Miye ni mhanga wa panya road. Huenda nawachukia kuliko wewe. Ila si sahihi kuwauwa wao wala watuhumiwa:
Kama tunataka Katiba Mpya, Tusiionee "Haya" Haki ya awaye yote
With due respect mkuu. Mimi siungi mkono polisi kujichukulia sheria mkononi lakini nina exception.
Kama huwa unasoma posts zangu, mimi sikuwahi kumuunga mkono hayati JPM kwa mambo mengi, ila alichokifanya Kibiti niliunga mkono.
Huwa kuna hali ikifikia sheria hazifuatwi ili kutatua tatizo kwa haraka, naomba kwanza uelewe kuwa sheria zetu bado zina mapungufu mengi, mapungufu hayo yanawapa mwanya wahalifu kurudi mtaani na kuendeleza uhalifu. Hawa panya road wengi walishawahi kufikishwa mahakamani, lakini wamerudi mitaani, na wengine gerezani lakini wamerudi tena, kuendeleza uhalifu ule ule, tena kwa majigambo kwamba hakuna wa kuwafanya kitu, watu tulianza kuhisi labda wanashirikiana na baadhi ya polisi!
Sasa mkuu, katika hali kama hiyo, nini kifanyike? Unajua procedure za mahakamani. Kuna mtu ni mhalifu kabisa, na katenda uhalifu kabisa, lakini ushahidi wa kumpa hakimu unaweza ukaleta changamoto, panya road akarudi tena mtaani, unataka hivyo?
Kama kweli wewe ni mhanga wa panya road, ni lazima utumie falsafa ya Pragmatism, The end justifies the means! Matokeo ndio yahalalishe njia iliyotumika, huyo uliyemnukuu, Mwalimu Nyerere, was a pure pragmatist, aliwahi kumhukumu kunyongwa mtuhumiwa aliyemuua mkuu wa mkoa wa Iringa bila kumpeleka mahakamani.
Ni kweli kuna madhara, lakini lazima tulinganishe madhara na faida, baada tukio la september 11, marekani waliruhusu mtu anaeshukiwa kuwa gaidi kupigwa risasi on sport! Sisi ni kama nani kujidai tunajua mno haki za binadamu, na nikuambie, mtu akihisiwa ni panya road, aidha atakuwa ni mvuta bangi au mbwia unga, ni ngumu kwa mtu wa kawaida kuhisiwa!
Inaumiza sana kwenye nchi huru, watu tuishi kwa uoga na hofu, tukihofia vijana waliokataa kwa maksudi kufanya kazi halali, na kuamua kukaba.
Na kwa maelezo tajwa hapo juu, ninasema bila kumung'unya maneno, mtu yeyote atakaehisiwa ni panya road apigwe risasi mara moja. WE WANT TO STOP THIS, ONCE AND FOR ALL.