Kusema upo upinzani kati ya Mbowe na Lissu siyo sahihi

Usichotaka kukikubali ni kwamba kwa sasa CDM wana jambo linalowaunganisha ambalo ni Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi.

Ni matarajio yetu wananchi kwamba hata kama maudhui ya hotuba zao lazima yatofautiane lakini sisi kama wasikilizaji pia ni lazima tuone wanachopigania kwa ajili yetu kinafanana.

Lisu ni kiongozi mwandamizi wa CDM, ni msomi na Mwanasheria nguli, anao pia chawa ndani na nje ya CDM, anaposema kwamba baadhi ya content ya maridhiano ni ujinga unataka sisi wananchi tufikiri nini? Kwamba content mojawapo ni kugawana ubunge wa kupewa;

Sote tunajua kwenye maridhiano mdau muhimu ni Mbowe!! Tunaambiwa hayo makubaliano ndani ya maridhiano ni Ujinga na kukosa akili!! Unadhani haya maneno unaambiwa wewe au mimi? Anaambiwa Mbowe!!

Sasa wenye akili wanaposema hawa jamaa wawili yaani Mwenyekiti na Makamu wake hawaelewani wewe akili zako zinatazama nini?

Maridhiano ni ya Mbowe, anayeyalalamikia ni Lisu; sasa wewe unawezaje kuwaona watazamaji wajinga. Hivi wewe unayedanganya na wale wanaosikia waziwazi nani mwenye akili?

Akili ni kuuona ufa na kuuziba. Period
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…