Kusema upo upinzani kati ya Mbowe na Lissu siyo sahihi

Kusema upo upinzani kati ya Mbowe na Lissu siyo sahihi

Mbowe anaweza kusema Rais Samia anafanya kazi nzuri sana: amejenga baarabara hapa na pale na pale. Lissu anaweza kusema Rais Samia ana matatizo makubwa sana; pale na pale na pale bado hajajenga barabara. Sasa, that is just two sides of the same coin. Hawajabishana kitu chochote.

Kwa mfano jana Lissu alikuwa anasema amepata habari kwamba Sheria ya Usalama wa Taifa wanataka waibadilishe waipe nguvu zaidi TISS, waiondoe mikononi kwa Mkuchika, waipeleke kwa Rais. Mkuchika yupo Ofisi ya Rais, sasa sijui Lissu ana malalamiko gani.

Lakini nasema hakuna ugomvi kati ya Lissu na Mbowe, ni kwamba hawa Mwananchi (gazeti), they are good at amassing the facts but not good at interpreting the facts.
Usichotaka kukikubali ni kwamba kwa sasa CDM wana jambo linalowaunganisha ambalo ni Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi.

Ni matarajio yetu wananchi kwamba hata kama maudhui ya hotuba zao lazima yatofautiane lakini sisi kama wasikilizaji pia ni lazima tuone wanachopigania kwa ajili yetu kinafanana.

Lisu ni kiongozi mwandamizi wa CDM, ni msomi na Mwanasheria nguli, anao pia chawa ndani na nje ya CDM, anaposema kwamba baadhi ya content ya maridhiano ni ujinga unataka sisi wananchi tufikiri nini? Kwamba content mojawapo ni kugawana ubunge wa kupewa;

Sote tunajua kwenye maridhiano mdau muhimu ni Mbowe!! Tunaambiwa hayo makubaliano ndani ya maridhiano ni Ujinga na kukosa akili!! Unadhani haya maneno unaambiwa wewe au mimi? Anaambiwa Mbowe!!

Sasa wenye akili wanaposema hawa jamaa wawili yaani Mwenyekiti na Makamu wake hawaelewani wewe akili zako zinatazama nini?

Maridhiano ni ya Mbowe, anayeyalalamikia ni Lisu; sasa wewe unawezaje kuwaona watazamaji wajinga. Hivi wewe unayedanganya na wale wanaosikia waziwazi nani mwenye akili?

Akili ni kuuona ufa na kuuziba. Period
 
Back
Top Bottom