's among of the most dirtiest & unplanned towns in Africa.
Kuna msanii mmoja wa muziki wa kizazi kipya huko miaka ya nyuma aliwahi kuimba wimbo wake aliouita kwa jina la 'Mwanza ni Jiji au ZIZI ??? The same applies to Dsm.