sayoo
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 5,280
- 7,930
Asilimia kubwa polisi huwajua wahalifu aisee,Tusishabikie huu upumbavu wa Police kupiga risasi watuhumiwa....
Iko hivi mtu unatoka jioni kwenda dukani kununua mahitaji... Wakati unarudi nyumbani ghafla unakutana na marafiki kadhaa kijiweni... Mnasalimiana kimtaani... Oyaa mwanangu..... Ghafla defender ya Polisi hii hapa...
Mnachukuliwa kijiwe chote.. Pamoja na wapita njia wa karibu... Pamoja na wengine...
Kesho ndugu wanapigiwa simu... Flani flani njoo hospitali flani.... Ukienda unaulizwa unamjua huyu... Hapo ni morchuary.....
Jamani tusishabikie huu mchezo...
Hawa polisi wakiendelea kupata kichwa cha hongera.... Bajeti ya kununua risasi itaongezeka... Maana hawa jamaa zetu huwa hawajui kupima kwa kiasi....
Watarusha risasi vijiwe vyote.... Itakuwa ni kila mtaa rambirambi
Maana kwenye hii operation vijana wengi wamekamatwa , Mimi namfano mtaani kwetu kuna baadhi ya vijana walikamatwa lakini hakuna hata mmoja aliyeuwawa waliishia kunyolewa nywele za viduku na virasta uchwara kisha wakaachiwa