Kushabikia Polisi kuua watuhumiwa, ni ujinga uliopitiliza

Kushabikia Polisi kuua watuhumiwa, ni ujinga uliopitiliza

Ficha UPUMBAVU wako,
Hatuna polisi vichaa nchi Hii wa kurusha rusha hovyo Kama unavotaka kutuaminisha.
Pumbavu wahed kabisa wewe...

Jinga kabisa... Mara ngapi Polisi wameua wafanyabiashara na kuchukua mali zao na huku wakidai ni majambazi?
Ndio maana nyie hamtaki tume ziundwe kuchunguza baadhi ya matukio kama haya...
 
Watanzania wengi hawajielewi ndio maana wakisikia kelele za mwizi hawaulizi hata kaiba nini wao ni kuua tu baadae ndio utasikia kwani kaiba nini? Hata mbaya wako akitaka kukutenda aseme tu mwizi umeisha. Itachukua miaka mingi kwa watanzania kujielewa acha washabikie Polisi wauaji

Kuna ujinga mwingi ambao umepitiliza kuwa upumbavu.
 
Mimi binafsi kama Mtoto wa Shule siungi mkono kabisa Polisi kuua watu, lakini kwa majambazi hasa yanayotumia silaha kuiba na kuua yauwawe tu!

Zingatia tofauti ya jambazi na mshukiwa wa ujambazi. Wawili hao ni ni mtu huyo huyo kwa polisi Tanzania na genge la mashabIki wao.
 
Pumbavu wahed kabisa wewe...

Jinga kabisa... Mara ngapi Polisi wameua wafanyabiashara na kuchukua mali zao na huku wakidai ni majambazi?
Ndio maana nyie hamtaki tume ziundwe kuchunguza baadhi ya matukio kama haya...

Achana na wajumbe hamnazo mkuu. Wa namna hiyo huwa wanapewa hifadhi ya kudumu wanako stahili.
 
Watu wengi wa tanzania bado sana kujali haki za watu wengine. Nadhani ugumu wa maisha unawafanya wasiwe na utu
Jumlisha kukosa ustaarabu,roho mbaya, malezi mabovu elimu isiyo na viwango na kukosa kumjua Mungu wa kweli
Na hapo kwenye kukosa kumjua Mungu wa kweli ndipo penye tatizo kubwa.

Mtu na akili zake timamu anaamini anaweza kumfanyia ukatili wa aina yoyote binaadamu mwenzake na isiwe kitu sababu tu ameenda kuungama kwa kiongozi wake wa dini na kiongozi anaweza kumfutia makosa yake, mwengine akeshaenda kuhiji,au kumaliza mfungo au khamsa swalawati basi anajiona Mr. Clean bila kujali kuwa Mungu anasamehe dhambi za mja na Mola wake, Ila dhambi zinazotokana na dhulma kwa mja wake, msamaha hautoki mpaka kwanza akusamehe yule mja uliemkosea/uliemdhulumu.
 
Una uhakika hawa waliouwawa wamechanja watu kama kuni?

Kwanini kama ni halali kuuwa watuhumiwa huu wigo usipanuliwe Ili kuwashughulikia wahalifu wote au hata kuidhinishwa tu kuwa halali kwa mujibu wa sheria?

Naunga mkono hoja. Wigo upanuliwe. Tuanze na ripoti ya CAG.

Wizara,Taasisi,Idara na Mashirika yote yaliotajwa, wafanyakazi wake WOTE ,kwa maana ya wote wale Shaba bila kufikishwa mahakamani wala kuchengua nani amehusika na nani hakuhusika.

Kwasababu wizi na udokozi huu unasababisha Serikali kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo ya kuwahudumia wananchi wake.
Wananchi wengi wanakufa kwa kukosa dawa hospitali, maji safi na salama yanakosekama maeneo mengi, watoto wanakosa elimu iliyo bora zaidi, tozo kandamizi kufidia huu ukwapuaji n.k.
Kama utekelezaji wa hili jambo ni gumu basi na washukiwa wa panya road wapate haki yao ya kisheria. Wakiadhibiwa waadhibiwe kwa mujibu wa Sheria iliyopo au watakayo tungiwa kama iliyopo inaonekana haikidhi haja.
 
Jumlisha kukosa ustaarabu,roho mbaya, malezi mabovu elimu isiyo na viwango na kukosa kumjua Mungu wa kweli
Na hapo kwenye kukosa kumjua Mungu wa kweli ndipo penye tatizo kubwa.

Mtu na akili zake timamu anaamini anaweza kumfanyia ukatili wa aina yoyote binaadamu mwenzake na isiwe kitu sababu tu ameenda kuungama kwa kiongozi wake wa dini na kiongozi anaweza kumfutia makosa yake, au mwengine akeshaenda kuhiji,au kumaliza mfungo au khamsa swalawati basi anajiona Mr. Clean bila kujali kuwa Mungu anasamehe dhambi za mja na Mola wake, Ila dhambi zinazotokana na dhulma kwa mja wake, msamaha hautoki mpaka kwanza akusamehe yule mja uliemkosea/uliemdhulumu.
Well said
 
Pumbavu wahed kabisa wewe...

Jinga kabisa... Mara ngapi Polisi wameua wafanyabiashara na kuchukua mali zao na huku wakidai ni majambazi?
Ndio maana nyie hamtaki tume ziundwe kuchunguza baadhi ya matukio kama haya...
Yaani panya road ni wengi sana. Wanaodhani wanapambana na panya road nao wana tabia hizo hizo
 
Ndugu yako angechinjwa ndio ungekuwa n uchungu n panya road au ulitaka waulizwe kwann wameua!?
Nimeandika mara kadhaa kuwa nami ni mhanga wa panya road. Labda nawachukia kuliko wewe. Hata hivyo sikubaliani na kinachoendelea.

Zingatia tofauti ya panya road vis a viz washukiwa wa u panya road.

Tumeambiwa panya road wanatambulika kwa macho yao. Usikute unafanana nao mkuu?

Ni hayo tu ndugu mjumbe.
 
Nimeandika mara kadhaa kuwa nanmi ni mhanga wa panya road. Labda nawachukia kuliko wewe. Hata hivyo sikubaliani na kinachoendelea.

Zingatia tofauti ya panya road vis a viz washukiwa wa u panya road.

Tumeambiwa panya road wanatambulika kwa macho yao. Usikute unafanana nao mkuu?

Ni hayo tu ndugu mjumbe.
Akili mtu wangu
 
Back
Top Bottom